UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
NA TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD (TPL BOARD)
04/02/2013
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawataarifu wananchi wote kwamba baada ya kufanya usaili kwa waombaji uongozi wa TFF na Tanzania Premier League Board (TPL Board), Kamati imefanya maamuzi yafuatayo:
1. TANZANIA PREMIER LEAGUE BOARD
(a) Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI INAYOGOMBEWA
|
S/N0.
|
JINA
|
MWENYEKITI WA TPL BOARD
|
1.
|
Hamad Yahya Juma
|
2.
|
Yusufali Manji
| |
MAKAMU MWENYEKITI WA TPL BOARD
|
1.
|
Said Muhammad Said Abeid (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)
|
MJUMBE –KAMATI YA UENDESHAJI (Management Committee)
|
1.
|
Kazimoto Miraji Muzo
|
2.
|
Omary Khatibu Mwindadi
|
(b) Mwombaji uongozi Ndg. Christopher Peter Lunkombe hakukidhi matakwa ya Kanuni za uendeshaji za TPL Board Ibara ya 28(2) kwa kuwa cheti chake cha Elimu ya Sekondari kina utata. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imemwondoa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya uendeshaji (Management Committee) ya TPL Board.
2. SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
(a) Waombaji uongozi wafuatao wamekidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF.Kamati inawatangaza kuwa wagombea wa nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
NAFASI
|
S/No.
|
JINA
|
RAIS WA TFF
|
1.
|
Athumani Jumanne Nyamlani
|
2.
|
Jamal Emily Malinzi
| |
MAKAMU WA RAIS WA TFF
| ||
2.
|
Ramadhan Omar Nassib
| |
3.
|
Wallace Karia
| |
MJUMBE WA KAMATI YA
UTENDAJI –
Kanda ya 1 (Kagera, Geita)
| ||
1.
|
Kalilo Samson
| |
2.
|
Salum Hamis Umande Chama
| |
Kanda ya 2 (Mwanza, Mara)
|
1.
|
Jumbe Oddessa Magati
|
2.
|
Mugisha Galibona
| |
3.
|
Samwel Nyalla
| |
4.
|
Vedastus F.K Lufano
| |
Kanda ya 3 (Shinyanga, Simiyu)
|
1.
|
Epaphra Swai
|
Kanda ya 4 (Arusha, Manyara)
| ||
1.
|
Elley Simon Mbise
| |
2.
|
Omar Walii Ali
| |
Kanda ya 5 (Tabora, Kigoma)
|
1.
|
Ahmed Idd Mgoyi
|
2.
|
Yusuf Hamis Kitumbo
| |
Kanda ya 6 (Rukwa, Katavi)
| ||
1.
|
Blassy Mghube Kiondo
| |
2.
|
Seleman Bandiho Kameya (Kupitishwa kwake kutategemea matokeo ya uhakiki wa vyeti vyake)
| |
Kanda ya 7 (Iringa, Mbeya)
|
1.
|
David Samson Lugenge
|
2.
|
John Exavery M. Kiteve
| |
3.
|
Lusekelo E. Mwanjala
| |
Kanda ya 8 (Ruvuma, Njombe)
|
1.
|
James Patrick Mhagama
|
2.
|
Stanley W. D Lugenge
| |
Kanda ya 9 (Mtwara, Lindi)
|
1.
|
Athuman Kingome Kambi
|
2.
|
Francis Kumba Ndulane
| |
3.
|
Zafarani Mzee Damoder
| |
Kanda ya 10 (Dodoma, Singida)
|
1.
|
Hussein Zuberi Mwamba
|
2.
|
Stewart Ernest Masima
| |
Kanda ya 11 (Morogoro, Pwani)
| ||
1.
|
Riziki Juma Majala
| |
2.
|
Twahil Twaha Njoki
| |
Kanda ya 12 (Kilimanjaro, Tanga)
|
1.
|
Davis Elisa Mosha
|
2.
|
Khalid Abdallah Mohamed
| |
3.
