Baada ya kipigo cha mara mbili mfululizo kutoka kwa timu
ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, timu ya Black Leopards ya nchini
Afrika ya Kusini, leo imepunguza machungu yake kwa kuichapa Simba ya
jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0, katika mchezo wao wa kirafiki wa
kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hata
hivyo imeelezwa kuwa kutokana na hofu Klabu ya Simba iliwachezesha
wachezaji wa timu B, jambo ambalo limewakera hadi mashabiki wa Simba
waliokuwapo uwanjani hapo leo, ambapo baadhi ya mashabiki waliohudhuria
mtanange huo uwanjani hapo walisikika wakilalama kwa kitendo hicho,
ambacho kimeelezwa kuwa ni sehemu ya hofu na dharau.
Katika
Kikosi cha simba wameonekana wachezaji wanne tu walio katika kikosi cha
kwanza cha ligi kuu. huku wachezaji wote waliobaki wakiwa ni wa kikosi
cha pili, ambao wengi wao wakiwa ni wchezaji wa kikosi cha timu B ya klabu hiyo.
Simba kupitia makamu mwenyekiti wake Godfrey Nyange Kaburu jana ilithibitisha kwamba watachezesha kikosi cha kwanza baada ya kuibuka kwa taarifa kwamba walikuwa na mpango wa kutaka kuchezesha kikosi cha pili cha timu hiyo, lakini Kaburu alizungumza kwenye Sports Xtra ya Clouds FM na kuthibitisha kwamba kikosi kilichotoka Oman ndio kitakachoshuka dimbani kupambana na Black Leopards.
Kitendo ilichokifanya Simba sio cha kiungwana kwa sababu imehairibia jina kampuni iliyoratibu mchezo huo ya Prime time promotions, ambao walitimiza kila kitu katika makubaliana yao na Simba ili wailete timu ya kwanza kucheza na Black Leopards lakini matokeo yake wakafanya kinyume na makubaliano.
Hili ndio tatizo la uongozi katika fani ya michezo.mchezo wa mpira viongozi wengi hawana taaluma ya uongozi.ni aibu kwa simba na
ReplyDeleteutategemea maendeleo gani katika klabu?.tuombeni radhi kwa dharau na ujinga wenu.
ninavyoona ni kwamba wameogopa yanga kuusoma mchezo wao maaana siku hizi bongo ni kucopy na kupaste yaani hongera simba nawewe kaka shaffi kwani waliocheza si ni simba na unasema wa timu A walikuwemo sasa shida nini ile sio ligi bwana hapakuwa na kupata point pale kama burudani hujapata basi big up mnyama hongera yanga Kibona wa chunya
ReplyDeletekiukweli inasikitisha mno, viongozi wa simba mbona hamtutendie haki mashabiki wapi simba ya oman, sasa shaffih hawa viongozi si wamekiuka mkataba na prime time promotions basi taratibu za kisheria zichukuliwe
ReplyDeleteipo wapi simba ya oman, ww kaburu mbona hututendei haki ss mashabiki na wapenzi wa simba, prime time promotions inabidi washitaki viongozi wa simba waliokiuka mkataba nanyi. shaffih na crew lako fanyeni hima muwashitaki
ReplyDeleteHII NDIYO SIMBA BWANA......NI UTAPELI KWA KWENDA MBELE....TENA MUWAAMBIE ILE HELA YA OKWI WAKATE KIDOGO WAPELEKE RAMBIRAMBI YA MAFISANGO....
ReplyDeleteHuu bado ni ukiritimba uliopo simba,hawawezi kuendelea kwa mambo kama hayo.ndio maana watu hawajitokezi kuwekeza kwenye mpira.
ReplyDeletesimba sio wastaarabu kabisa na daima hawata fanikiwa katika soka
ReplyDeletewoga tu hawana lolote!
