Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeondolewa kwenye
michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika inayoendelea
nchini Afrika Kusini, baada ya kutoka sare ya kufungana bao moja kwa
moja na Mali, katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
DRC ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia kwaju wa penalti uliopigwa na Dieumerci Mbokani.Lakini Mali ikajibu dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Mahamadou Samass.
Mali, ilihitaji sare ili ifuzu kwa robo fainali huku ikitegemea Niger ishindwe na Ghana.
Congo ambayo ilikuwa mwakilishi wa pekee wa kanda ya Afrika Mashariki na Kati katika mashindano hayo, imeyaaga bila ya kupoteza mechi yoyote.
DRC, ilitoka sare katika mechi zake za kwanza mbili na hivyo ilihitaji ushindi katika mechi hiyo ili isonge mbele.
Mali sasa imefuzu na robo fainali hizo baada ya kuzoa alama nne na inaunga na Ghana katika kundi hilo kusonga mbele baada ya ghana kuilaza Niger kwa magoli matatu kwa yai.
Kabla ya Mali ilifanya mabadiliko manne katika kikosi chake ambacho kilishindwa na Ghana na yanaonekana kuzaa matunda kwa kuwa wameonyesha mecho mzuri katika kipindi cha kwanza.
Baada ya dakika za kwanza 45, timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Mlinda lango Molla Wague, mchezaji kiungo Samba Sow na washambuliaji Mahamadou Samassa na Modibo Maiga wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji wa kwanza kumi na mmoja.
DRC ilipata bao lake kupitia kwaju wa penalti uliopigwa na Dieumerci Mbokani.
Lakini Mali ikajibu dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Mahamadou Samass.
ghanaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDelete