Timu
ya Young Africans Sports Club iliyokuwa imeweka kambi ya wiki mbili
katika mji wa Antalay nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko
wa pili wa ligi kuu ya vodacom na mashindano ya kimataifa tayari
imeshatua nchini leo aflajiri.
Msafara wa watu 33 ukiwa na wachezaji 27 na viongozi 6 umewasili
katika uwanja wa ndege wa kimataifa majira ya saa 10 kasoro alfajiri kwa
shirika la ndege la Uturuki Turkish Air ambapo katika mkuu wa Young
Africans Lawrence Mwalusako aliongoza mapokezi hayo.
Young
Africans iliweka kambi katika hoteli ya Fame Residence kwa kipindi chote
cha mafunzo ambapo pia ilipata fursa ya kucheza michezo kadhaa ya
kujipima nguvu na timu kutoka barani ulaya katika nchi za Uholanzi,
Uturuki na Ujerumani.
Mara baada ya kutoka nje ya uwanja wa ndege
bus la klabu liliwachukua wachezaji na viongozi tayari kwa kwenda
kupumzika ambapo kocha mkuu Ernest Brandts ametoa mapumziko ya siku 2
kwa wachezaji kukaa na familia zao kabla ya kuanza mazoezi tena siku ya
jumatano kujiandaa na ligi ku ya vodacom.
No comments:
Post a Comment