Search This Blog

Tuesday, November 13, 2012

JAAP STAM ATOA YA MOYONI: FERGUSON ALINIUZA LAZIO TUKIWA KWENYE KITUO CHA MAFUTA

Mchezaji wa zamani Manchester United Jaap Stam ametoa siri juu ya uhamisho wake wa kuondoka Manchester United kwenda Lazio.

Mlinzi huyo wa zamani wa kati wa United na timu ya taifa ya Uholanzi amefichua kwamba kwamba Sir Alex Ferguson alimfuata kwenye kituo cha kuuza mafuta na kumwambia anauzwa kwenda Lazio.

Jaap Stam amefichua siri hiyo wakati akizungumzia autobiography yakd aliyipa jina la Head to Head.

Stam alijiunga na United mwaka 1998 kwa ada ya uhamisho ya £10.6 million lakini alikuja kuuzwa miaka 3 baadae kwenda Lazio. Alisema kwamba Sir Alex alianza kumfuatilia kinyume cha sheria akiwa bado anaichezea PSV.

Mlinzi huyo wa kidachi alikuwa kipenzi cha mashabiki pale Old Trafford, na washabiki wa klabu walishtushwa na kuondoka kwake.

 “Niligundua klabu haikuwa inanihitaji tena na walitaka niondoke. Pia walihitaji fedha. Kwa haraka kitabu changu kikaleta mjadala kwa mara nyingine tena. Kilileta mtafaruku kati yangu na kocha," Stam aliiambia Sunday Mirror.

 “Asubuhi moja nilimwambia nilivyojisikia na nikaondoka kwenye uwanja wa mazoezi. Njiani nikielekea nyumbani nikapokea simu kutoka msaidizi binafsi wa Fergie. Akaniambia kwamba Boss wake alikuwa akitaka kuongea na mie, na hapo hapo Kocha akachukua siku na kuanza kuongea.

“Ferguson alisema: ‘Upo wapi?’ “Nikajibu: ‘Nipo karibu na nyumbani kwangu, katika kituo cha mafuta.’ Ferguson akasema: ‘Nisubiri hapo!’ Akaingia kwenye gari yake na kuja mpaka nilipokuwa.

“Pale katika kituo cha mafuta akapaki gari lake na kuingia kwenye gari langu. Akaniambia kwamba inabidi niuzwe. Halafu akasema: "Tafadhali unaweza kuhamia Lazio haraka?’

“Nilikubali. Kutokea hapo kwa mazungumzo yasizidi dakika 3 tayari yalimaanisha kwamba nilikuwa naondoka kwenye ile kubwa. Ninapofikiria suala lile sasa hivi, suala ambalo sikuwahi kuzungumzia, naona ni kitu ambacho ni vigumu kuamini kwamba niliiacha kitu kinitokee kama mchezaji."

No comments:

Post a Comment