Search This Blog

Friday, January 18, 2013

UPANGAJI MATOKEO YA MECHI KWENYE KAMARI UNAZALISHA MABILIONI YA FEDHA KWA MWAKA

Katibu mkuu wa Interpol Ronald K. Noble amesema mapato yanayotokana na upangaji wa matokeo kwenye mechi za soka yanafikia mabilioni ya fedha.
 
Pamoja na vyombo vinavyoongoza soka UEFA na FIFA, Interpol inaongoza mkutano wa siku mbili kuhusu upangaji wa matokeo kwenye soka huko mjini Rome-Italy. 

Noble alisema biashara isiyo halali ya kucheza kamari kwenye soka inayopelekea upangaji matokeo inatengeneza mabilioni ya Euro kwa mwaka, mapato ambayo ni sawa ya na kampuni kubwa duniani ya CocaCola. 

Katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke amesema njia sahihi ya kupambana na suala hili kuanzia kwenye ngazi ya chini kabisa, kwa wanasoka wa wadogo na kuwafundisha maadili mazuri ili wakue nayo na kujiepusha na mchezo huo wa upangaji wa matokeo ambao ameuita ni kirusi kwenye soka.

Mapema wiki hii makamu wa Raisi wa La Liga alisema kwamba anaamini kwenye ligi kuu ya Spain kumekuwepo na mechi nyingi zinazopangwa matokeo, huku akionya kwamba skendo iliyoikumba soka la Italia inakaribia kwenye la liga.

No comments:

Post a Comment