Search This Blog

Thursday, January 10, 2013

JE BARCELONA INAMTEGEMEA SANA LIONEL MESSI? NA JE GUARDIOLA NDIYE ANASTAHILI HIZI TUZO ZA MESSI? (PART 111)

Kwa kumtengeneza Messi kama nyota wa timu, Guardiola alitengeneza mzimu. Kwa kujaribu  kumfurahisha Messi makocha Pep na Tito waliiathiri timu. Hili linaweza kuakisiwa kwa jinsi Barcelona "Inavyomtendea" David Villa.

Villa aliahidiwa kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati aliposajiliwa, lakini akatupwa kushoto kama ilivyokuwa kwa Henry. Alifanikiwa mwanzoni baada ya kufunga kwenye msimu wa mwaka 2010/11, kabla ya jeraha alilopata msimu uliopita kulikuwa na ripoti za kuwa kwenye hali isiyo nzuri ya kisaikolojia kwa Villa kutokana na jukumu analopewa uwanjani kwenye timu na jinsi Messi alivyokuwa anabebwa kwenye timu na Guardiola.
Zikaanza kuvuja taarifa kuwa Villa anataka kuhama huku taarifa hizo zikizidi msimu huu baada ya mchezaji huyo kupona. Hata kabla ya kuondoka kwa Vilanova kabla ya kuugua kwake alishamuondoa Villa kwenye kikosi cha wachezaji kumi na moja wanaoanza mara kwa mara. 


Nadhani ni sahihi kuitazama hali hii kama hali ambayo inajenga kitu kibaya Barcelona. Mambo mengi sana yanapitia kwa Messi hali inayofanya wenzie kukosa umuhimu na pamoja na Barca kuanza na kufikia hatua ya kati ya ligi vizuri bado kuna ukosefu mkubwa sana wa balance kwenye timu.

Msimu huu uliopita kumekuwa na hali ya 'figisu figisu' kati ya David Villa na Messi ambapo Messi alionekana kukerwa na kitendo cha Villa kutompa pasi mwenzie mapema. Isaac Tello amelazimika kubadili mchezo wake ili kukidhi haja ya yeye kucheza kikosi kimoja na Messi. Timu imekuwa sana kwa Messi kiasi kwamba mtu anajiuliza mafanikio barani ulaya yatapatikanaje. 


Ligi inaonekana kuwa ya Barca tayari na hata huko kama kambi ya Real Madrid isingekuwa na matatizo yake pengine hali isingekuwa hivi, ila mafanikio ya ukweli yanapatikana ulaya kwenye ligi ya mabingwa na kwa sasa kuna timu ambazo zinaonekana kuwa na balance kuliko Barca kama Bayern na Juventus.

Barcelona imekuwa 'MESSI SHOW' na hii imefanya aonekana kuwa mchezaji bora kuliko wengine kwenye historia ya mchezo wa soka. Hata hivyo hiyo imekuja kwa gharama kubwa ya timu ambayo inaonekana kuwa chini ya Messi na haina umuhimu zaidi yake. Wachezaji wenzie na makocha wamekuwa chini yake kwa kuwa ana nguvu sana kuwaliko wao huku wachezaji wenzie wakiwa na woga wa kutompa mipira na kumuudhi wala kutompanga kwenye kikosi cha kwanza.


Je haya ni mazingira ya kujenga mafanikio kweli au mazingira yanayojenga mwanya wa kufeli, mtu mmoja hawezi kushinda kila kitu kwa timu nzima, ni timu ndio zinazopata mafanikio. Hispania imetwaa ubingwa wa Euro mara mbili na kombe la dunia kwa kuwa wana timu iliyokamilika na yenye balance na hawakuwa na mchezaji kama Messi na kama Barcelona hawatakuwa makini watakuwa kama Argentina ambayo ina messi ambaye hana msaada mkubwa sana.


Ukweli ni kwamba Messi amekuwa jawabu jepesi kwa Barca wakati mchezo ukiwa unahitaji bao kwa upande wa timu yake. Utegemezi kwa mtu huyu utakuja kuwa na madhara, mchezaji ataona kama jukumu lake kwenye timu halipingiki na bila kujijua atatumia uwezo wake vibaya. Messi anatajwa kama kijana mpole asiye na makuu ila hakuna wa kupinga kuwa anafahamu fika kuwa ana uwezo gani na umuhimu gani kwa timu yake na hili linampa nguvu kwenye kikosi cha Barcelona.


