Kocha wa zamani wa Zimbabwe Sunday Chidzambwa, ambaye sasa anatafuta namna ya kusafisha jina lake katika kesi ya upangaji matokeo, ameonywa na FIFA anaweza akakutana na adhabu kali zaidi ikiwa ataendelea na harakati zake za kupeleka kesi mahakamani kama alivyofanya wiki iliyopita.
Chidzambwa alifungiwa maisha na Chama cha soka cha Zimbabwe kwa kuhusika kwake na kupanga matokeo ya timu yao ya taifa kupoteza mechi kwa kudhamiria huko barani Asia katika kipindi cha kati 2007 na 2009 kwa malipo ya pesa kutoka kwa wacheza kamari wa huko Asia.
Kocha huyo wa zamani alituhumiwa kuwa ndio aliyepanga mchongo mzima kwa pamoja na Method Mwanjali wa Mamelodi Sundowns na mlinzi BidVest
Wits Thomas Sweswe, ambao nao wamefungiwa maisha.
Lakini swali la kujiuliza ikiwa Chidzambwa tayari anatumikia adhabu ya kufungiwa maisha na FIFA, je shirikisho hilo la soka ulimwenguni ambalo mamlaka yake yanaishai kwenye soka tu, litampa adhabu gani nyingine kubwa kuzidi hiyo?
anaweza kuambiwa alipe na dola 40,000 kwa kosa la kupeleka kesi mahakamani, hiyo ni mbali na adhabu ya maisha
ReplyDelete