Search This Blog
Wednesday, January 9, 2013
SIASA ZIMEANZA KUPOTEZA MAANA YA TUZO ZA BALLON D'OR NA KIKOSI CHA FIFPro WORLD IX
Tuzo za Ballon d'Or zenyewe zimekuwa zikikosolewa sana siku za hivi karibuni. Wakati hakuna anayeweza kupinga ushindi wa Messi na washindi wa siku za nyuma, kuna suala la namna zoezi zima la kupata mshindi ndio lenye utata. Utaratibu wa upigaji kura upo kisiasa zaidi na matakwa binafsi ya wapiga kura.
Ushindani unakuwa haupo sawa kwa sababu makocha na manahodha wanawapigia kura marafiki zao wanaocheza timu za taifa na vilabu. Pia mahusiano baina ya nchi za America Kusini, Scandinavia, nchi za Uingereza siku zote zitaleta tatizo kwenye kupiga kura. Ikiwa Jack Wilshare au Joe Hart atakuwa akigombea tuzo hiyo, we unadhani England, Wales, Ireland na Scotland zitampigia kura nani?
Wengine wanaweza kusema kura zimetokana na viwango vya wachezaji kwenye michuano mikubwa kama vile Euro 2012. Lakini hili linawapa faida kubwa wachezaji wa bara la ulaya ambao wanapata nafasi ya kucheza kwenye michuano hiyo. Tatizo kama hilo pia kwenye michuano ya Copa America. Kitu kingine, wakati Blatter na Platini wamekuwa wakizijadili nchi kama England, klabu za kiingereza, na premier league kwa kutoa maoni hasi, siku zote kutakuwepo hali ya kutokueleweka inayozunguka upendeleo kwenye ligi fulani, nchi na wachezaji.
Mwisho, ni vigumu kuitetea tuzo hii ambayo wachezaji kama Thierry Henry, Maldini, Baresi, Nesta na Raul hawakuwahi kushinda. Pia inaonekana imekuwa tuzo ya wachezaji wanaocheza nafasi za ushambuliaji kila mwaka.
Timu bora ya mwaka uliopita, kama ilivyochaguliwa na kura za wanasoka wapatao 45,000 kutoka ulimwenguni kote, yote imetokana na wachezaji wanaocheza kwenye ligi kuu ya Spain La Liga, kulikuwepo na mchezaji mmoja tu wa Atletico Madrid Radamel Falcao, wengine wote wakitoka kwenye vilabu vya Real Madrid na Barcelona. Ligi kuu ya England ambayo mara nyingi imekuwa ikitajwa kuwa ndio 'ligi bora duniani' kwa wachezaji, makocha na mashabiki kutokana na ushindani mkubwa kwenye ligi na mafanikio ya vilabu kwenye champions league kwa miaka mingi sasa. Pia kutokana na mafanikio ya Bundesiliga msimu huu na uliopita kwenye UCL, wengi wanasema kwamba ligi hiyo nayo ni bora duniani. Vyovyote vile, ni jambo lisilofikirika , au la kijinga, ama la kipuuzi ama vyovyote unavyoweza kuliita kuona hakuna mchezaji yoyte kutoka kwenye Bundesiliga na EPL aliyechaguliwa kuingia kwenye FIFPro World XI.
Kila mtu ana mawazo yake na wachezaji wake anaowapenda lakini hisia za mashabiki wa soka kutoka ulimwenguni kote. Kukosekana kwa mchezaji japo mmoja wa Manchester City kumeleta mjadala sana, hasa kwa mchezaji Vincent Kompany, na Yaya Toure. Hakuna anayeweza kutetea ni vipi nahodha wa mabingwa wa England, yupo nyuma ya Gerard Pique, ambaye mafanikio makubwa binafsi yalitoka nje ya uwanja akiwa na Shakira. Alikuwa na muda mzuri wa kufarahia maisha na mtoto mzuri wa kikolombia na akakosa msimu karibia nusu msimu wa La Liga 2011-12 na alikuwa hayupo kwenye fomu nzuri wakati patna wake Carles Puyol alipopata majeruhi.