Barcelona wanaweza kuchagua mojawapo kati ya mambo mawili. Kinachohitajika ni balance kwenye timu, na balance hii itapatikana kwa kupata mtu atakayecheza mbele na Messi kuliko inavyoonekana sasa ambapo kuna viungo wanaofanya kazi ya kumpa Messi mipira. Kama Villa sio jawabu basi atafutwe mtu wa kutimiza jukumu hili, mtu ambaye anaweza kutoka pembeni na kuingia ndani  Neymar anaonekana kuwa mtu ambaye hata Messi amemuidhinisha kufanya kazi hii.


Pili na la kushangaza kwa wengi ni hili, kama Barca wanaweza wamuuze Messi kwa fedha nyingi, ni mchezaji bora kwa sasa kuliko wote, hakuna ubishi kwenye hili na ndio anayelipwa fedha nyingi kuliko wachezaji wote pia, ila Barca watapata faida kubwa kama wakimuuza kwani mwisho wake kwenye kikosi hiki hautakuwa mzuri kwa timu yake.


Barca wanaweza kupata ada ya uhamisho ya rekodi ya dunia kwa Messi kama wakiamua kumuuza na pia itakuwa maamuzi mazuri, kuna wachezaji wengi na kuna mfumo ambao upo utakaoifanya Barca iendelee kuwa Juu. Klabu inaendelea kubaki na wachezaji wanapita hivyo kama Barcelona wakikubali kumuacha Messi apite watakuwa wamefanya la maana na kujinasua kwenye mtego mkubwa ambao siku si nyingi utaigharimu.

Mwisho!

35 comments:

  1. Inaelekea unamchukia sana messi..too bad wewe ni mzaramo tu wa bongo...nothn u can do about it...dogo anatisha.

    ReplyDelete
  2. naona imekuuma sana kaka,. Pole bt ukwel uko pale pale namba 10 anaweza uyu Jamaa kjana anapga kaz, namba 7 wako akashndanie urembo cuttn fashion.

    ReplyDelete
    Replies
    1. barca kuna wataalamu wakubwa wa mpira na wenye uzoefu pia hawajaona hilo tatizo..ww mbongo ambae hata ya hapa kwetu yanakushinda umeona tatizo...duh..ndio maana ulipata kura mbili DRFA.

      Delete
  3. aisee ume-base kwenye negative side kweli kaka. Binafsi sidhani kama messi ni tatizo coz anafanya jukumu lake la kufunga kama mshambuliaji na pia kutoa assists kwa wenzie. Kwa mfano uliotoa ina maana leo ataondoka messi lakini ataibuka mtu mwingine ndani ya barca atawika je, na yeye auzwe. Bila shaka naheshimu mawazo yako ila sidhani kama yana usahihi coz mechi ambayo messi alitupiana na villa niliiona na ni kweli villa alifanya kosa na messi alifanya kazi kubwa kuanzisha movement ile wakati timu inatafuta ushindi baada ya kuonekana inaelekea kukosa ushindi. Labda nitoe mfano kidogo, Kwa mfano upo kwenye usaili wa kazi unaweza ukaulizwa udhaifu wako ni nini?, basi unaweza kujibu kuwa kwa kawaida meneja mzuri anapaswa kuwa mvumilivu na anayeweza kujizuia na hasiralaki udhaifu mkubwa ni kuwa huwa unashindwa kuzuia asira kwa wafanyakazi wavivu na wasioweza kumeet deadline. Jibu hili lina negative implication kwa upande wako lakini lina positive implication kwa kampuni kwani utaiokoa na wafanyakazi wavivu kwa ujumla wake. Hivyo basi alichofanya messi kukemea kitendo cha villa kuwa goigoi kilikuwa kibaya kwa upande wa messi kutupiana maneno na villa lakini kilikuwa cha kujenga na kwa manufaa ya timu hususani kwa mazingira ya kutafuta ushindi yaliyokuwepo. Kwa kuongezea ni kwamba mara zote messi akiulizwa juu ya kuvunja rekodi huwa anajibu kuwa la umuhimu kwake ni kufunga kwa kuangalia maendeleo/mafanikio ya timu na kama anavunja rekodi lakini cha kwanza ni mafanikio ya timu. Nina mengi ya kuandika na ku-argue isipokuwa hapa si mahali pa kuandika kupitiliza lakini kwa upande wangu sidhani messi ametendewa haki kutabiriwa kusababisha mambo mabaya kwa barca huko mbele.

    ReplyDelete
  4. Umenena jambo shaffih. Wanaokupinga ni washabika wa.... na si wachambuzi. Labda ni seme tu hivi, anachokiongelea shaffih ni ukweli Barca kwa sasa imekuwa ni ya Messi au kama ilivyokuwa kwa Casilas na Madrid. Usipo muuza Messi saivi anavyohit mwisho utauza kwa bei ndogo ama akaondoka huru. Wapo wachezaji bora ambao waliuza si kwa sababu hawakuwa wakihitajika na vilabu vyao hapana, Kwele kwa wenzetu kuna kitu kinaitwa " LET THINK ABOUT THE FUTURE" kutoka na msemo huo mtazame sasa KAKA wa AC milan na wa sasa si kwamba AC MILAN hawakuwa hawamhitaji la hasha ni Ankala tu. Njoo Kwa C. RONALDO si kwamba babu SAF alikuwa hampendi hapana ni Mkwanja. Mtazame Zidane alivyokuwa Juventus hadi Benabeu, mwangalie Ronaldo alipotokea Inter Milan au mtu mzima Figo. Sitoi historia bali nasemea ni jinsi gani mchezaji anauzwa pindi akiwa katika fomu nzuri. Kumbuka Messi wa leo si wa kesho ama kesho kutwa. Si kwamba Messi anachukiwa hakuna na ukimchuki basi mpira uhujui. Na hata akiuzwa kwa sasa kwa kuvunja rekodi ya C. Ronaldo ni timu chache zitahimili kama PSG, MAN CITY, MADRID kwa uchache.

    BIASHARA MAPEMA BARCA!

    ReplyDelete
  5. Kweli bongo hakuna mpira eti huyu pia nimchambuz. Messi ni zaid ya Laliga

    ReplyDelete
  6. kwa mpira wa cku hz,timu lazima iwe na mtu ambaye anaweza akafanya lolote ktk muda wowote na anaegopwa xana na wapinzan.dah,upo wrong vbaya braza coz sometimes 2namuona Messi akiassist wenzie wafunge. hlf vp braza,hujiuliz kwa nn babu Fagason alimlazimisha rooney asiondoke Man U. Najua ushabik unakusumbua

    ReplyDelete
  7. shaffih you know nothing about football, we zungumzia mambo ya kina ngasa na sio messi, umekosa cha kuandika kwenye hiki ki blog chako basi usipoteze mda wa kuandika ujinga, uwe unabaki na diva usiku kwenye kipndi cha hara za roho.

    ReplyDelete
  8. Wewew jamaa umezidi kukurupuka kuhusu mambo ya mpira ila hili la MESSI unaingia chaka endelea kuwa mtangazaji 2 ila uchambuzi wa mpira ni ziro.

    ReplyDelete
  9. kwa point iz ckubal shaffi uwe unajpanga bac...

    ReplyDelete
  10. shafih..umetoa mtizamo wako...ila mzee ni wazi huwa upo so negative na barca na messi...hata habari unayo ileta ya barca au messi huwa unajaribu kutafuta ile yenye utata...kocha yoyote anapenda kutengeneza kikosi au mfumo ambao utaleta mafanikio kwake haraka hata kama ana mfeva mtu fulani lakini yee mwisho wa siku kapata kombe na heshima..kumbuka pep alikuja barca messi tayari yupo 1st team na xavi iniesta puyol wote walikuwepo wanakamua..yeye aliangalia mtu gani ataleta impact kwake na kupata kombe..kuna mwandishi mmoja makala fulani aliongelea suala la messi kumpa jina pep na wewe unaleta leo pep kumpa jina messi..hahaha...dogo ukimpa mpira tu utaona kipaji chake..na messi alikuwa na uwezo tangu akiwa 12yrs wa hali ya juu sana...now u r talking as if messi is nothing..tumeshuhudia mechi kibao messi anacheza bila xavi na iniesta na kupata magoli na kuichosha beki...kama unakumbuka last yr messi alifikia record ya maradona team ya taifa je kule kuna pep na xavi na iniesta..???..nakumbuka messi amewanyanyasa sana brazil last three games ikiwepo na kupiga hatrik na pia messi akiwa captain wa argetina..je argentina kuna pep na xavi?