|
Kusianga Mohamed Kiata
| |
Kanda ya 13 (Dar es salaam)
|
1.
|
Alex Crispine Kamuzelya
|
2.
|
Juma Abbas Pinto
| |
3.
|
Muhsin Said Balhabou
|
(b) Waombaji uongozi wafuatao hawakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewaondoa kugombea nafasi walizoomba kama ilivyoonyeshwa hapa chini:
(i) Ndg. Omary Mussa Nkwarulo anayeonba kugombea nafasi ya Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(ii) Ndg. Michael Richard Wambura anayeonba kugombea nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kuwa Ndg. Michael Wambura alifungua kesi ya madai namba 100 ya 2010 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba akiwa ni mwanachama wa Klabu ya Simba, kinyume na Katiba ya Klabu ya Simba. Kwa kufanya hivyo, Ndg. Michael Wambura alivunja Katiba ya Klabu ya Simba, alikiuka Katiba ya TFF na Katiba ya FIFA.
(iii) Pia Kamati inaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF kuhusu uchaguzi mwaka 2008 kwamba Bw. Michael R. Wambura hakukidhi matakwa ya Ibara ya 29(7) ya Katiba ya TFF na Ibara ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF haina mamlaka ya kubadilisha maamuzi yaliyofikiwa na Kamati hiyo ya Rufaa. Maamuzi hayo yanaweza tu kubadilishwa na Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo (CAS).
(iv) Ndg. Abdallah Hussein Musa anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 1 (Kagera, Geita) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(v) Ndg. Mbasha Matutu anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 3 (Shinyanga, Simiyu) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa aliingilia mchakato wa Uchaguzi kwa kushirikiana na waweka pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake.
(vi) Ndg. Charles Mugondo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 4 (Arusha, Manyara) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF kwa kuwa vyeti vyake vya Elimu ya Sekondari na cheti cha Ualimu vina utata.
(vii) Ndg. Ayubu Nyaulingo anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 3 inayotaka awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5) na pia hakukidhi Ibara ya 9(7) kwa kutokuwa na ufahamu wa kuridhisha kuhusu majukumu na wajibu wa nafasi anayoomba na uwezo wa kutekeleza majukumu na malengo ya TFF.
(viii) Ndg. Nazarius A.M Kilungeja anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 6 (Rukwa, Katavi) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa amekuwa sehemu ya migogoro ya muda mrefu mkoani Rukwa.
(ix) Ndg. Eliud Peter Mvella anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 7 (Iringa, Mbeya) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mwaminifu kwa kukiuka uamuzi wa pamoja wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu mabadiliko ya Katiba.
(x) Ndg. Farid Nahdi anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(2) na (7) kwa kuwa maelezo ya umri wake na vyeti vya elimu havikubaliani.
(xi) Ndg. Hassan Othuman Hassan anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 11 (Morogoro, Pwani) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(5) kwa kuwa hakuhudhuria usaili.
(xii) Ndg. Omary Isack Abdulkadir anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa alikaidi maagizo ya TFF ya kuahirisha uchaguzi wa chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na maagizo ya TFF kwa kuwa alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa FRAT kwa kutotimiza matakwa ya Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.
(xiii) Ndg. Shafii Kajuna Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.
3. Usaili uliofanyika kwa waombaji uongozi ulizingatia pia taarifa zilizoifikia Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia pingamizi zilizowasilishwa dhidi ya waombaji uongozi wa TFF na TPL Board.
4. Uchaguzi wa TPL Board utafanyika tarehe 22 Februari 2013, na Uchaguzi wa TFF utafanyika tarehe 24 Februari 2013 jijini Dar es salaam.
duh!!!SHAFY HUO NDO UBABAISHAJI WA SOKA LETU,
ReplyDeleteNI NGUMU SANA KULIAMINI HILO KUWA SHAFY HUJUI KANUNI ZA TFF.
SIKU ZOTE WAKWELI NA WACHAMBUZI WA MAMBO HAWATAKIWI KWENY PROGRAM YYTE INAYO ENDESHWA KISIASA NA HUISHIA KUPIGWA CHINI!!
