Mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi klabu bingwa ya Tanzania bara timu ya Simba SC ya Dar leo imeanza vizuri mbio za kuutetea ubingwa wake wa Mapinduzi kwa kuichapa Jamhuri ya Zanzibar kwa mabao 4-2 katika mchezo ulioisha hivi punde huko visiwani.
Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na kinda Haruna Athumani Chanongo aliyepiga mawili, Felix Sunzu na Shomari Kapombe wakitupia kambani goli moja kila mmoja.
Jamhuri ndio walikuwa wa kwanza kuliona goli la Simba katika robo ya kwanza ya mchezo kwa goli lilofungwa na Mfanyeje Mussa, kabla ya Simba kusawazisha katika dakika ya 27, na baadae kidogo akaongeza bao la pili kwa shuti kali. Mfanyeje tena aliwaumiza tena Simba na timu zikaenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.
Awamu ya pili ya mchezo Simba walirudi vizuri na kupata mabao mawili yaliyofungwa na Felix Sunzu na Shomari Kapombe na kuipa timu yao ushindi wa kwanza ndani ya mwaka 2013.
Mabingwa watetezi wa kombe la mapinduzi ni Azam, Simba ni mabingwa wa kombe la Urafiki.
ReplyDeleteHaya haya ya Shibori yamerudi tena, tusije tukafanya km yale ukiifunga Simba au Yanga basi we ni mzuri, tuone ya huyu Mfanyeje Mussa kwa guu lake katupia mbili nyavu za Simba.
ReplyDeleteKazi nzuri Chanongo kaza butiiiii
ReplyDeleteNi vyema Simba wakawa Serious na Mashindano haya ili wapate maandalizi kwaajili ya Ligi Kuu na hasa Mashindano ya Kimataifa (Klabu-bingwa).Waweke Kikosi kamili ili Kocha awapime.Haya mambo ya kuweka Watoto Kikosi kizima, haitawasaidia maana hao hawatacheza African Champs League au Ligi KUU.Watoto wawaingize dk 15 za mwisho ili nao wajifunze.Nilishangaa Mechi na Tusker Kenya waliweka Watoto wengi muda wote
DeleteMdau wa Soka
kwani usajili wa timu zetu siwa kukurupuka hata huyo usishangae kuona kasajiliwa kwa dau zuri kwa hayo magoli mawili tu
ReplyDeleteHongera Simba!Patrick L.na Jamhuri K. tengenezeni timu bora....Viongozi wekeni mipango ya kuwamiliki wachezaji muda mrefu ili timu izoeane.
ReplyDeleteTatizo la timu zetu si kucheza mechi nyingi za majaribio bali akili za wachezaji kushika mafunzo kwa vitendo.wengi wao wana upeo mdogo na hawako makini.na viongozi wengi nao hamna mipango endelevu wala taaluma za uongozi wa michezo.mambo ni ya kubahatisha na ndio maana soka letu haliendi juu,soka letu limezungukwa na watu wenye njaa na wasio na kazi maalumu au taaluma za michezo. Tubadilishe tamaduni wetu tusonge mbele.mpira wa soka ni biashara kubwa duniani yenye mafanikio sana tu.
ReplyDelete