Search This Blog

Thursday, February 7, 2013

KILIMANJAR​O LAGER YARIDHISHW​A NA KIWANGO CHA STARS

· Yatoa pongezi kwa kuicharaza Cameroon
· Yataka mechi zaidi za kirafiki


Wadhamini wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium lager, wamesema wanarishishwa na kiwango cha timu hiyo kwa sasa hku wakiomba TFF iandae mechi nyingi za Staridi za kirafiki hapa nyumbani. Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe siku moja baada ya Stars kuicharaza Cameroon bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa katika Uwanja wa Taimu hiiifa Jijini Dar es Salaam.

“Kwa kweli tunafurahishwa na mafanikio ya timu hii tangu tuchukue udhamini mwezi Mei mwaka jana….tumeiangalia ikicheza ndani na nje na kwa kweli kikosi ni kizuri kwani kimewaletea watanzania ushindi,” alisema.

Aliwapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao kama kauli mbiu ya KIlimanajro Premium Lager inavyosema…”Sherekea kilicho chetu.
“Hawa walikuwa wanajulikana kama Simba wa Afrika lakini wameondoka wakiwa wamenyong’onyea baada ya kufungwa 1-0,” alisema.

Bw Kavishe alisema ushindi huu wa Stars umewapa nafasi nzuri ya kuendelea kuidhamini Taifa Stars ili kuwapa watanzania nafasi ya kusherekea kilicho chao kwa kupitia burudani ya mpira.



“Dhidi watanzania wanavyozidi kutuunga mkono kwa kunywa bia yetu ya Kilimanajro Premium Lager ndio sisi tunazidi kupata fedha za kuidhamini timu na kuendelea kuwapa burudani ya mpira,” alisema Kavishe.

Alisisitiza kuwa TFF inatakiwa kuandaa mechi nyingi za kirafiki hapa nyumbani  ili watanzania wazidi kuiona timu yao ikicheza.
Huu ni ushindi mnono wa pili mfululizo kwa timu ya Taifa baada ya kuichapa Zambia 1-0 Disemba mwaka jana.

Kilimanjaro Premium Lager imetoa udhamini wa zaidi ya Shilingi Bilioni 10 kwa miaka mitano. Huu ndio udhamini mkubwa kabisa wa mpira ambao umewahi kutokea Tanzania

4 comments:

  1. Thank you Stars and Kilimanjaro Premium Lager. Vijana waongeze juhudi zaidi.

    ReplyDelete
  2. acheni ujinga timu hiyo haijafanya kitu

    ReplyDelete
  3. We ndiye mjinga na umepofuka maacho.

    ReplyDelete
  4. Haijafanya k2 ulicheza ww? chezea Samagoal weye, asante kwakua mzalendo na ku2pa raha watanzania wanzako thank"s Samagoal

    ReplyDelete