Search This Blog

Friday, January 4, 2013

JUMA OMARY- ' NILIUZA SUPRA ZANGU ILI NIPATE NAULI YA KUJA DAR KUCHEZA SOKA'



Kihistoria mchezo wa soka huchezwa na watu wengi walio maskini,lakini si maskini wote wamefanikiwa kuucheza kwa mafanikio, Historia zinaonyesha  wanasoka wengi kutoka mabara ya Amerika na Afrika walio wengi wametoka kwenye familia za kimaskini sana, ila juhudi na mipango ya kutokukata tamaa imewasaidia kuibuka wanasoka nyota ulimwenguni, mifano ipo mingi tukianza tu na majina maarufu kama Pele na Maradona wote wametokea kwenye familia za kimaskini.
Yapo majina lukuki ya wanasoka maarufu ulimwenguni waliotoka kwenye familia za kimaskini miongoni mwa majina hayo ni kama vile Rivaldo, Ronaldo Di Lima na Carlos Tevez kutoka bara la America ya kusini, Abeid Ayew, Samuel Etoo, Michael Essien hayo ni baadhi ya majina kutoka barani Afrika na wengine wapo kibao yaliyotokea katika familia maskini na wameanza soka katika mazingira magumu.
Lakini kwa juhudi zao binafsi wachezaji hao wamefika walipokuwa wakipataka na kuwa midomoni mwa klabu tofauti kubwa barani ulaya kila linapofunguliwa dirisha la usajili.
Hapa  nchini kwetu Tanzania kila kukicha tunamuomba mungu walau asikie kilio chetu tuweze kumpata mtanzania wa kucheza soka la kulipwa kwenye ligi kubwa barani ulaya,kuna mambo mengi ya kiuweredi yanatukwamisha katika hili lakini kuna wenzetu UTHUBUTU waliokuwa nao umewasaidia.
Tukianzia kwa majirani zetu Kenya juhudi binafsi za kina Mariga,Oliech na sasa Victor Wanyama zimewasaidia sana,uthubutu wao pamoja na kukubali changamoto mbali mbali vimewafanya kuchezea ligi kubwa barani ulaya,
Kijana  JUMA KARIM OMARY  mwenye umri wa miaka 16, mzaliwa wa maeneo ya Misunkumilo ,wilaya ya Mpanda Mkoani Rukwa ameamua kuanza safari yake ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza soka la kulipwa nchini England, kijana huyu kutoka familia ya mzee Omary Yusuf, Mzee Omary ameoa wake watatu na mmoja wa wake zake watatu ni Bi Saada Damas ambaye ni mama wa watoto wanne kati ya watoto saba wa mzee Omary, Juma Karim ni mtoto wa kwanza wa Bi Saada pia ni mtoto wanne kuzaliwa kwenye familia ya mzee Omary.
Kutokana na matatizo ya kifamilia kijana Juma Omary aliamua kujikita kwenye mchezo wa soka ili kuweza kujinasua kimaisha lakini alipata upinzani mkubwa kutoka kwenye familia,
Pamoja na familia kutomruhusu kucheza soka lakini tayari  yupo jijini Dar-es-salaam akiwa na malengo na kiu ya kufanya vyema kwenye medani ya Soka na hatimaye kufanikiwa kucheza Ulaya na kujipatia pesa.
Kijana huyu ameonesha kiu yake ya kufanikiwa katika soka kwa kuanza mchezo huo akiwa na umri wa miaka 7 ambapo alianza kucheza nafasi ya ulinzi,kabla ya baadae kuhamia kwenye nafasi ya kiungo.
KARIM aliendelea na soka  hadi alipokuwa shule ya Sekondari Rungwa huko Mpanda ambapo muda mfupi baada ya kumaliza kidato cha nne alijiunga na timu ya Polisi mkoani humo.
Jambo la kustua na la kutia moyo kwa kijana huyu, ni namna alivyosafiri kutoka Mpanda Mkoani Katavi hadi Jijini hapa kutafuta timu ya kuchezea ambayo anaamini itaanzisha safari ya mafanikio yake kwenda barani Ulaya……...

Itaendelea…..

1 comment:

  1. maisha ni safari asikate tamaa tu mdogog wangu akaze buti na akumbuke amesafir umbali mmrefu kuja kutafuta channel ya kutoka kisoka dar kuna mambo mengi ambayo asipokua makin anaweza akshangaa kipaji chake chote kinapotea ni hayo tu by Rajabu abdallah wa kimara.

    ReplyDelete