Search This Blog
Tuesday, November 13, 2012
MATUMZI YA BANGI KWENYE MCHEZO WA SOKA NA SHERIA
Wakati ligi kuu ya Tanzania bara ilipokuwa katika hatua za mwisho za kuanza miezi kadhaa iliyopita, Raisi wa shirikisho la soka Tanzania Leodgar Tenga aliwatangazia vita wachezaji wanaotumia vilevi au madawa yanayokatazwa uwanjani. Alikaririwa akisema imefikia mwisho kwa wachezaji wa kibongo kuvuta bangi, lakini sasa ligi imefikia katikati hakuna hatua yoyote ambayo imeonekana katika kuhakikisha wachezaji wanapimwa na kujiridhisha hawatumii vitu vilivyokatazwa michezoni.
Haya sijui zilikuwa siasa au mipango ya kuelekea kwenye utaratibu inaendelea hatuna majibu ya kueleweka. Hata hivyo ebu tuzungumzie utumiaji wa bangi na madawa yaliyokatazwa michezoni.
BANGI, SHERIA NA SOKA
Unapowaza kuhusu wanasoka na madawa ya kulevya, wengi hufikiri kuhusu madawa yanayosaidia kuongeza uwezo wa mchezaji uwanjani au madawa yaliozoeleka kama cocaine. Mara chache kinachowazwa na wengi ni ule utamaduni wa kunywa pombe kwa wengi uliozoeleka barani ulaya na wachezaji kuvuta sigara.
Bangi haiwekwi kwenye mawazo ya wengi jambo ambalo linashangaza hasa ukichukulia jinsi watu barani ulaya na Marekani wanavyoichukulia bangi.
Mtazamo wa wengi kuhusu bangi upo tofauti, mfano nchini Marekani ambako vita dhidi ya utumiaji wa madawa ya kulevya unavyoonekana kulipa sifa jeshi la polisi na serikali badala ya kuzuia au kupunguza matumizi ya madawa yenyewe, na nchini Uingereza na barani ulaya ambako bangi imewekwa kwenye kundi tofauti na madawa mengine.
Kama ambavyo takwimu zinavyoonyesha kuhusu mahusiano ya jinsia moja utagundua kuwa kuna wanasoka wengi ambao ni mashoga kuliko watu wanavyodhani, takwimu kuhusu matumizi ya bangi kwenye nchini za Uingereza, Uholanzi, Hispania, Ufaransa, Ujerumani na Marekani zinaonyesha kuwa asilimia 20% mpaka 35% ya watu wenye umri wa kati wamewahi kutumia bangi kwenye nchi zilizotajwa na hii itakuonyesha kuwa hata wanasoka wamewahi kutumia bangi walau kwa sababu za starehe wakiwa na umri mdogo. Takwimu hizi zinabadilika.
Ukifikiria kuwa bangi ni moja ya madawa yasiyoruhusiwa Uingereza na ushahidi wa matumizi yake unaweza kuonekana kwenye mfumo wa damu na hapa ndio wachezaji wanapoona vipimo vya kutambua watumizi wa dawa za kulevyaka na kitu cha kufadhaisha.
Hadi leo kuna tukio moja la mchezaji kukiri kuwa na tatizo la kutegemea bangi lakini unapotazama mitindo ya maisha ya wachezaji wa kisasa hakuna pingamizi kuwa wamewahi kutumia bangi katika kipindi fulani.
Cha muhimu zaidi haijalishi kama wamewahi kuvuta bangi au la , cha muhimu ni kutoruhusu bangi iathiri soka lao au jinsi wanavyocheza uwanjani(kucheza ukiwa umevuta bangi ni somo la siku nyingine tofauti kabisa).
Wakati wengi wakiwa wanapenda kuwapiga picha wachezaji wakiwa kwenye starehe zao, ukweli ni kwamba wachezaji hukamatwa wakitumia dawa za kulevya kama bangi na nyinginezo lakini huficha matukio haya wakati wakishindwa kujua kuwa kihalisia hawavunji sheria
Wanasoka na Bangi
Je tunawatambua wachezaji soka ambao huvuta bangi? Na hata kama tunawafahamu hatuwezi kufichua utambulisho wao kwa sababu za kisheria. Huwezi kuacha kujiuliza kinachoweza kuendelea pale mwanamuziki Snoop Dogg anapokutana na Rio Ferdinand au David Beckham. Haimaanishi kuwa watajwa hao wamevuta au wanavuta bangi.
