Search This Blog

Sunday, November 4, 2012

LIVE MATCH CENTRE: YANGA 2-0 AZAM - MTIBWA 2-0 SIMBA

FULL TIME MOROGORO: Dakika ya 89, kipa Juma Kaseja, anafanya kosa la mwaka. Baada ya kurudishiwa mpira na Kapombe, akataka kumpiga chenga, Kisiga, lakini akashindwa na Hussein Javu akafunga bao la pili .Mpira umekwisha. Dakika ya 90.

FULL TIME TAIFA: YANGA 2-0 AZAM FC

 Taifa:Dk 90 Luhende anaangushwa ndani ya eneo la hatari la Azam, mwamuzi anapeta.

Dk 89 Yanga inaendelea kutawala mchezo na Azam inapoteza pasi nyingi. AZAM 0-2 YANGA

Dk 85 Yanga inaishambulia Azam na kwa dakika 10 Azam inapotezwa uwanjani kwani Yanga imetawala mchezo.

 Simba wanapata kona dakika ya 78, lakini haina madhara. Mwamuzi, Judith Gamba, anampatia kadi ya njao, kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif, kwa kosa la kuchelewa mpira. Dakika ya 79 sasa

Taifa: Dk 77 David Luhende wa Yanga anapiga shuti kuelekea lango la Azam, lakini kipa wa Azam, Mwadin anapangua.

Kutoka Moro: Dakika ya 70, Mtibwa inaongoza bao, 1-0

Taifa: Dk 69 GOOOO.... Hamis Kiiza anaifungia Yanga bao la pili akiunganisha krosi ya Chuji. AZAM 0-2 YANGA

Dk 62 Azam inafanya mabadiliko, anatoka Khamis Mcha amengia Abdi Kasim.

Kutoka Moro: Kwa dakika 55 sasa, walinzi wa Mtibwa, chini ya Salumu Sued wanaonekana kucheza kwa umakini na kuwabana sana washambuliaji wa Simba, Okwi na Sunzu. Bado mchezo umepooza

Taifa:  Dk 59 Azam inafanya mabadiliko, anatoka Erasto Nyoni anaingia Haji Nuhu.

Dk 56 Yanga inafanya mabadiliko, anatoka Simon Msuva anaingia David Luhende.

Dk 54 Azam inapata kona mbili langoni kwa Yanga ambazo zote zinakolewa.

 Kutoka Morogoro: Simba, wamewaingiza,Mrisho Ngassa mahali kwa Akuffor na Nassoro Chollo, ameingia mahali kwa Ochieng. Sub zote zimefanya dakika ya 45. Babuu Ally wa Mtibwa amepata ,YELLOW card, katika dakika ya 50. Sasa ni dakika ya 55 na Simba wanaonekana kushambulia zaidi kupitia, Ngassa.

 Dk 51 Erasto Nyoni anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumkanyaga Niyonzima wa Yanga.

Dk 48 Bocco anashindwa kuuwahi mpira aliopigiwa na Khamis Mcha lakini Chuji anautoa na kuwa kona. Azam inapata kona ambayo inakolewa na mabeki wa Yanga.

Kipindi cha pili kinaanza hapa uwanja wa taifa kati ya Yanga na Azam 

 Morogoro: Simba, wanajaribu kuingia katika lango la Mtibwa, lakini bado hawana mipango ya maana. Mlinzi, Amir Maftah na yule wa kulia, Kapombe, wanajaribu kutumia mipira mirefu, lakini bado haiwasaidii sana. Dakika ya 45 sasa. Mwamuzi, Judith Gamba, anampatia kadi ya njano, Daniel Akuffor, kwa kosa la kumjibu mwamuzi. Mwana Mama, huyu ameweza kuchezesha vyema kwa kipindi hiki cha kwanza.


 Taifa; Dk 45 HALF TIME..... AZAM 0-1 YANGA

 Kutoka Morogoro: Mtibwa wanapata kona tatu mfululizo, lakini, Kaseja anadaka, dakika ya 42 sasa

 Taifa: Dk 39 Yanga na Azam zinashambuliana kwa zamu na mpira unachezwa katikati sana.