Pia ingekuwa ngumu kutetea hoja ya kikosi bora cha FIFA ambacho hakijatoa hata mchezaji mmoja aliyeshiriki kwenye fainali ya UEFA Champions League 2012. Ndio, Chelsea walikuwa na bahati nzuri kwenye mechi nyingi mpaka walipoenda kuchukua ubingwa, lakini kama Blatter na Platini wataendelea kutoitendea haki Premier League kutokana na matumizi makubwa ya fedha kama wasemavyo wakuu wao hao wa taasisi kubwa za soka duniani, na huku wakisisitza kwamba Champions League inaonyesha ubora wa kweli wa timu, basi Drogba, Cech, na Ashley Cole hawastahili kutambuliwa kwa ubora wao??? Ashley Cole anatajwa na wengi kwamba ndio beki bora wa kushoto, na huku ubingwa wa ligi ya mabingwa wa ulaya ukiwa himaya yake, kwa hakika alitakiwa kupewa nafasi mbelel ya beki wa Real Madrid Marcelo.
Kwa wengine, uchaguzi uliowashangaza zaidi ni Dani Alves kwenye beki wa upande wa kulia. Wakati wa mwanzo wa ligi msimu uliopita, mbrazili alikuwa kweli beki bora wa kulia duniani. Lakini 2012 ulikuwa mwaka m'baya zaidi kwake tangu awasili nchini Hispania, alipatwa na matatizo chini ya Guardiola na baadae akawa anawekwa benchi na Tito Vilanova. Kuwepo kwake ndani ya kikosi cha wachezaji bora wa 2012 ni ushahidi tosha wa jinsi hii timu ilivyoundwa kwa kujuana, majina yanayojulikana yaliyochaguliwa na watu ambao hawaangalii soka vizuri au walifanya kusudi tu.
Tusi la mwisho katika kikosi hiki, lilikuwa ni kukosekana kwa jina la Andrea Pirlo. Mchawi huyu wa soka wa kiitaliano atakumbukwa kwenye historia kama mmoja wa viungo bora wa kati wa muda wote, mwaka 2012 ulikuwa ndio mwaka wake bora akiiongoza Juventus kunyakua Scudetto bila kufungwa mechi hata moja, kabla ya kushinda tuzo tatu za mchezaji bora wa mechi wakati akiiongoza Italy kwenda fainali ya EURO 2012. katika msimu huu unaoendelea sasa kiwango chake bado ni maradufu.
Mwisho kabisa tuzo za Ballon d'Or zimeshapoteza maana kutokana na siasa kuingizwa kati kati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nakuunga mkono kwa asilimia mia moja, najua wengi watakuponda kwa kuona unaleta ushabiki lakini jamaa wapo bias mno sio siri...
ReplyDeleteDaah..wazungu wanasema ''you stole the words from my lips'' yaani ndo nilichokuwa nataka kusema lakini coincidentally naona umekiandalia makala,nakubaliana na wewe ''Super Soccer Pundit'' Shaffih Mwana Wa Dauda..salamu toka Tottenham
ReplyDeletesaaaaaaaafi sana coz hata mimi nililiona hilo, fifa na uefa wana bifu na FA toka wawachane kuhusu rushwa imewauma, then wanaibeba sana ligi ya spain wakati haina mvuto kiivyo ligi yenyewe ni ushindani wa timu mbili kila mwaka kama mbio za kupokeza vijiti bana mambo gani, then kweli hizo tuzo siasa, kujuana na mapenzi binafsi pasipo kuangalia mchango wa mtu ndo maana walimnyima wesley mwaka 2010 na wengine waliopita Raul, totti, etc ivi ina maaana ligi zingine hakuna wachezaji wanaocheza vizuri jamani maana kila siku spain na watu haoa hao tu... aaaah!!! jamani....
ReplyDeleteKaka co hao tu Borutia kachukua ubingwa mara 2 mfululizo,umeongea kweli
ReplyDeleteHAPO UMENENA SHAFFI MAANA HATA MIMI NILIJUA WANACHAGUA KWA MAFANIKIO KT TIMU YAKO NA TAIFA...MWAKA JANA BARCA UBINGWA HAWAJACHUKU ARGENTINA HATA UBINGWA WA AMERIKA HAWAJACHUKU SASA MWAKA 2012 MESSI KAFANYA NINI..? CHENGA ZAKE NA MAGOLI...?