Mara nyingi watu maarufu hukiri kutumia dawa za kulevya kama bangi, wachezaji huachwa nyuma kwenye mkumbo huu kwa kuwa hupenda kuficha. Hakuna ushahidi kama Matumizi ya bangi yanaweza kusaidia uchezaji wa mtu akiwa uwanjani lakini kisaikolojia yanaweza kusaidia kuondoa woga na kumsaidia mchezaji kutulia.
Hakuna matatizo kwenye kutumia bangi huku ukiwa unatazama mchezo uwanjani au nyumbani , vyanzo vingi vinaeleza kuwa mara nyingi watu “huenjoy” sana wakiwa wanatazama mchezo huku wakiwa “high” kwenye bangi au pombe.
Haijalishi kama unatazama ukiwa nyumbani au uwanjani japo kutazama uwanjani ni bora kwa wanaotumia pombe kuliko bangi.
Kwa wale wanaotazama nyumbani mara nyingi bangi hutumika nah ii husababisha shabiki kuwa na uwezo wa kupoza machungu pale timu inapopoteza mchezo.
Kwa kuwa bangi ni kinyume cha sheria kwenye maeneo mengi ulimwenguni ni rahisi kwa wengi kunywa pombe ndio kitu chepesi kufanya ukiwa nyumbani (kibiashara hiki ni kitu ambacho makampuni mengi ambayo yanatoa udhamini yanataka mashabiki wafanye). Hata kwenye nchi ambazo matumizi ya pombe yamepigwa marufuku kama Pakistan na Iran huku matumizi ya bangi yenyewe yakiruhusiwa na baadhi ya makundi ya dini bado utakuta pombe ikitumika kuliko utakavyokuta bangi.
Mfumo wa kibiashara unachangia katika hili, kuna fedha nyingi inahusika kwenye kuwashawishi watu wanywe pombe kuliko kutumia bangi.
Ni ajabu kwa jinsi watu wanavyoweza kushawishi wenzao kunywa pombe na kupata madhara ya kiafya huku wakipinga matumizi ya bangi ambayo yanaweza kuwa na madhara madogo kuliko pombe.
Uingereza inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya unywaji pombe kwa vijana hasa wa kike kuliko mahali kokote barani ulaya nah ii ni takwimu inayoelezea mustakabali wa baadaye wa vijana wa nchi za ulaya. Lakini kiukweli kuvuta bangi na kubaki kutazama mchezo wa soka nyumbani hakuna madhara.
Yote kwa yote madhara ya bangi kwa mtumiaji na wale walio karibu naye ni madogo kuliko yale yanayopatikana kwenye pombe, japo wadhamini ambao ni makampuni ya pombe hawawezi kukuonya kwenye hili,
Kucheza huku ukiwa umetumia bangi.
Kumbuka ilipoandikwa kuwa kuvuta bangi kabla ya mechi hakusaidii uchezaji ukiwa uwanjani? Hiyo ni kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa ila inapokuja soka la ridhaa mawazo hayo yanaenda mbali . Watu wengi kwenye vyuo vikuu na wanamichezo wengine wameripoti kuwa ukicheza ukiwa umevuta bangi “unaenjoy” kucheza kuliko ukiwa kawaida.
Unaweza kushindwa kucheza vizuri, na kama we ni beki au kiungo mkabaji 'tackling' zako zinaweza kuwa mbovu kuliko zile za Paul Scholes lakini utakuwa unauona mpira vizuri tu na hata baada ya kucheza raha ya kuvuta itaonekana.
Kunywa pombe kabla ya mchezo hata hivyo ni hatari kwa afya yako kuliko kawaida , na hali ni mbaya zaidi kwa wachezaji wenzio kwa kuwa hali yako ya kiakili inakuwa chini kwa kuwa umelewa na mtu akiwa amelewa huwa anafikiria katika hali isiyo kawaida (Jiulize ni watu wangapi hupigana wakiwa wamelewa au wakiwa wamevuta bangi)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
nimeipenda hii dauda kila siku bangi inaonekana kama sumu ya panya lakini powa ni dawa ya msukumo wa damu mwilini hata viongozi wanakunywa pombe yaani inaonekana iko sawa tu
ReplyDelete