Inaonekana waliokuwa washambuliaji wa Chlesea msimu uliopita Didier Drogba na Nicolas Anelka wameingia choo cha kike kama watoto wa uswahilini wanavyosema. Hiyo imekuja baada ya taarifa za wachezaji hao kutolipwa mishahara yao na klabu ya Shanghai Shenhua.
Vyombo vya habari vya China vimeripoti kwamba management ya Nicolas Anelka ipo katika mazungumzo na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya China ili kusitisha mkataba baina yao huku mshambuliaji Didier Drogba amekuwa akihusishwa kurudi barani ulaya.
Drogba alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu ambayo inaripotiwa una thamani ya $300,000 kwa wiki mwezi June mwaka huu, lakini Oriental Sports Daily limesema kwamba mshambuliaji huyo mwenye 34 amekuwa akiidai mishahara yake ya wiki kadhaa.
Wakati huo huo, msemaji wa Shenhua amethibitisha Anelka yupo katika mazungumzo ya kusitisha mkataba wake.
No comments:
Post a Comment