    siku zote unaletaka makala yenye utata kwa messi na makala yenye utamu kwa Ronaldo...kweli mapenzi ni upofu!!

    jahaclassic!!!....

    ReplyDelete
  11. MH! NAPITA TU,HIYO MAKALA YAONYESHA UMEKOPI MAHALI NA MUANDIKAJI AWEZA KUWA VILL AU MMOJA KATI YA WATU WAKE,"KWA SASA MESSI TUMUACHE TU"

    ReplyDelete
  12. Messi ashaanza kujaa kiburi wampige sale fasta. Ila jamaa anatisha mi namuogopaaaa acha awe mchezaji bora duniani ni haki yake.

    ReplyDelete
  13. nimesoma wote maoniyenu..but wote hamjui soka,.mnafata mkumbo tu,.shaffih kaeleza ukweli usiopingika,.kiukweli hamna messi bila wachezaji wa spain,.messi ni tegemezi la kina xavi,iniesta na wenzie,.yeye mpaka apew,.hajui kutafuta.,kama ni ufundi wa vyenga,.walikuwepo kina dinho,zizzou.,huo ndio ukweli,.messi anabebwa na wacatalunya.

    ReplyDelete
  14. kaka shafii rejea uchambuzi wako ambao unaonekana unataka kujenga taswira mbaya kwa kijana Messi.Mimi naona hapa umeleta siasa zile umbazo tumezikataa katika uteuzi wa mchezaji bora.siku zote kocha mzuri anajenga timu kwa kupitia mfumo fulani ambapo huwa na key players wake . kwa barca timu imejengwa kupitia kwa messi. Nakukumbusha kuwa hapo awali timu hii iliwahi kufanya hivyohivyo kwa kuwatumia watu kama Ronadinho, rivaldo,Luis Figo,Luis enrique na Wengine wengi Tu. Hata huyo Namba Saba Wako pia timu yake imejengwa kwa kupitia kwake mbona hilo hulisemi? Acha siasa.

    ReplyDelete
  15. Sijawahi kuona uchambuzi wa kijinga kama huu, halafu mkiambiwa hamjui kitu kuhusu mpira mnakasirika. Wazungu wana msemo " if it's not broken don't fix it". Barcelona wako katika level ya juu kabisa ya mpira halafu wewe unataka kutuaminisha kwamba wana matatizo eti kwa sababu Villa hapati nafasi. Timu huwa zinauza wachezaji kutokana na sababu kadhaa kama vile: (i) Mchezaji mwenyewe hataki kuendelea kuichezea timu hiyo au ametangaziwa dau kubwa na timu nyingine na anataka kwenda huko. (ii) Timu haimuhitaji mchezaji huyo kwa kuwa ha-fit kwenye mipango ya klabu, kiwango kushuka au timu nyingine imetangaza dau kubwa na klabu inataka kufanya biashara. Sababu zote hizo hapo juu hazi-apply kwa situation ya Messi sasa kwa nini auzwe? Au kwa kuwa huwa ananyanyasa vitimu vyenu vya EPL. Watu wanashindwa kuelewa kwamba Messi na Barcelona it's more than football, it's about life, loyalty. Ni kama ilivyokuwa kwa Raul na Real Madrid.

    ReplyDelete
  16. Mimi nadhani hamjamuelewa Shaffih, ningeomba msome tena then mtoe maoni yenu kwa upya. ngoja niwakumbushe kitu unakumbuka mzimu wa Rooney ulivyokua unaitafuna Man U??, Unakumbuka mzimu wa Yaya Toure unavyoitafuna Man City?? hiyo ni mojawapo ya mifano ya timu ambazo zinaundwa kupitia mchezaji flani, ili timu iondokane na mzimu huo lazima wa-balance timu, lazima timu iwe na mpango mbadala na wachezaji wote waone umuhimu wao katika mafanikio ya timu. sio lazima kila mtu afunge ndio aonekane muhimu bali kila mtu awe ana sauti sawa katika timu na anafanya kazi yake bila kuwa na shinikizo kutoka kwa mwenzake. umeona wote ambao walikua wana-compete na Messi kiliwakuta nn?? kumbuka samuel eto'o fils, zlatan ibrahimovic, thiery henry, bojan kric wote hao walipotezwa na barca katika timu ili messi awe bora. najua barca & messi fans ni watanzania halisi ambao ni wagumu kuukubali ukweli lakini bado kitambo tu watakua kama Inter Milan waliokataa kumuuza sneijder kwa pesa nyingi na sasa wanaganga njaa. Hongera shaffih ni mwanzo tu soon utakua the best, hao wanaokuponda walete makala zao hapa tuone wanavyojua soka. kila safari ndefu huanza na hatua ya kwanza. BIG UP BRO

    ReplyDelete
  17. Hello Wadau! Inavyoonekana wengi wetu tunafuata mkumbo tu, kinachonishangaza hii story imeanza kitambo,hii PART 3 ndo mmetoa comments nyingi,lakini kabla ya kutoa maoni yenu someni kwanza kuanzia PART 1 ili mumuelewe Shaffih,afu kitu kingine sisi mara nyingi tunatukana tuu badala ya kupinga hoja,maana yangu ni nini ? Badala ya kushutumu tuu nasisi tuandike hoja za kupingana na hoja Shaffih.huo ndo mtazamo wake tuuheshimu baada ya kuanza matusi,Dauda ni kijana aliyeleta mapinduzi makubwa kwenye hii tasina ya michezo hilo lazima tulikubali,lakini asilimia kubwa ya wabongo hatu--appreciate ila kazi yenu ni ku-hate tu,

    ReplyDelete
  18. Najiuliza tu! Benchi la ufundi pamoja na uongozi mzima wa Timu kubwa kama Barca, waliosheheni watu wasomi na wazoefu wa soka n.k. Wanaofanya tathmini ya maendeleo ya timu kila mara kuona matatizo na mafanikio na maeneo ya kurekebisha kwa manufaa ya timu. Wana maono na mipango ya miaka 100 ijayo Barca itakuwa wapi n.k. Hawa wote wasione tatizo eti Bongoambao mnajua Simba na Yanga ndo muone tatizo. Ha ha haaaa! This is interesting frankly!

    Sawa, nadhani kutoa maoni ni haki ya kila mtu kwa hiyo tunashukuru kwa maoni ila nadhani mngekuwa wachambuzi na wataalamu wa soka mngesaidia Tanzania kuondokana na usimba na uyanga na kuendeleza soka letu lifikie walau robo tu ya Barca, Madrid, Man U, Bayern n.k. Vinginevyo sidhani kama hapa kuna issue kama inavokuzwa ionekane tatizo. Nadhani kuna ushabiki unaotokana na EPL fans (ambao ndo wengi kwa Tanzania kwa kuwa waingereza mpira ni matangazo zaidi)dhidi ya soka zuri, la kuvutia na la kitaalamu la Spain, number one in the world for the past 5yrs, World Champions and Europian Champions as well!

    ReplyDelete
  19. Shafi unachosema hujakosea kabisa, mi mara nyingi nashangaa kama barca ina mchezaji mmoja, ubora wa Messi si juhuudi binafsi bali za viungo bora wa Kihispania, Javie na Inieta, natamani kumuona Messi akicheza bila hawa watu, mi nadhani hata ukimweka Etoo,Van Perse, Demba Mba,Michu au hata Falcao lazima watangaa tena zaidi ya Messi kutokana na msaada wa viungo hawa bora duniani. Mi nadhani hata tuzo ya mchezaji bora aliistahili Cristiano Ronaldo au Shafi unasemaje?