Kutoka Morogoro: Mtibwa inaongoza kwa bao moja dhidi ya Simba, mfungaji Vincent Barnabas. MTBWA 1-0 SIMBA


Taifa:  Dk 32 Azam inapata kona baada ya Mbuyu Twite kuutoa mpira nje
Khamis Mcha anapiga kona lakini Bocco anautoa mpira nje.
Dakika ya 28, Akuffor, anashindwa kutumia makosa ya mlinzi wa Mtibwa ambaye alipiga pasi fupi kwa mwenzake na kuiwahi. Lakini, akiwa ndani ya sita anashindwa kuamua kufunga au kutoa pasi, na kupiga pasi mkaa iliyonaswa na mlinzi wa Mtibwa. Dakika ya 30 sasa.
Kutoka Taifa: Dk 28 Bocco anapiga shuti kali langoni kwa Yanga lakini kipa Ally Mustapha anadaka
 Dk 26 Athuman Idd Chuji anamchezea faulo Michael Bolou.
Kutoka Morogoro: Kwa dakika 20 za mwanzo, mechi bado imebalansi hakuna mashambulizi ya maana sana ambayo timu zinayaandaa. Kila timu inacheza kama haitafuti ushindi. Mara mbili, mshambuliaji, Said Mkopi wa Mtibwa amejaribu kumtoka Amir Maftah, lakini hakufanya cha maana. Emmanuel Okwi anajitahidi kuwakimbiza mabeki wa Mtibwa Sugar, lakini bado hapati, sapoti ya karibu kutoka Sunzu na Akuffor. Mtibwa, wamepiga kona nne hadi sasa, wakati,Simba, wamepata kona moja tu. Kiujumla, mchezo bado umepooza hadi sasa.
 
 Kutoka taifa: Dk 18 Niyonzima wa Yanga,anakosa bao la wazi kwa kupiga nje mpira aliopokea kutoka kwa Oscar Joshua.
Dk 15 Erasto Nyoni wa Azam anamchezea rafu Msuva 
Dk 14 Simon Msuva wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya kushindwa kuuwahi mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Dk 13 Mpira unachezwa kwa kasi sana na timu zote zinatawala kiungo
 
 Kutoka Morogoro - Kwa dakika hizi kumi za mwanzo, timu zote zinaonekana kucheza kwa kuogopana zaidi. Mtibwa, walianza kufika katika lango la Simba, kupitia kwa Shaaban Nditti. Walinzi wa Simba, Keita na Ochieng, wakamthibiti. Bado hakuna soka la kuvutia na la mipango, japo, Mtibwa, wanaonekana kucheza kitimu hadi sasa. Simba, wanapata kona ya kwanza, lakini haina madhara, dakika ya 12 
Dk 9 GOOO...... Didier Kavumbagu anaifungia Yanga bao la kwanza baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Azam. AZAM 0-1 YANGA
Kutoka taifa: DK 3 Hamis Kiiza anakosa bao la wazi kwa upande wa Yanga.
 Kutoka taifa: Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya
Azam Fc Vs Young Africans
Morogoro - Mpira umeanza hapa Morogoro - Simba wakianza kwa kasi.
Leo tunaendeza utamaduni wetu wa kuwaletea matukio muhimu yanayoendelea kwenye viwanja tofauti vya ligi kuu ya Tanzania bara - kwa siku ya leo tunawaletea matukio ya mechi mbili kubwa kati ya Azam na Yanga, na Simba dhidi ya Mtibwa.
Kutoka Morogoro - Hiki ndio kikosi cha kwanza cha Simba kinachoanza: Kaseja, Kapombe, Maftah, Keita, Ochieng, Mkude, Kiemba, Kazimoto, Sunzu, Okwi, Akuffor
Hiki ndio kikosi cha Yanga ambacho tumefanikiwa kukipata. 
1.Ally Mustapha 'Barthez'
2.Mbuyu Twite
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub 'Cannavaro'
5.Kelvin Yondani
6.Athuman Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Yaw Berko
2.Juma Abdul
3.David Luhende
4.Nurdin Bakari
5.Nizar Khalfani
6.Jeryson Tegete
7.Said Bahanunzi

3 comments:

  1. Huyu Kavumbagu huyu...wee acha tu

    ReplyDelete
  2. Ndo mara ya kwanza maishani kuiona Yanga ikishinda mechi ikiwa imecheza pasi nyingi na mpira wa burudani.................
    Walikaba mpaka mwisho kitimu.
    Pia tulinyimwa penalty ya Luhende but 3 points ni muhimu zaidi n life goes on

    ReplyDelete