Afrika Kusini imeondolewa nje ya mashindano ya kuwania kombe la
mataifa ya Afrika, baada ya kulazwa magoli matatu kwa moja kupitia
mikwaju ya Penalti na Mali.
Timu
hizo mbili zilitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja katika
dakika tisini za kawaida na hata baada ya dakika zaidi thelathini
kuongezwa hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenzie na hivyo mechi
hiyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Kinyume na matarajio ya wengi, wenyeji wa
fainali hizo Afrika Kusini ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupiga mikwaju yake
na kufanikiwa kupata mkwaju wa kwanza pekee.
Mali ilijibu kwa kufunga mikwaju mitatu na
katika mkwaju wa kuamua ikiwa wataendelea, mkwaju uliopigwa na mchezaji
wa Afrika kusini ulipaa juu ya goli na hivyo kuwapa Mali ushindi bila
kupiga mkwaju zaidi.
Mali na Ghana tayari zimefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo.
Washindi wengine wawili kuamuliwa katika mechi baina ya Nigeria na Ivory Coast na Togo na Burkina Faso siku ya Jumapili.
Goli la Afrika Kusini limefungwa katika dakika ya 31 na Tokelo Rantie.
Afrika Kusini ilifuzu kucheza robo fainali ya
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiwa mshindi wa kwanza kutoka
kundi A, huku Mali wakitokea kundi B wakiwa washindi wa pili.
No comments:
Post a Comment