    ReplyDelete
  20. Jamani kama magoli ya Ronaldo na Messi yangeondelewa kwa msimu uliopita, msimamo Laliga ungekuwa hivi
    Pld Pts
    1. Real Madrid 38 75,
    2. Valencia 38 67,
    3. Malaga 38 62,
    4. Atletico Madrid 38 61,
    5. Levante 38 59,
    6. Barcelona 38 58,

    http://www.whoateallthepies.tv/la_liga/124415/stat-attack-how-the-la-liga-table-would-look-without-messi-and-ronaldos-96-goals.html

    nimeweka hiyo website ili yeyote anayetaka kuthibitisha hili basi akajionee mwenyewe.

    jamani hiki ndicho anachosema Shaffih.... si kwamba Messi ni mchezaji mbaya la hasha.... kwa sasa Messi ni mchezaji bora kabisa ulimwenguni.... lakini kwa mfumo uliowekwa Barca ili kumpatia mafanikio makubwa una madhara yake kwa timu hapo baadaye..... jamani nadhani mnakumbuka ya Diego Armando Maradona na Napoli yake? hivi mnajua baada ya Maradona Napoli ilishuka hadi daraja, sina maana hili linaweza kutokea kwa Barca lakini najaribu kuonesha madhara yanayoweza kutokea kwa kujenga timu kupitia mchezaji mmoja.

    hebu jiulize ni kwa nini Barca hawakuwa mabingwa wa Laliga ilihali Messi alifunga magoli ya kumwaga? wakati Messi alifunga magoli 73 ya Laliga msimu uliopita, hakuna mchezi mwingine wa Barca aliyefikisha Magoli 20.

    Kama Shaffih atakuwa amemaanisha kuwa Messi ni Mchezaji wa kiwango cha kawaida, kitu ambacho si kweli maana nimesoma kwa makini makala yake, atakuwa amekosea sana. Messi si mchezaji wa kawaida na ndio maana hata jukumu la kuibeba timu alilo nalo amefaulu kwa asilimia 90... ni wachezaji wangapi wanaopewa majukumu kama ya Messi na wasifanikiwe?

    ila hoja ya msingi ni namna timu ilivyojengwa kupitia Messi, na hivyo kutokuwa na uwiano mzuri katika timu...., ikumbukwe kuwa Messi si natural striker kama walivyokuwa akina Ronaldo De Lima, Samwel Eto'o, Ramadel Falcao, Robin Van Persie, Michael Owen, Chriatian Vieri, Roberto Baggio, Gabriel Batistuta na wengine wengi unaowafahamu...., Messi ni Kiungo Mshambuliaji, mwenye uwezo wa hali ya juu.... ila amekuwa "transformed" na Pep ili aweze kuwika. Hivi mnakumbuka maneno ya Pep mwenyewe? alisema “If Leo smiles, everything is easier”. kwa hiyo ni lazima mambo yote yafanyike ili kumfanya awe na furaha... hii ni pamoja na kumtimua Ibrahimovic kwa kutaka kucheza nafasi sawa na Messi, Eto'o kwa kudhani anaweza akacheza free role kama Messi na hata sasa Villa kupigwa benchi kwa sana au kuchezeshwa katika nafasi ya kumfanya awe ni mpishi wa mabao wa Messi nk.

    Ninachoweza kusema ni kumpongeza Lionel Messi kuwa hajawaangusha wote waliofanya kila linalowezekana kumfanya awe na furaha na kisha afunge kama mashine. hata kama madhara yakitokea baadaye, atakayeumia ni nani? Pep. hatakuwepo, Vilanova hatokuwepo..., na hata wakati Napoli inashuka daraja, Maradona hakuwepo..., ni sisi mashabiki ndo tutakaoumia.. lakini hatutajali maana tutakuwa tunakumbukia furaha ya kuwa na Messi ndani ya Barca..., aaaah aaaah! Mesiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!