DONT COME DOWN SHAFY ENDLEA KUPAMBAN KAKA.
BY MUSSA MAJUGWE LINDI
Hili hapa chini zengwe kabisa
ReplyDelete(xiii) Ndg. Shafii Kajuna Dauda anayeomba kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Kupitia Kanda Na. 13 (Dar es salaam) hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 9(7) kwa kuwa si mkweli: aliposhindwa kwenye uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) alipotosha umma kuhusu ushiriki wake kwenye uchaguzi huo na mchakato mzima wa uchaguzi. Pia hana ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF.
Pamoja kuruka viwanja vya Ulaya kupiga picha na wachezaji wa wachezaji wa klabu uipendayo ya Man united wamekuondoa. DRFA wakuondoe TFF tena haaaaa jamani mpeni
ReplyDeletetunasubiri majibu toka kwa Shafii Dauda kuhusu hasa hoja ya kutokuwa mkweli!
ReplyDeletehahahahahahahhahahahhhaha
DeleteHistoria inaonesha kuwa wasema kweli wote huchukiwa sana na baadhi ya watu ktk jamii,ili kuwapoteza huundiwa tuhuma na kuwaita majina mabaya ili jamii iwachukie na mwisho wao huwa mbaya..Lakini ukweli utabaki kuwapo hata km wanaosema ukwelli hawatakuwapo,.Msikate tamaa,kuweni na subira,uvumilivu na kumtegemea mungu,maana siku zote hakuna jambo lolote zuri likafanikiwa bila kupitia mitihani,,.ALUTA CONTINUA BROTHER..
ReplyDeletehiyo editing ya photo yako nimeipenda nzuri sana..
ReplyDeleteBaba Dauda wewe nijembe, mkweli mtu wa watu usie na matatizo ulichokutana nacho ni kiutuko cha kawaida hapa Bongo land usijali.
ReplyDeletesikubaliani na maamuzi hayo,wasema kweli sikuzote hawapendwi,inaonekana Shafii akipewa nafasi atakua anawaumbua viongozi wenzake kwa kua msema ukweli,tunasubiri kauli ya Shafii
ReplyDeleteKama kamati inasimamia weledi, Yusuf Manji uzoefu wa kuongoza mpira kwa miaka 5 ameupata wapi? Tunajua amekuwa mfadhili ya Yanga kwa muda mrefu lakini hakuwa kiongozi, nadhani double standard zimetawala ktk kamati hii.
ReplyDeletewamejisahau na kunatatizo la ufahamu katika kamati iliyopewa majukumu ya kuratibu upatikanaji wa viongozi wa TFF watakao simamia uukuaji wa soka TZ.
ReplyDeleteIt is paining to remove shaffii for such office made (fake) reasons but they should remember the TFF is for tanzanian.
weak people alwayz do hate the strong people,,,,,,,,,ndio maana wambura na wewe shaffii,,,,,,hamuweziiiiiii kupataaaaa wanajuaaaaa uwepo wenu TFF,,,,ni hatariiii kwaooooo,,,,,,,wale waliojiwekeaaa kaukoooo ka mpiraaaa km mtajiii wao na km mti wa embe wa uani
ReplyDeletempira fitna bongo
ReplyDeletenadhani wadau tusimtetee sana Shafi, ni vyema yeye akatuweka wazi ni vipi ameonekana si mkweli na hana ufahamu kuhusu katiba ya TFF? yeye ndiye aliyehudhuria usaili na inawezekana alichemka maeneo fulani katika kujibu hoja za usaili hivyo ni vyema akatuweka wazi hasa ni mambo gani waliyokuwa wanajadili kwenye huo usaili, vinginevyo tutakuwa tunatoa hukumu kwa ushabiki tu.
ReplyDeleteteh te teh teh, kamatiimefanya kazi nzuri kama imefanya kwa mujibu wa katiba,kuzungumzia mpira wa ulaya co kwamba unaweza kuongoza...
ReplyDeleteHii ni Hatarii yaan of all the ppo wewe ndo wanasema huna ufahamu kuhusu Katiba ya TFF na majukumu ya Kamati ya Utendaji ya TFF??????????.Kweli nabii hakubaliki nyumbani ila sishangai maana sisi hatutaki maendeleo ya soccer thats y hatutaki watendaji kazi tunataka viongozi wa posho na safari tu .Hapo ndo ujue kwa nn kina marehemu MZIRAY walichukiwa sana humo TFF....Kina gidai in TOC NOW KINA WAMBURA NA DAUDA IN TFF ETI SOCCER LIENDELEEE WAPIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
ReplyDeletehuo hufahamu wa majukumu ukoje?mbona wanafichaficha sana,waweke majukumu na katiba ya TFF watu wanunue wazisome,inamaana wanazijua wao tu?kwann wasiziweke wazi kwa wadau wote wazifahamu?mbona imekuwa siri kama mtihani wa national wazijuwe walio madarakani tu?
ReplyDeletedauda uliwaumbua sana kwenye uchaguzi wa DRFA, mimi sishangai walivyokubwaga. UONGOZI HAUKUFAI ENDELEA TU KUWA MCHAMBUZI WA SOKA LA MTANDANONI NA HADITHI ZA WACHEZAJI WA NJE.
ReplyDeleteNyie ndio walewale mkiingia kwenye uongozi mnakuwa vigeugeu.
Aaaaaaah! hizo ndo fitina za bongo ktk mpira. wakweli siku zote huundiwa mizengwe ili kuwadhibiti. ndugu yangu shaffy usikate tamaa - pigana hadi kieleweke. tupo pamoja.
ReplyDeleteAbeid, DSM
Kiufupi kilichpofanyika safari hii kamati ya Lyato ilikuwa ikijaribu kuangalia namna ya kuhakikisha kwamba viongozi wanaopita kwenye vyama vya michezo vya mikoa hawapiti kwa lengo la kukuza mpira katika maeneo husika,bali ni kuhakikisha kwamba wanaopita huko mikoani wanakuja hapa Dar kwa ajili ya kupiga kura kuwachagua viongozi w TFF na hasa wale watu wanaowahitaji kwa ajili ya kulinda maslahi yao.
ReplyDeleteDeo Lyato na kundi lake wamejitahidi sana kuhakikisha kwamba mgombea wa nafasi ya Urais Athumani Nyamlani anapita kwenye uchaguzi utakaofanyika Februari 24 mwaka huu,hili liko wazi kwa sababu kampeni kubwa zimefanyika kwenye chaguzi za mikoa ambapo mkoa wowote ambao wagombea wake walikuwa hawauingi mkono upande wao walikuwa wakifanyiwa vituko vya kila aina.
Kwa mfano kuna mikoa ambayo ilifikia hatua ya uchaguzi kuahirishwa wapigakura tayari wakiwa ndani ya ukumbieti sabau ikiwa ni wagombea kutokuwa na vigezo,hivi kama watu wamejadiliwa na kupitishwa na kamati za uchaguzi za maeneo yao na kisha TFF yenyewe chini ya Lyato kuwapitisha na kuruhusu uchaguzi ufanyike hao mambo ya hana sifa yanatoka wapi tena,mfano Mkoa wa Tabora,Ruvuma na mingine.
Hiio ni aibu kwa Lyato na kundi lake,lakini nisema tu kwamba hawa watu siku zao za kula pesa za watanzania huko TFF zinazotolewa na FIFA kisi za zaidi ya shilingi milioni 800 kila mwaka zimefikia ukingoni,kwa sababu hao wanaowategemea watapigwa chini siku ya uchaguzi.
jbvgvcg
ReplyDeleteduh jamaa ni nomaaa hawa,
ReplyDeleteAnony wa tarehe 4, 3:20pm.. Unakuwa na wivu hadi kwenye picha? Au ndio wale waleeee TFF?!! Hiyo picha ni siku ya Seattle Sounder vs Man U mechi ambayo Ngassa alicheza, siku ile Shaffih alikuwa USA.
ReplyDeleteKaka ww na Wambura you suffer from the same consequences... Kusema ukweli na kuwakosoa wenye kufanya makosa ya kijinga (TFF) Ndio kumekuponza LKN USIKATE TAMAA..
Jamii yenye akili inaona na inajua kinachoendelea
Mohamed de bebeto.
Jamani niwe mkweli kwa sasa naumia sana na mambo mengi yanayoharibu harakati za maboresho ya mfumo wa maendeleo ya nchi yetu. Tukumbuke Tanzania ni taifa kubwa lenye ongezeko kubwa la watu, na wengi wao wako wako tu mtaani, na asilimia kubwa ya hao watu wamejitupa kwenye SOKA na sio siri wanavipaji, sasa kama hakuna uongozi imara unaoweza kutoa dira ya maendeleo ya MICHEZO nchini kama sehemu ya harakati za kuwakomboa vijana ni tatizo, na sio vijana tu,nasi tumechoka kushbikia timu za wenzetu sasa tunataka yetu isonge. Ona LIGI yetu kwanza haina tija, hivi ligi kubwa kama hii jamani ni halali kweli mdhamini atoe millioni arobaini hizo kweli? Naamini kweli vizuri TFF havina nafasi,but pigana Shafii tuko nyuma yako( ila si ngumi kaka)
ReplyDeleteKukusaidia tu ndugu yangu Dauda wewe una ufahamu mzuri wa soka la Ulaya na la Tanzania, hongera sana ila ujue hii si tiketi ya kuwa kiongozi bora wa mpira wa TZ, uongozi wa mpira unataka uzalendo na weledi ambao mimi naona ndugu yangu Dauda unaukosa. Mimi siku zote huwa nakusikiliza katika kipindi cha michezo cha clouds cha saa 3.00 usiku na cha saa 7.00 mchana siku ya j2, mara nyingi ndugu yangu unakuwa hukubaliani na wenzako na kutozipa nafasi hoja za wenzako na pia kutokubaliana na mambo mengi ikiwemo kubeza juhudi za la soka la Bongo, kila chochote au jitihada zozote za kukuza soka la Bongo wewe unaona kazi bure, sasa aina ya mtu kama wewe ukiingia uongozini sidhani kama utakuwa na mchango wa kuliinua soka letu sanasana utalididimiza. Mimi nawakubali Alex Luambano na Jeff Lea kwa kiasi fulani wana uzalendo na nia ya kuinua soka letu kutokana na michango yao ya kimaendeleo, ni kweli tuko nyuma lakini nyinyi waandishi wa habari wengi wenu huwa mnakatisha tamaa wachezaji, viongozi na wapenzi wa soka la bongo kwa maoni yenu hasi yasiyo chanya, si mnajua nyie mko nyuma ya microphone na sauti zenu zinasikika nchi nzima na hata huku nje ya nchi, sasa kama zikiwa hasi zinaathari kwa soka na michezo yetu kwa ujumla. Natoa Mfano mmoja tu, siku moja ulisema hakuna ligi mbovu kama ya Tz ukazisifu ligi za Misri, DRC n.k ukawa unasema mifano hii ukiwa huna data, kwa taarifa tu hakuna ligi mbovu kama ya DRC ligi ambayo marefa wanapigwa uwanjani, ligi ambayo ina timu 8 tu zinazoshiriki, ligi ambayo timu nyingine zinagoma kucheza mechi kwa sababu ya upangaji wa matokeo na hatima yake bingwa anapatikana bila kucheza mechi zote, ligi ambayo siku zote inatoa timu za Mazembe,Vita,Lupopo na Motema Pembe hii si ligi ya maana licha ya timu 8 zinazoshiriki hakuna mpango madhubuti wa kuzipa nafasi timu ndogondogo kuingia premier ligi, sasa mimi nilishangaa data za ubora wa ligi ya DRC ulizipata wapi, hazikuwa za kweli!!! usione Mazembe wanachukua ubingwa wa Afrika ukadhani DRC wana ligi nzuri, maendeleo ya Mazembe ni juhudi binafsi za Rais wa Klabu hiyo Moise Katumbi, lakini chama cha FECOFA na ligi yao ni bomu. Nadhani ushauri wangu utakusaidia.