ReplyDeleteBLATTER KACHOKA KATIKA ILE NAFASI....IMENISHANGAZA HATA KUTETEA UBAGUZI WA RANGI KWA KUPONDA UAMUZI WA BOATENG...!! IT IS A RAL SHAME TO BLATTER AND FELLOWS AT ZURICH...!!
AHSANTE KA DAUDA
ReplyDeleteKA
nakubaliana na wewe kaka shaffih.
ReplyDeletelakini naomba nitoe ushauri binafsi kwako. mimi ni mpenzi mkubwa wa blog yako. na kwa kweli kila siku huwa ninaanza siku yangu kwa kupita kwenye blog yako. sasa kaka, jaribu kuweka na mawazo yako basi. mambo yamebadilika sasa. wakati mwingine pitia kwenye vyanzo vingine vya habari, which is good and come with something different. ongeza ladha zako. usifanye ile copy and paste. kidogo napata shida mimi kama mshabiki wako kukutana na taarifa iliyotafsirirwa kaka.
ni mtazamo tu. kwa sababu mara nyingi ndivyo unavyofanya na mfano ni hii taarifa. kila kitu umekitafsiri kutoka kwenye kiingereza ukaleta kiswahili, sasa dah, unanionea mimi shabiki wako ambaye tayari nilishakutana na habari hii KULEEEEEE...
mwisho wa yote. keep it up bro.. tuko pamoja!
kaka mimi nilikuwa mmoja wa watu nao kuheshimu nakuona kama unaleta mabadiliko kwenye uchambuzi wa soka hapa bonga lkn na kadri siku zinavyozidi kusonga mbele na wewe unazidi kuangukia kwa wale waandishi(wachambuzi) wetu ambao wanaandika kile wanacho ona kitatufurahisha sisi wasomaji na sio ukweli wa mambo. katika suala la kupigia kura marafiki zao kama unavyodai basi ronalda ama iniesta akashinda iyo tuzo mana mi naamini ulaya inawapiga kura wengi katika hii tuzo na wote hao ni wa huko tena wanaundugu(spain n portugal. umezunguzia suala la kina maldini baresi na wengineo kutokushinda lkn huweka walikuwa wanashindania hii tuzo na kina nani ili watu wajue uwezo wa hao wengine kupima kama kweli hawakusitahili.tukija kwa messi kushinda hii tuzo mi naona alistahili kutokana na watu aliongia nao fainali (iniesta na ronaldo) tukianza na iniesta sawa kashinda euro mwaka jana lkn je mchango ktk ushindi wa spain ni mkubwa ivo?sijui kama umenielewa let me put it this way kama iniesta angekuwa kaumia je spain wasinge shinda kikombe? jibu unalo na ukizingatia jinsi spain wanavyocheza kitimu mata au silva wanafiti na huwezi kuona pengo kama ingetokea iniesta hayupo...mtu pekee ambaye mimi kwa mtazamo wangu alistahiki kuingia tatu bora ni pirlo mana kwenye euro yeye ndio alikuwa anaiendesha italia na hata kwenye timu ya juve pia ni ivoivo.
ReplyDeleteso iyo notion ya siasa mi sizani kama ipo unless na wewe umeanza kuingia kwenye lile kundi la watu wa "MPIRA"
Huu ni ujinga,mi ni shabik wa Arsenal bt kuna m2 km Ashley Cole,Drogba,Lahm,Pirlo,Chielin walistahili kuwemo coz walifanya mambo makubwa last season.Toa Marcelo,Alves,Pique,Alonso na Falcao tia wale kwa nafas zao.John Mwakalebela Dsm.
ReplyDeleteahahahahaha falcao ana nini kujumuishwa? inanitia wasiwasi saaaaaaaaaaaaaana drogba kachukua uefa, na fa na kufika fainali za africa japo hakuchukua falcao???????? ahahaha. pirlo unawezaje kumuacha ? ana ubingwa wa italy ana final ya euro ana kiwango bora. ahahaha dani alves??????????wat hasa? kombe la mfalme?
