Search This Blog

Monday, February 18, 2013

SIMBA YAANZA VIBAYA MICHUANO YA AFRIKA

BAO pekee lililofungwa na Joao Martins katika dakika ya 24, limeifanya CRD Libolo ya Angola kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Martins alifunga bao hilo kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Carlos Almeida kutoka wingi ya kulia. Almeida alipiga krosi hiyo mbele ya mabeki Shomari Kapombe na Mussa Mudde.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kutakiwa kupambana kufa na kupona katika mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki mbili zijazo huko nchini Angola. Simba inatakiwa kushinda si chini ya bao 1-0 au idadi yoyote ya ushindi wenye kulingana na 1-0.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu hizo zilikuwa zikishambuliana kwa zamu lakini Libolo ilionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.
Katika kipindi cha kwanza, Libolo ilizima mashambulizi mengi ya Simba huku sehemu yake ya kiungo ikionekana kuwa imara kuliko Wekundu wa Msimbazi.
Kipindi cha pili timu zote zilikianza kwa kushambuliana kwa zamu lakini kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza, lakini mipango mingi ya Simba katika idara ya kiungo haikufua dafu.
Viungo wa Simba, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Mrisho Ngassa walijitahidi kuipenya ngome ya Libolo lakini viungo wa timu hiyo Manuel Lopes, Sidnei Mariano na Dorivaldo Dias walikuwa imara kuokoa hatari zote.
Katika kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Mussa Mudde (dk 53), Haruna Chanongo (dk 66) na Haruna Moshi ‘Boban’ (dk 84) na nafasi zao kuchukuliwa na Amir Maftah, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Salum Kinje.
Kwa upande wao Libolo, waliwatoa Joao Martins (dk 72), Dario Cardoso (dk 82) na Maieco Antonio (dk 76) na nafasi zao kuchukuliwa na Andres Madrid, Nuno Silva na Henry Camara.
Hata hivyo, mabadiliko hayo hayakuweza kubadili matokeo ya mchezo huo ulioudhuriwa na mashabiki wengi kiasi.
Dakika ya 83, Boban alimpiga kiwiko beki wa Libolo, Pedro Ribeiro lakini mwamuzi hakuchukua hatua yoyote kwani hakumuona Boban akitenda kosa hilo.
Dakika ya 94, Libolo ilitawala mchezo kwa kugongeana pasi 25 ndani ya sekunde 50.

4 comments:

  1. Kila la heri wazee wa Oman mtakapokwenda Angola. Mpira si maneno bali vitendo.

    ReplyDelete
  2. KILA MWAKA KIBADILI MAKOCHA BADO TUNATAKA USHINDI WAPI NA WAPI.......... MPIRA HAUTAKI SIASA BWANA RAGE HIZO SALAM ZAKO NA JOPO LAKO. WANA SIMBA TUNAUMIA NA MADUDU YENU.

    ReplyDelete
  3. UONGOZI UNASTAHILI KUBEBA MZIGO HUU WA LAWAMA. NA IKIWEZEKANA KUUBADILI NI NJIA YA KUINUSURU TIMU. SIKUWAELEWA KWA NINI WALIINUKANA NA KUTOKA NJE WAKATI WA SUB YA BOBAN KWANI WAO NDIO WALIOMBADILI KOCHA NA NDIO WALIOFANYA USAJILI MBOVU.

    ReplyDelete
  4. Simba!...hivi hamwon kwamba manacheza bila forward!...Haruna moshi,Mwinyi kazimoto cyo forward jaman!..hawa niviungo!...tuache ubabaishaji jaman,Wachezaji jitumen.

    ReplyDelete