Search This Blog
Monday, February 18, 2013
SUNZU KURUDI DIMBANI DHIDI YA PRISONS - KAPOMBE NJE SIKU NNE
MSHAMBULIAJI wa Simba Felix Sunzu yuko tayari kuivaa Prisons kesho, huku beki wa nguzo wa timu hiyo Shomari Kapombe alilikosa pambano hilo kutokana na kusumbuliwa na maumivu misuli.
Simba na Prisons zitakabiliana katika pambano la ligi kuu litapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza jana akiwa safarini kuelekea jijini Mbeya, Daktari wa Simba,Cosmas Kapinga alisema kuwa, Sunzu ambaye alikuwa majeruhi wa muda mrefu baada ya kuchanika nyama za paja kwa sasa yuko timamu kuchea mechi yoyote ya ushindani ikiwemo dhidi ya Prisons kama kocha wa timu hiyo Patrick Liewing ataamua..
"Sunzu amepona kabisa maumivu ya goti yaliyokuwa yanamsumbua, kilichobaki ni uamuzi wa kocha kupanga au kutompanga katika pambano la Prisons.
"Hapa tunavyozungumza tuko na Sunzu pamoja na wachezaji wengine tunaelekea Mbeya kwaajili ya mechi yetu ya Jumatano na Prisons ,"alisema Kapinga.
Akizungumzia kwa kina tatizo la Kapombe, Kapinga alisema
kuwa matokeo ya vipimo yamebaini beki huyo ana matatizo ya misuli ya paja ambayo yatamweka nje ya dimba kwa muda wa siku nne.
"Kapombe anasumbuliwa na tatizo misuli kuvuta hivyo atakuwa nje ya dimba kwa muda wa siku nne kabla ya kurejea tena uwanjani,".alisema Kapinga.
Kapombe alikumbwa na kadhia hiyo dakika za mwisho za pambano la Kombe la Klabu Bingwa Afrika baina ya Simba na Libolo lililopigwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment