Naomba kunukuu MAADILI (CODE OF ETHICS) za IOC wao wamezivunja wazi wazi na kwa vile inaonyesha wazi wazi kwamba maisha yao yanategemea ofisi ya TOC wapo tayari kufanya lolote ili warudi, wale na waishi vizuri kwa mika mingine minne; wakidhani serikali haina mkono mrefu wala jicho lionalo mbali!!.
1). Kwa mujibu wa kitabu cha SPORTS ADMINISTRATION MANUAL lililochapishwa na Olympic Solidrity chini ya uangalizi wa INTERNATIONAL OLYMPIC COMMITTEE toleo la 2010; kuna mambo matatu ambayo mimi ninaona wazi kwamba waheshimiwa hao wamekiuka maadili ya IOC ambayo ni sambamba na maadili ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA:
(A). Dignity: Kuna vipengele sita ambavyo mimi naona vyote vimekiukwa, lakini kipengele cha 6 ambacho kinasema;
7. The Olympic parties shall guarantee the athletes conditions of safety, well-being and medical
care favourable to their physical and mental equilibrium.
care favourable to their physical and mental equilibrium.
Ninathibitisha kipengele hicho maana HAPAKUWA NA DOCTOR KTK KAMBI ILIYOWEKWA KWENYE HOSTEL YA KATIBU MKUU WA TOC!!. Ndo maana mwanariadha MUSANDUKI MUHAMED aliugua alipofika LONDON kwa kukosa matibabu ya awali ambayo angeyapata wakati akiwa mazoezini. 'Hili ni kosa ambalo limeelezewa kuwa ipo katika "read line which must not be breached"
(B). Integrity: Kuna vipengele vitano pia, lakini twende katika kipengele cha 3 ambacho kinasema; 3. "Any form of conflict of interest must be avoided".
Kipengele hicho kinajieleza vizuri na ushahidi wake ni wazi; KWAMBA, TIMU YA TAIFA LETU ILIPELEKWA NYUMBANI AMA KATIKA HOSTEL ZINAZOMILIKIWA NA KATIBU MKUU WA TOC, AMBAYE PIA NI MJUMBE WA KUDUMU WA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA, HIVYO BASI KATIBU HUYO ALITUMIA INFLUENCE YAKE KUPATA MASILAHI YATOKANANAYO NA MASHINDANO YA OLYMPICS!!. KATAA KUBALI HILINI KOSA LA JINAI HATA HAPA KWETU, AMA KWA JINA LINGINE TUNAITA "ABUSE OF POWER". MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA. PIA KATIBU HUYO MKUU ALIJILIPA MWENYEWE KWA KUJUA NI KIASI GANI KINATOLEWA KWA MAANDALIZI YA TIMU. Pia ifahamike kwamba hakuna katibu mkuu mwingine duniani wa NATIONAL OLYMPIC COMMITTEE ya nchi zaidi ya 200 duniani zinazoshiriki Olympics amediriki kupeleka timu ya taifa lake katika himaya yake ili afaidike na mapato ya moja kwa moja kutoka Olympic Solidarity.
(C). Resources: Katika section hiyo kuna vipengele vine lakini mimi niongelee vipengele 1 na 2 inayosema kwamba; 1. The Olympic resources of the Olympic parties may be used only for Olympic purposes.
2.1 The income and expenditure of the Olympic parties shall be recorded in their accounts,
which must be maintained in accordance with generally accepted accounting principles.
An independent auditor will check these accounts.
which must be maintained in accordance with generally accepted accounting principles.
An independent auditor will check these accounts.
Nawatuhumu kivipi; kwa sababu: Tumekuwa tukilalamikia mapato na matumizi kutoka kwa Olympic Solidarity na dola 100,000 kutoka India, bila kusahau dola 100,000 ambazo zilitumika kwa maandalizi ya timu(kimsingi mzee alijilipa mwenyewe) fedha ambazo BAYI NA GULAMU wanakuwa bubu pindi wanapoulizwa, pia kuna uwezekano kwamba accountant anayekagua mapato na matumizi ya TOC ni mfanyakazi/mjumbe wa TOC!!. Sasa basi ipo wapi dhana ya IOC inayotaka kuwepo kwa INDEPENDENT AUDITOR ?.
NINI KINAFUATA BAADA YA HAYO YOTE:
A fall from grace, 'Ipo siku, tena hivi karibuni BAYI ataanguka kutoka juu!!, nikimaanisha siri zake zote zitakuwa hadharani na dunia nzima itajua, na tunafahamu kuwa mataifa ya mgharibi haipendi UFISADI, na FILBERT BAYI ana sifa nzuri sana kimataifa kwani anajulikana kama "The miracle miler", ila mimi nasema laiti angelijua jinsi ambavyo heshima yake itakavyoshuka kama ile ya LANCE AMSTRONG, asingekuwa na kiburi cha kuwa kin'gan'ganizi katika uongozi bali aachie madaraka ili aonekane wa maana hadi kufa kwake!!. AMA SIVYO tayari tumeandaa sahii 2,000 za wadau ambao dunia haitawadharau, na tutatuma malalamiko yetu hadi IOC na kopi kwa Olympic Solidarity, ripoti ambayo itaipaka matope serikali sababu kuna VIGOGO WAWILI wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wamehusishwa na ripoti yetu ambayo gharama ya uchunguzi imechangiwa na wazalendo. Asishangae muda mfupi ujao akabatizwa jina la "The criminal Miler badala ya lile zuri la The miracle miler".
Yeye na hela yake SISI na uzalendo wetu na nchi yetu!!.
Mambo mengine yaliyoharibika BAYI na Gulamu walipoingia:
1). Olympic Possible ilifutwa, program ambayo ndio iliwawezesha wao kushinda medali 1980 baada ya kufadhiliwa kupitia program hiyo inayofadhiliwa na IOC kila mwaka. Je wamezi-locate hizo hela wapi?.
2). Matumizi mabaya ya PUMA na LINING ambapo hadi sasa taifa letu halina SPONSOR kutokana na Tanzania kuonekana matapeli sababu ya wawili hao ambao bora wafe kuliko kukosa uongozi TOC.
3). Zanzibar na Bara kutumiwa vibaya kwa madai "TOC INAJALI MUUNGANO", wakati huo ndo uongo wao, tangu waingie madarakani si Zanzibar wala Bara wamejengewa chochote, bali wao wamejijengea mashule, majumba ya kifahari na sasa wanaomba kura ili labda wakamilike kwa kujijengea AIRPORTS KABISA!!.
HII INASIKITISHA, INASHANGAZA, INAKATISHA TAMAA, LAITI BMT WANGETAMBUA HILO TANZANIA TUTASONGA MBELE!!.
By: Gidabuday.
NB: Niliyoyasema nimeyanukuu kutoka kwenye kitabu cha IOC, ukihitaji kopi za kurasa muhimu za kitabu hicho please be free to ask me at any time:
Nimekubali ni kweli maadili nyamevunjwa. Waondoke na kusitakiwa.
ReplyDelete