Search This Blog
Thursday, January 24, 2013
ANACHOFANYIWA MALOUDA NA CHELSEA KINADHOOFISHA UMOJA MIONGONI MWA WACHEZAJI WA CHELSEA
Mnamo mwaka 1996, kocha wa Chelsea wa wakati huo Ruud Gullit alimfungia vioo mchezaji Gavin Peacock katika kujihusisha na shughuli zote za kikosi cha kwanza huku akimpeleka kiungo huyo kwenda kufanya mazoezi na kikosi cha watoto wa timu hiyo.
Kocha huyo mpya wa klabu hiyo hakuwa na mapenzi na Peacock, kiungo mzuri wa ligi ya England, na tayari alishamtafutia mbadala wake ambaye alikuwa ni Roberto Di Matteo.
Uamuzi wa Gullit kumuondoa Peacock haukupendwa na wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo na hivyo uamuzi huo ukaanza kuathiri molari ya timu miongoni mwa wachezaji.
Ingawa walimheshimu Guillit na maamuzi yake ya kiueweledi, Peacock alikuwa anapendwa na wenzie kwa kujituma kuliko ndani ya kikosi chao.
Alikuwa mweledi aliyejituma na kuipenda kazi yake na wachezaji wenzie waliamini kumuondoa kwenye timu kulikuwa ni kuharibu molari na umoja wa timu.
Hatimaye nahodha Dennis Wise, alimfuata Guillit na kumpa sababu nyingi kwanini Peacock alikuwa anahitajika kuwemo kwenye kikosi cha kwanza
Gullit alikubali mawazo ya wachezaji wake wakubwa kupitia nahodha wao na akamruhusu Peacock kurudi timu ya kwanza mpaka pale alipopata timu nyingine.
Hivi tukio kama la Peacock limemtokea mchezaji Florent Malouda, ambaye kwa muda sasa nae ametengwa na timu ya kwanza akilazimishwa kufanya mazoezi na timu ya watoto - jambo ambalo limeonekana kuiathiri umoja wa timu ya kwanza.
Hakuna anayefahamu kwa mchezaji kariba ya Malouda anafanyiwa matendo hayo - akilazimishwa kufanya mazoezi na timu academy.
Malouda wa sasa sio yule miaka kadhaa iliyopita, lakini amekuwa mchezaji mzuri na mtiifu kwa klabu ya Chelsea na kuisadia kupata mafanikio.
Amefunga mabao 35 katika EPL kwenye mechi 149, takwimu safi kwa nafasi yake ya winga wa kushoto.
Katika mechi yake ya kwanza, chini ya Jose Mourinho mwaka 2007, alifunga bao zuri katika ngao ya hisani dhidi ya Manchester United kwenye uwanja wa Wembley.
Alikuwa mmoja ya wachezaji walioipa Chelsea ubingwa wa kihistoria wa Ulaya msimu uliopita akiingia kama mbadala wa Ryan Bertrand katika fainali dhidi ya Bayern Munich.
Mfaransa huyo akiwa kwenye msimu wake wa saba na Chelsea, alishinda taji la EPL chini ya Carlo Ancelloti na amebeba makombe matatu ya FA Cup tangu alipohamia darajani akitokea Lyon.
Uamuzi wa kumtenga kutoka kwenye timu ya kwanza unatokana na kukataa kwake kwenda Mexico alipotakiwa kuuzwa na Chelsea wakati wa dirisha la usajili lilopita.
Malouda, ambaye alikuwa anakaribia kuingia kwenye mwaka wake wa mwisho wa mkataba, alikuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Amerika ya kusini kwa kipindi chote cha kiangazi.
CEO wa Chelsea Ron Gourlay, ambaye aligusia kwamba mikataba ya wachezaji Ashley Cole, Malouda na Frank Lampard itaongezwa baada ya ushindi wa UCL, akabadilika.
Malouda, ambaye alitimiza miaka 32 mwezi sita mwaka jana, anaweza kuondoka Chelsea bure kutafuta klabu nyingine.
Baada ya uhamisho wake wa kwenda Mexico kushindikana aliambiwa asirudi timu ya wakubwa na wala aruhusiwi kufanya mazoezi na kikosi hicho.
Amekuwa akitengwa kwa msimu wote huu, kitu ambacho hakiwapendezi wachezaji wengine wa Chelsea.
Chelsea wamekuwa na tabia hii hata huko, msimu uliopita walimfanyia hivi Anelka na Alex ambao waliambiwa walikuwa hawahitajiki tena kikosi cha timu ya kwanza hivyo wakaambiwa wafanye mazoezi na timu ya watoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment