Luiz Felipe Scolari ametangazwa kuwa
kocha mpya wa wenyeji wa Kombe la Dunia 2014 Brazil leo, akirejea
katika benchi la ufundi la nchi yake kwa mara ya pili katika jaribio la kutwaa ubingwa
wao wa sita kwenye ardhi ya nyumbani ndani ya kipindi cha miezi 18 ijayo.
Scolari, ambaye aliiongoza
Brazil kutwaa taji lao la tano na la mwisho la dunia katika fainali za
mwaka 2002 - miaka 10 iliyopita, alitambulishwa rasmi na Shirikisho la Soka la Brazil kwenye
mkutano na waandishi wa habari, akichukua nafasi iliyoachwa na Mano
Menezes aliyetimuliwa Ijumaa iliyopita.
Carlos Alberto Parreira,
ambaye aliiongoza Brazil kutwaa ubingwa wao wa nne wa dunia mwaka 1994,
alitangazwa kuwa mkurugenzi wa ufundi wakati shirikisho hilo la soka la
BraziL.
No comments:
Post a Comment