Uongozi wa klabu ya Yanga unaomba radhi kwa taarifa zilizotolewa jana
juu ya uteuzi wa meneja Shaban Katwila, Afisa Mawasiliano Baraka
Kizuguto, habari ambazo zilitolewa na Kaimu Katibu Mkuu Lawrence
Mwalusako.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu makutano ya
mitaa ya Twiga/Jangwani, Mwalusako amesema anaomba radhi kwa hali
iliyojitokeza, kwani ameharakisha kutangaza uteuzi huo ambao bado
ulikuwa haujadhibitishwa.
Unajua mtu anapoteuliwa kushika nafasi
ya kazi, inapaswa kumpa taarifa mhusika kisha baada ya hapo mnakaa
mwajiri na mwajiriwa kukubaliana mazingira ya utendeaji kazi na taratibu
zingine, kitu hichi kilikuwa bado hakijafanyika hivyo vitakapokuwa
tayari tutawajulisha tena alisema 'mwalusako'
Kikao cha kamati ya
utendaji kilikaa mwishoni mwa wiki na kupendekeza Katwila na Kizuguto
kushika nafasi hizo, lakini taratibu za ufanyaji kazi wao zilikuwa bado
hazijajadiliwa, hivyo hayo ndo makosa yaliyofanyika kuwatangaza rasmi
ikiwa bado makubaliano hayafikiwa. (http://www.youngafricans.co.tz)
No comments:
Post a Comment