ReplyDeleteNawaomba muendelee kuwachezesha hao yoso ligi kuu muone cha mtema kuni.Mtashuks daraja ili liwe fundisho kwa timu nyingine zenye woga wa mechi za kimataifa kama simba.
ReplyDeletePrime time na nyini muwe professional. Inawezekana vipi timu ije leo then icheze leo leo mechi ten mechi kubwa, Come on guys! Na nyinyi mnamakosa pia, mlikua kibiashara zaidi bila kufikiria upande wa pili..
ReplyDeleteMdau Mkubwa wa Simba
Uctupangie nani acheze,kwani timu mlioileta ni mbovu kama wale watoto wamewatoa jasho unafikiri ingekuaje wangekutana mmyama mwenyewe
ReplyDeleteWATU WA YANGA NAWAOMBA MREKEBISHE MAJINA YA WACHEZAJI KWENYE WEBSITE YENU.
ReplyDeleteALLY MUSTAPHA "BARTHEZ"
ONDOENI BARTHEZ WEKENI JINA HALISI.
CALVIN YONDANI "VIDIC"
ONDOENI VIDIC WEKENI JINA HALISI.
HAILETI MAANA SEHEMU KAMA HIYO KUTUMIA HAYO MAJINA.
NIPO NA MTU HAPA TENA NI MTURUKI ANASHANGAA NA KUNIULIZA HAWA NDIO MAJINA YAO HAYA?
NIKAMJIBU HAPANA WANAFANANISHWA NA HAO WATU TU.
AKAULIZA TENA HAWANA JINA LA TATU?
JIBU SINA .
NAOMBA MFIKISHE UJUMBE WANGU KWA WANAOHUSIKA NYIE WANACHAMA NA WAPENZI WA YANGA NDALA YEBOYEBO FC ACHENI UTANI KWA HILI
Kueshimu Makubaliano ni jambo la msingi sana ktk maisha, hvyo basi kwa kukiuka makubaliano SIMBA wanaonesha jinsi ambavyo hawako makini, kuanzia kwa, SAMATA(GX100), YONDANI, TWITE,REDONDO N.K SIMBA Badilikeni!
ReplyDeletewatanzania 2namatatizo xana,hii inaxababishwa na kutokuwa na viongozi ambao n watu wa michezo
ReplyDeleteWatanzania hapa ndipo tunashangaza kipi kibaya kupromoti vijana na soka lao au kuenzi ushabiki wa Simba na Yanga? Shaffih walichofanya Simba ni sahihi kwani wamewajengea uwezo vijana wao.
ReplyDeleteHawa hawa Cloudz si ndo walikua wanadai hiki kikosi B ndo SIMBA wale wengine magari ya mkaa!imekuaje tena leo mnalalamika wakati wenzenu wanakuza vipaji,au kwenye mijiheraaaa sera zenu hazitekerezeki?walichukua kombe flani wakawa habari ya mujini leo kufungwa moja matusi yote kwao,mnawafundisha nn mnaowaita tegemeo la kesho!kwamba hawaaminiki au?MJI BEHAVE KIDOGOOOO
ReplyDeleteSimba hawajafanya Kosa kufundi, Kwani kwa benchi la ufundi makini lisingeweza kukubali kutoka safari ndefu j'tano, Alhamisi wakacheza mechi kubwa tu na tena J'mosi wana mechi muhimu ya VPL! Mnao laumu inategemea kipaumbele chenu kipo wapi. Kwenye mechi ya kirafiki au Ligi kuu!!!
ReplyDeleteSioni sababu ya nyie kulalamika wakati mnajua iliyochaza ni Simba, mlitaka Simba? au wachezaji mnao wataka ninyi, acheni rongorongo hiyo ndiyo simba au kama vipi mngepanga kikosi nyinyi basi.
