Search This Blog

Monday, January 28, 2013

YANGA NA PRISONS WAINGIZA FEDHA MARA MBILI ZAIDI WALICHOINGIZA SIMBA NA LYON

Yanga na Tanzania Prisons zimeingiza mapato ya jumla ya sh. 101,016,000 katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara iliyofanyika jana (Januari 28 mwaka huu).

Mechi hiyo namba 94 ilichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Watazamaji 17,946 walikata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.

Watazamaji 16,158 kati ya hao walikata tiketi za sh. 5,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ni 98 waliokata tiketi za sh. 20,000.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 24,314,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 15,409,220.34. Asilimia 15 iliyokwenda kwenye uwanja baada ya kuondoa VAT na gharama za tiketi ni sh. 12,363,433.45.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 7,413,060.07, Kamati ya Ligi sh. 7,418,060.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,709,030.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,884,801.14.

3 comments:

  1. bado makato kwenye mapato bado ni mengi jamani

    ReplyDelete
  2. Suluisho ni vilabu kujenga viwanja vyao, itawasaidia sana. Pia hawa DRFA na FDFwatafute vyanzo vingine vya mapato, toka mwaka 47 vyanzo ni vilevile tuu.

    ReplyDelete
  3. bado mpira wetu ni magumashi matupu,sera za michezo zibadilike na ndio tutaona mabadiliko kwenye mambo mengine na hasa mapato kwa timu zinazosota uwanjani halafu zinaambulia kiasi kidogo kama hicho.

    ReplyDelete