ReplyDeleteJohnJohn
wewe uliyetuma hii coment ni mnafiki na umetumwa...yeye sio kwamba anabeza ligi yetu anwakosoa sasa unataka akiona madudu mfano unaenda kuangalia mechi ya simba au yanga na timu kama tusker ya kenya unauziwa tiketi ya simba na jkt tena ya nyuma sana si wizi akae kimya asiseme..kama unaona huwezi kuchangia hapakufai fungua blog yako unatuchukiza sisi wachangiaji..ameonewa basi mambo mengne ni own interest
DeleteMwisho wa siku tunatakiwa tukubari kwamba hii ndiyo tanzania na hawa pia ndiyo viongozi wetu wa tanzania, tumerithishwa kutoka ktk vyama vya siasa mpaka tunaingia ktk vyama vya michezo sasa.........Mimi binafsi nilipoona ktk magazeti yaliyopita kwamba michael wambura na shaffih dauda wamepitishwa kugombea nafasi walizozihitaji sikuamini kiukweli na nikasema kabisa kwamba kweli TFF sasa wanahitaji viongozi wapya lakini niliposikia madudu waliyofanya jana kuwaengua hawa watu basi ata ile dhana ya kucheza african cup of nation imetoweka....pumnzikeni ndugu zangu na waachieni tff yao wavimbe vizuri matumbo.
ReplyDeleteWewe unayejihita JohnJohn achana na zengwe lako , na wewe inaonekana ni wale wale viogozi wabovu wa TFF,
ReplyDeleteWewe unamchukia Shafii eti hafai, eti hata kuchambua soccer anadanganya.
Mfano umesema kuna siku aliisifia league ya DRC, unasema hakuwa na data.
Wewe data zako unatwambia humu eti league ya DRC ina team 8 tu, wewe hizo data umezipata wapi au na wewe ni mjinga unaongea ongea tu hauna data, tupe link tuone hizo team 8 tu,
Ki ukweli Shafii alikuwa right, league ya DRC ni nzuri, ina team 14 kama kwetu hapa Bongo, na kama unafatilia soccer nadhani umeweza ona kwenye AFCON inayoendelea DRC walivyokuwa wanacheza.
Suala la kuiponda league ya Bongo, Shafii ktk sport extra na sport roundup yeye kama mwanamichezo hawezi kusifia league ya kibongo au wachezi wa kibongo kwa sababu hakuna walichofanya,,
Wewe unataka asifie tu hata kama kitu kibovu?
Kiongozi bora au Mwalimu bora ili apate mafanikio ni yule asiye ridhika na marks ndongo alizozipata mwanafunzi.
Usituletee ushamba wako ktk mpira, inaonekana nyie ndo wale munaoichukia MAN united kwa sababu zenu, na pia munawachukia na marefa wanaopangwa kuchezesha mechi za MAN U.
HARUFU YA UKABILA?TUMEEPUKA WATU AMBAO WANGELETA UKABILA TFF,HIVI KAMA MTU AMEONEWA SI AKATE RUFAA?,KUPONDA VIONGOZI WA SOKA LA BONGO BILA KUPENDEKEZA SULUHISHO AU MBINU ZA KULETA MAENDELEO YA SOKA NDIO UPEWE UONGOZI?MICHAEL WAMBURA KABLA HAJAINGIA KWENYE SOKA ALIKUWA KIONGOZI WA KRIKETI,KAMA KWELI ANA UCHUNGU NA MICHEZO SI ARUDI KWENYE KRIKETI?
ReplyDeleteShaffii Dauda ni nani? anajua nini katika soka? kuponda? kudanganya? kujua kila kitu? ana uwezo wa kuongoza hata timu ya mtaa?
ReplyDeleteakae atulie