    ReplyDelete
  21. To be honest Shaffih huwa upo negative na MESSI na +ve kwa R7 bt umejtahd kuchambua vyema though Bado attitude yako bnafc kwa Messi umeshindwa kabisa kuifuta. Km ni mtazamaji balanced cku zote utamuona Lionel Messi anaanzisha mashambulizi kuanzia katikat kama kiungo na cku zote amekuwa juu ktk orodha ya assist na pasi za magoli, angalia nafac wanazopata akina Tello na zinazotumiwa kupata magoli bado Messi anabaki wa Kipekee ktk kutumia Nafasi, lakn kumbuka pia kuna tym Messi anachambua karibu mabeki wote jamii ya akina Marcelo halafu akafunga goli na haya co mara moja!!1
    Kwangu LIONEL MESSI anabaki mchezaji bora zaidi duniani. Ukiitizama Madrid Real ktk viungo utawakuta Mesut Ozil, Di maria, Alonso, Khedira viungo ni wa kiwango cha juu sana ambao wanajtahd sana kumlisha Ronaldo na kumchezesha lakn bado utagundua Ron 7 sumtym anakuw na papara kwa kutak kufunga goli popote kitu ambacho kinampunguzia umakini,kwani ktk mashuti 7 pocbly akafunga moja wakt Messi atatafuta mbinu mpk asogee golini na obvious hufanikiwa na kufunga magoli kirahiis zaidi. Ron7 na Messi ni wachezaj wa kiwango cha dunia lakini bado Messi atakuwa mbele ya R7.
    Shaffih ukubali ukatae Messi HAKUNAGA.

    ReplyDelete
  22. barca ni klabu kubwa, na inahitaji kuwa na wachezaji wakubwa kama messi sioni sababu ya kumuuza messi kwani ni zao la la masia na analipa fadhila kwa barca kwa kumtoa mbali. Barca ina utamaduni wake na messi anawika kwa sababu anaujua vizuri. na si lazima messi akacheze sehemu nyingine kwani barca nayo ni klabu kubwa duniani sioni kama klabu fulani zinazotumia fedha nyingi kuzijenga. kabla ya messi wamepita wengi na messi naye ataondoka lakini barca itaendelea kuwepo kwa sababu wanacheza kwa utamaduni wao na sio kwa fedha nyingi ambazo wakati mwingine zinaharibu mpira.

    ReplyDelete
  23. kaka xeElias Hezron, umeongea kitu ambacho anayeipenda taswira yake akiiona kwenye kioo bila kujua kwanini inatokea ndio wanaojaribu kumpinga Shaffih na kumtolea maneno yasiyo eleweka... hv mnataka kusema messi ndiye mchezaji bora ambaye mmewahi kumuona?....Dinho,,Zozou,,De Lima,,Figo,,Gerald na wengineo...hakuna timu iliyojaribu kutengeneza mfumo unaowategemea hao wachezaji ndio maana hata walipo ondoka au wakiwa hawapo kwenye vikosi vya kwanza bado timu zao zilibaki kama kawaida...

    ReplyDelete
  24. U a all right. Ila kwa sasa Messi hana mpinzani. Shaffii angalia Barca B si mchezo. Conveyor belt yao iko full loaded. Kuna vitu si mchezo. Zlatan kwa kweli angewafaa sana kwenye mechi kama ya Chelsea, lakini kwa muda mrefu hakuzaa matunda. Attitude yake nayo ikawa shida. Pamoja na hayo Messi is a good futballer and a team player for both Barca and Argentina. Hata akiwa bora kiasi gani wachezaji wengine wanamchango sana. Bila Hugguein, De maria, Agguero, Tevez hawezi fanya kitu. Argentina hawajawa na bahati lakini 2010 walikuwa wanaogopwa. Spain wenyewe wamepata mafanikio kwa staili ya Barca. Yaani bila kuwa na natural center forward. Torres, Llorente walikuwa wanaanzia nje. Del bosk anaamini mfumo huo. Na ndio maana Morinho hapendwi na mashabiki hasa wa Real ambao wanaumia sana kwa mfumo huu wa vululu vululu. Enzi zile Zidanne ndio alikuwa ana dictate mchezo. KAMA KUNA TIMU INAMUHITAJI MESSI IJITOKEZE AU ALAZIMISHWE KUSTAAFU.

    ReplyDelete
  25. Del Bosque "Messi without Xavi-Iniesta? He'd stay the best, nothing would change. Put him anywhere, he'll dribble all." Weka uZaramo wako pembeni wewe ndo maana soka la bongo halikui wazaramo mmelikaria mno etii ndo wachambuzi. Nenda Cost Un na Azam bila kusilimishwa husajiliwi, Wazaramo bwana mnaturudisha sana nyuma.

    ReplyDelete
  26. U a all right. Ila kwa sasa Messi hana mpinzani. Shaffii angalia Barca B si mchezo. Conveyor belt yao iko full loaded. Kuna vitu si mchezo. Zlatan kwa kweli angewafaa sana kwenye mechi kama ya Chelsea, lakini kwa muda mrefu hakuzaa matunda. Attitude yake nayo ikawa shida. Pamoja na hayo Messi is a good futballer and a team player for both Barca and Argentina. Hata akiwa bora kiasi gani wachezaji wengine wanamchango sana. Bila Hugguein, De maria, Agguero, Tevez hawezi fanya kitu. Argentina hawajawa na bahati lakini 2010 walikuwa wanaogopwa. Spain wenyewe wamepata mafanikio kwa staili ya Barca. Yaani bila kuwa na natural center forward. Torres, Llorente walikuwa wanaanzia nje. Del bosk anaamini mfumo huo. Na ndio maana Morinho hapendwi na mashabiki hasa wa Real ambao wanaumia sana kwa mfumo huu wa vululu vululu. Enzi zile Zidanne ndio alikuwa ana dictate mchezo. KAMA KUNA TIMU INAMUHITAJI MESSI IJITOKEZE AU ALAZIMISHWE KUSTAAFU.

    ReplyDelete
  27. Hapo umesimama kama shabiki na si mchambuzi pole sana Shaffih

    ReplyDelete
  28. Binafsi nataka nimuite shafii ni mshabiki wa cristian ronaldo kwanza amesahau messi ndo anaongoza kwa pasi za magoli hivi sasa licha ya kufunga pili mbona hatoi mfano wa cristian ronaldo wa kutafutiwa magoli mpaka penati hivyo ananipa wasi wasi wa kumuamini kama anujua mpira shafii kua mkweli messi anjua na je anpokua argentina yale magoli anyofunga pia wakina di maria wanamuogopa acha ubinafsi wa fikra sasa messi ndo bora na ubora wake kaudhiirisha kumaliza msimu kwa kua na goli 25 akiwa amefunga penati moja tofauti na wenzie acha mtazamo wa uongo shafii ntakushusha thamani brother kumbe na wewe malupe lupe ndugu yangu acha ushabiki ndo mimi hua nasema mchambuzi wa soka tanzania ni dr leak pekee yake wengine nyie mnatafuta ugali mpe haki yake kijana mdogo messi angekua mhispania mngesema anapewa kwa sababu ya uhispania wake muargentina mnasema anapendelewa na guardiola na vilanova hivi kwa kiwango cha messi sasa ni kocha gani dunian angemuweka aanzie benchi villa aanze au umtoe etoo na gaucho umuweke henry

    ReplyDelete
  29. Kaka shafii punguza chuki binafsi na tuangalie maendeleo ya soka uko ulaya ambapo utakuwa ni mfano hapa kwa wachezaji wetu

    ReplyDelete
  30. Laiti Shafihh Dauda ungekuwa mchambuzi wa soka ktk Bara la Ulaya na unaitwa lwenye TV mojawapo uchambue Soka basi utafukuzwa kabla kipindi hakijaisha! Ukitaka kuwa mchambuzi wa Soka lazima uwe kama refa!

    ReplyDelete
  31. Still messi we shaffi umesomea wapi uchambuzi wa soka?na hukuna unachokijua kuhusu messi tofauti na makala zako za kukopi sasa unalazimisha auzwe we ni nani?mbona kuna mechi wanacheza bila messi na wanashinda?iv we shaffi huwa ni mtumwa wa kichuki juu ya messi?wel kwa ushauri kajifunze uchambuzi wa soka na sio kukopi makala na kupost bila kuzifanyia statistical analysis

    ReplyDelete