ReplyDeletehao watu wa michezo ni akina nani au wale wanaodai mchezaji anaweza kucheza kwa mkopo ktk klsbu moja kwa miaka sita? Shaffii tangu aumbuliwe na mzee akilimali amekuwa kasuku maana hata yanga ikijikuna tu anasifia hongereni sports extra kwa kuacha fani yenu na kuanza kuimba taarabu maana kipindi chenu cha jana mlitoa singo mpya mkiongozwa na mzaramo mwenye sauti kama redio mkulima iliyoisha betri mko kibiashara ili muiumize simba sikutegemea kama mngeongea yale mlioyaongea jana.
ReplyDeleteHamna lolote na nyie prime time coz the way mlivyo itagaza mechi ya simba sivyo mlivyofanya kwa hao nduguzenu wa kubebwa na shaffii toka mzee akilimali akulipue huna unachofanya zaidi ya kuwasifia tu hao yanga mtupangie mechi mbili ba watu wanyewe wabovu wale si bora tucheze na smba b yetu elimisheni watu msijenge majungu.
ReplyDeleteNILIKUWEPO UWANJANI NIKIONA SOKA LA AINA YAKE TOKA KWA WATOTO.WALICHEZA VIZURI MNOO KULIKO HATA HAO WAKUBWA.HEBU FIKIRIA WASOUTH WALIVYOKIMBIZWA MUDA WOTE.ILIKUWA NI BURUDANI TOSHA SANA HATA YANGA WENYEWE WALIOKUWEPO WALIKUBALI MUZIKI NA KUBAKI UWANJANI HADI MPIRA UNISHA.MIMI MWENYEWE MWANZONI NILIBOREKA NIKASEMA NITAANGALIA KIPINDI KIMOJA TU THEN NITOKE NIKAANGLIE AFCON, LAKINI NIKANOGEWA.
ReplyDeleteTATIZO LA SIMBA NIKUSHINDWA KUONA FAIDA YA MECHI HII UKIZINGATIA WANA MECHI NGUMU AFRICAN CHAMPS.WALIPASWA WAPIME KIKOSI CHAO.LAKINI PIA HEBU FIKIRIA SIMBA KAMILI WAMEINGIA JUMATONO JIONI KESH YAKE ALHAMISI WACHEZE HALAFU TENA JUMAMOSI WACHEZE LIGI!!.Hivi kwa maingira yetu hilo linawezekana?
YANGA WASIJISIFU KECHEZA NA ILE TIMU YA SA INAYOSHIKA NAFASI YA 3 TOKA MWISHO.KWA MPIRA NILIOUONA NA WATOTO WA SIMBA, HII TIMU YA BLACK LEOPARDS NI MBOVU SI YAKUJIVUNIA UKISHINDA.BORA KAIZER, ORLANDO, SS, SUNDOWS ETC
Ingekuwa Yanga ndo imefanya madudu hayo aaah shafi angelalamikaje hapa?? lakini imefanya SIMBA yake aah poa tu kwani kitu gani bwana??? sie tunawasubiri tuwaonyeshe soka
ReplyDeletewapeni vijana waonekane na sio lazima simba kuchezesha full kikosi. hao hao clauzi wanapiga kelele kwamba timu ziwape nafasi vijana sasa nashangaa kwann wamamind, ndo kawaida yenu mnataka pesa irudi mliyowaleta toka sauzi. walichokifanya simba ni pongezi kwao kwani wamewapa vijana nafasi, hatuna haja ya kuwaona waakina bobani kila siku kwani umri emeenda, tunawahitaji waakina singano.
ReplyDeleteIssue sio Timu A au Timu B kwani waandaaji walitaka nini?au tulikuwa kifedha zaidi?nashangaa kama kila siku tunasisitiza kuendeleza soka la vijana,timu imecheza kwa mseto na imewatoa jasho na burudani mmeiona,hao Chui weusi hawakuweza kutikisa nyavu wenyewe isipokuwa watu wamejifunga ila wameshambuliwa kwenda mbele huoni hii nimtimu bora ya mseto,tuache hizo na ushabiki
ReplyDelete