ReplyDeleteblatter na mshikaji wake platin ambaye anaandaliwa wanaharibu mambo epl itabaki kuwa super league above all
Ubaguzi haukuanza jana kaka,hadi leo huwa siamini kama kwel mkali Henry hakuwahi kutwaa tuzo hii!!! Umeongea kiprofessionally zaidi, big up sana!!
ReplyDeleteUkweli mtupu kaka Shaffih...hapo umenena! nakubaliana na ww kwa 100%....Upendeleo wa wazi kbs...Its laughable kuona Pique yupo kwenye kikosi bora cha FIFA wakati Kompany akikosekana..Its also ridculous kuona kiungo alie kwenye kiwango bora kbs kama Toure au Pirlo..hawapo..Ni upuuzi, upuuzi mtupu...
ReplyDelete,m naona hz tuzo zpo kishabiki sana siku hizi, sababu kuna wachezaji wengi m nilitaraji watakuwepo ila hawapo, na hata ushindi wa tuzo hii hapo nyuma tuliambiwa unatokana na mafanikio aliyopata mchezaji msimu ulioisha na sio magoli au jina lake ila sasa ni kinyume. Tuanze na kikosi, beki wa kulia wa Bayern ALABA alistahili kuwepo kwenye kikosi kutokana na ulichofanya msimu uliopita, pia kuna mabeki wakati wa BORUSIA mmoja wapo alistahili kuwepo kutokana nakiwango walichoonesha pia hata Kompany, ashley cole pembeni kushoto. Kwenye viungo cjui wamemuacha kwa sababu zipi SILVA wa man city, na mwisho ni DROGBA kwa falcao. pia M nakubali uwezo wa messi ila ki halali washindi wa tuzo hii kwa mwaka huu walipaswa kuwa aidha RONALDO, CASILLAS AU INIESTA.
ReplyDeleteHapo hakuna cha ushabiki au la, Shaffii unachoongea ni kweli. Haiwezekana hata siku moja na wala haingii akilini wachezaji 11 bora wa dunia watoke katika ligi ya spain. It cant be, nooo and big nooo!!!!!!!!!!!!1
ReplyDeleteKaka dauda!tusiwe watu wa kufuata upepo,especially mwingereza akikosoa nasi tujiunge nao,cos FA always wanabeef na FIFA,so kila kitu wanakosoa,so hizi kura ni world wide za member yeyote wa FIFA,so nashangaa people kukata maoni ya wengi.izi issue ni kama issue ya Pele & Maradona,leo ppl wanaamini Maradona mkali kuliko Pele but since Maradona ni adui wa England,leo hii ukweli wanaupindisha,so kila kitu wanachokichukia ndicho wanachotaka Dunia ikubali ,tell them "u can't cheat ppl 4 the whole time"now kila kitu open.mdau NGARIBA CHODER
ReplyDeleteBAADHI MNAENDELEZA USHABIKI...KINACHOULIZWA HAPO KWANZA NI KIGEZO GANI KIMEWAPELEKA HAO WACHEZAJI WATU KWENYE FAINALI UKAMWACHA MFANI DROGBA ALIYEKUWA NA MAFANIKO KWENYE TIMU YA TAIFA NA HATA CLUB YAKE...?
ReplyDeleteAM TELLING BLATTER IS TIRED THERE....PIA KAIFANYA FIFA NI TAASISI MUNGU ISIYOHOJIWA YENYEWE NI MAHABUSU NA YENYEWE NI MAHAKAMA NA YENYEWE NI HAKIMU...!!
Dah jamani bc hata mchezaji mmoja w chelsea hawajaingiza FIFA team, wamechukua FAcup n champions league kombe lipi wanataka wachukue ili wangewashawishi kuwaingiza sidhani kama kuna zaidi ya UCL, hawajafanya fair european champion kutotoa mchezaji, nadhani DROGBA alipaswa hawepo kafunga goli facup n UCL magoli muhimu kabisa.mie bado cjaelewa vigezo walizotoa kwa kuwachagua hao wachezaji,inamana LA LIGA kubwa kuliko CHAMPIONS LEAGUE
ReplyDeleteduuuu yaani hata huyo MESSI anabebwa
ReplyDeleteKweli kabisa
ReplyDeletedrogba asingeweza unless umchomoe falcao.chomoa pique weka kompany chomoa alonso weka pirlo km 1st eleven ya euro
ReplyDeleteHakuna washambuliaj hatari sahv duniani zaidi ya Messi, Ronaldo na Falcao yaani hapa hapana ubishi,
ReplyDeleteKtk kiungo PIRLO angetakiwa kuchukua nafac ya Alonso, ktk beki Kompany badala ya Wakawaka, A> Cole badala ya , na Lahm kwa Alves!!
