David John Mwantika, beki kisiki wa Tanzania
Prisons anakuwa beki wa tatu kusajiliwa na Azam FC baada ya Malika
Ndeule na Omary Mtaki, hawa wanaungana na Uhuru Selemani na kufanya
jumla ya wachezaji waliosajiliwa na Azam FC kufikia wachezaji wanne.
Azam FC inatarajia kuelekea Kinshasa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 13 hadi 23 December kushiriki mashindano
ya Ngao ya Jamii (Charity Cup)
Mashindano hayo ambayo
yatashirikisha timu kubwa za kutoka Kongo kama DCMP na AS Vita Club timu
kutoka nje ya kongo kama Azam FC, Tusker FC, Gombe United ya Nigeria na
Diable Noirs na Congo Brazavile yatatumika na Azam FC kama maanadalizi
ya Confederations Cup
Azam FC inahitaji maandalizi na mechi
nyingi za kirafiki nje ya Tanzania ili kupata uzoefu kabla ya kushiriki
Confederations Cup. Kwa maana hiyo hii ni nafasi muhimu sana kwa Azam FC
No comments:
Post a Comment