Search This Blog

Tuesday, January 29, 2013

MCHUMBA WA CASILLAS ASEMA JOSE MOURINHO AMEACHA KABISA KUZUNGUMZA NA WACHEZAJI WAKE MADRID

Mchumba wa golikipa wa Real Madrid Iker Casillas - Sara Carbonero amesema Jose Mourinho ameacha kabisa kuwasiliana na wachezaji wa klabu ya Real Madrid.

Taarifa za hivi karibuni zilizotolewa na gazeti la Marca zimesema kwamba Casillas na msaidizi wake kwenye unahodha Sergio Ramos wametishia kuondoka kwenye klabu hiyo ikiwa Mourinho ataendelea kuwepo kwenye klabu hiyo, ingawa hata hivyo Raisi wa klabu hiyo Florentino Perez alizipinga vikali sana taarifa hizo.

"Hali sio shwari ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo vya Real Madrid, na suala ambalo linafahamika kwamba Mourinho hazungumzi na wachezaji wake," Carbonero aliiambia La Jugada.

Aliongeza, "Kuna mgawanyiko kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Tutasubiri kujua nini kitatokea mwishoni mwa msimu na kama Mourinho ataondoka."

Jose Mourinho ana mkataba wa mpaka 2016 baada ya kusaini mkataba mpya kiangazi kilichopita, lakini magazeti mengi ya Spain yanatabiri kwamba kocha huyo wa zamani wa Inter ataondoka mwishoni mwa msimu.



No comments:

Post a Comment