but
Mh! Hongereni na poleni kwa maoni yenu. Swali langu ni kwamba, mlitaka FIFA iwaelekeze wapiga kura wawachague wachezaji wa Chelsea mnaowataka au mlipenda baada ya kura kupigwa FIFA wachakachue matokeo ili kukidhi matakwa ya soka la England ambalo mnaaminishwa kuwa ati ni bora duniani?
ReplyDeleteTHE ONLY REASONS WHY rONALDO CAN NEVER WIN THE BALLON D'OR IS MESSI
ReplyDeleteAnaepinga Messi kupewa tuzo basi ana kasoro.Messi ni bora na mchezaji wa karne,hii tuzo haitolewi eti kila mchezaji apate ila inatolewa kwa mchezaji bora wa kipindi hicho.Kama Messi yupo bora basi tumpe haki yake hata kama mara 1000.
ReplyDeleteWakati EPL ina mvuto La liga ni bora na ina timu bora ambazo huwezi kuzifananisha na timu zenu za kuuza sura.Barca na Madrid ni bora zaidi ndo mana zinatamba lakini kuna timu nzuri sana kuliko hata hizo Man U ,Chelsea zenu mnazozizipia kelele.Luna Valencia,Atletico Madrid n.k ,Msikalili
acha ushamba wewe ligi haiwez kuwa bora kwa timu mbili peke yke, aende uingereza huyo messi wako km hujamchukia
Deletewahaya wanasema " wamara" meaning umemaliza yote....yani siongezei chochote/upo sahihi kabisa tuzo zimeingiliwa kisiasa zaidi! its Kashaga wa kashaga
ReplyDeleteDah... inasikitisha kuona kasumba za England zinaharibu mitazamo ya wengi duniani akiwamo Shaffih na wachangiaji wake wengi wasiofuatilia ukweli wa mambo. Jambo likiwakera Waingereza, nao wanakereka bila hata kuchunguza ukweli. Ni hivi, Blatter na FIFA hawahusiki moja kwa moja kutangaza 'World XI' au mshindi wa Ballon d'Or. Wao ni organizer tu. Wahusika wakuu ni Shirikisho la Wanasoka wa Kulipwa Duniani (FIFPro). Hii FIFPro, mabosi wake ni pamoja na rais Leonardo Grosso (Muitalia), makamu wa rais Philippe Piat (Mfaransa) na katibu mkuu Theo van Seggelen (Mholanzi). Utaratibu wa FIFPro katika kuchagua kikosi cha Wordl XI huwahusisha wanasoka wote wa kulipwa duniani. Kikosi cha hivi juzi kwa mfano, kilitokana na kura za wachezaji zaidi ya 55,000 duniani kote na mwisho wa siku, waliovuna kura nyingi ndiyo hao waliotajwa. Utaratibu wa kumpata mshindi Ballon d'Or nd'o rahisi kabisa kueleweka. Makocha na manahodha wa nchi 209 duniani walipiga kura, pamoja na wawakilishi wa waandishi wa habari wa nchi mbalimbali duniani. Tena kura zao huwa si siri... inafahamika kwa mfano ni nani alimpigia nani na mwishowe akapata kura ngapi. Anayebisha awaulize nahodha Juma Kaseja na kocha Kim Poulsen wa Taifa Stars pamoja na mwandishi aliye Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura. Waingereza wasiudanganye ulimwengu. Hakuna upendeleo wowote FIFA kuhusiana na ushindi wa Messi au Ronaldo na Iniesta kuingia 'top 3'; wala kikosi bora cha dunia ambacho wacezaji hupimwa kwa mwaka mzima kuanzia Januari 1- Desemba 31!
ReplyDelete