Mchezaji
Alain Kabange Twite hataweza kuichezea Yanga msimu huu (2012/2013)
baada ya klabu hiyo kuingiza nyaraka zenye upungufu wakati ikimuombea
Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa njia ya mtandao (Transfer
Matching System- TMS).
Kwa
mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), baadhi ya
nyaraka zenye upungufu katika maombi hayo ni mkataba kati ya Twite na
Yanga, lakini vile vile makubaliano ya mkopo (Loan Agreement) kati ya
Yanga na FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambayo ndiyo
inayommiliki mchezaji huyo.
Ili
mchezaji aweze kupata ITC kwa njia ya TMS, kwa mujibu wa Kanuni za
Uhamisho wa Wachezaji za TFF kuna nyaraka kadhaa muhimu zinatakiwa
kukamilika katika maombi hayo ili hati hiyo iweze kupatikana.
Bora siku hizi ni FIFA, hwa ni wataalam wa kuchakachua ingekuwa TFF wangepita tu. Acha wajifunze kufuata taratibu
ReplyDeletehili jambo lilishasemwa tangu awali kabla Yanga hawajaenda Uturuki wakajifanya kutosikia, sasa inakula kwao
ReplyDeleteHAHAHAHAHAHA ACHA UNAZI WEWE ,
ReplyDeleteHaya ndiyo matatizo ya kuwa na viongozi wasiojua soka la kisasa linataka nini katika timu zetu.Tumechoka kusikia kusikia haya kila mara makosa ni yaleyale.Tutaendelea kuzishabikia timu Man Utd na nyinginezo. Eti oohh...! tupende vya nyumbani.Hatuwezi kupenda vya nyumbani kwa mambo ya kipuuzi kama haya.Leo Yanga na kesho Utasikia kitu kile kile Simba.TUBADILIKE JAMANI.....!
ReplyDeleteKama taratibu za kina Yondani na akina TWITTE zingepita fifa mojakwamoja wasinge chezea yanga katu
ReplyDelete