Search This Blog

Wednesday, November 14, 2012

EPISODE 2: SALVADOR CABANAS MWANASOKA ANAYEISHI NA RISASI KICHWANI




Nchi mojawapo ambayo iliweza kupambana na vita dhidi ya madawa na vurugu zake ni Colombia. Kwenye miaka 1980 na 90, nchi hiyo ilikuwa ndio sehemu inayopendwa zaidi na wauza madawa ya kulevya ambao waliyachukua maisha ya mcheza soka Andres Escobar, miongoni mwa wahanga wa wauza madawa hao.

Escobar, akiwa na miaka 27 wakati alipouliwa, alijifunga goli katika michuano ya kombe la dunia 1994 dhidi ya USA, na Colombia wakapoteza mechi na kutolewa kwenye hatua ya makundi.

Wauza madawa, inaaminika waliweka fedha nyingi kwenye kamari kwa ajili ya timu ya taifa ya Colombia kufanya vizuri, hivyo walihakikisha Escobar analipa kwa kuwapotezea fedha zao na wakamuua. Mazishi ya Escobar yaliudhuriwa na watu wapatao 120,000.


Kwa upande wa Cabanas akiwa anapigania maisha yake kwenye Hospitali ya Angeles Predregal, alipata sapoti kubwa, watu takribani 5,000 walikusanyika kwenye uwanja wa timu ya taifa na kufanya sala la kumuombea kipenzi chao, hali hiyo pia ilitokea Mexico kwenye uwanja wa Azteca.

"Najisikia faraja sana kwa mapenzi makubwa ninayopewa na watu kila ninapoenda hapa nchini Paraguay," anasema Cabanas. "Mapenzi yananisukuma sana na pia ujumbe mbalimbali ninaopokea kutoka kwa wacheza soka mbalimbali duniani, hasa kutoka kwa wachezaji ndio walionisaidia kwa kiasi kikubwa pamoja na maombi ya mashabiki."



Cabanas na Raisi wa Paraguay Fernando Lugo

Mwezi mmoja baada ya kuanza kupata nafuu alitembelewa na raisi wa Paraguay Fernando Lugo. Kabla ya kushambuliwa Cabanas  alifunga mabao 10 katika mechi 44 za Paraguay. Mjini Auancion, watu wanaamini timu ya taifa isingefungwa na Spain  kwenye robo fainali ya kombe la dunia 2010 kama angecheza. Oscar Cordozo alikosa penati amabyo kama Cabanas angeipiga angefunga, mashabiki wanasisitiza. Lakini Cabanas anakataa kukubalina na hisia hizo za mashabiki na kusema kilichotokea kilipangwa kutokea, huku akisisitiza nia yake ni kurudi kuichezea timu yake ya taifa: "Wakati tu ndio nimetoka hosptali nikawa nipo nyumbani naangalia timu yangu ta Taifa ikicheza kwenye kombe la dunia. Nilikuwa naomba itendeke miujiza nipone haraka niende kuiwakilisha nchi yangu. Sikufanikiwa wakati ule lakini sasa nashukuru mungu nimepata nafuu kabisa, ninachokitaka na kuwa fiti na kuitumikia timu yangu ya taifa. Naamini siku si nyingi wakati wangu utafikia ninachopaswa kufanya ni kuonyesha uwezo wangu tu kwa kocha."

Akiwa amezaliwa kwenye familia ya kimaskini katika eneo la Itaugua, akiwa mvulana alikuwa akiuza 'Chipa' mkate wa kiparaguay: "Ilibidi kufanya kazi bado nikiwa mdogo ili kuweza kula kila siku," - anakumbuka.
Mtu ambaye aligundua kipaji chake, kocha wa Kiargentina Mariano  Falcon, alijua Cabanas ana kipaji cha aina yake na hivyo akamchukua kinda lenye miaka 10 wakati huo na kulipeleka kwenye klabu ya de Octubre, ambapo alifunga mabao 31 katika mechi 14 wakati wa msimu wake wa kwanza na timu ya vijana ya klabu hiyo.

Magoli hayo aliyafunga ndani ya 18 na mengine mashuti ya mbali, huku akitumia miguu yote miwili. Akiwa na miaka 15, Cabanas akaanza kuichezea timu ya wakubwa, na akaisadia timu yake hiyo kufika kwenye ligi kuu ya Paraguay kwa mara ya kwanza mwaka 1997. Kwa pesa waliyopokea Octubre kwa mauzo ya Cabanas kwenda klabu ya Chile Audax Italiano 12 de Octubre walifanikiwa kujenga jukwaa kwenye uwanja wao wa Juan Pettengill.

Na alipoenda Amerika, Cabanas akijiweka kuwa moja ya namba 10 bora kabisa huko Latin Amerika na alikuwa mfungaji bora mara mbili - 2007 na 2008 katika Copa Libertadores ambalo ni kombe la mabingwa wa Amerika ya kusini.

Baada ua kupigwa risasi, madaktari walimwambia Cabanas  kwamba hatocheza kabisa soka: "Walisema itakuwa haiwezekani mie kucheza soka. Niliwaambia kwamba hawapo sahihi. Niliongea na mke wangu na wazazi wangu na nikasema nitarudi tena uwanjani. Sikuwahi kuwa na mashaka juu hilo."

Kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ikiwa na kutokana na majeruhi ya ndani aliyoyapata. "Kitu cha kwanza nilichokumbuka baada ya kuzinduka alikuwa ni bibi yangu akiongea na mie. Alifariki mwaka mmoja kabla. Aliniambia itabidi nicheze tena mpira kwa sababu watu wengi bado walikuwa wananitegemea mimi.

"Hilo lilinipa nguvu kubwa sana. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nalala nyumbanikwake kwa sababu alikuwa anakaa peke yake  na siku zote alipenda kuwa karibu na mimi. Pia kuwaona watoto wangu wawili kulinipa nguvu sana."

Cabanas anaongea huku akiwa na matumaini na nia ya kweli ya kurudi kuichezea timu ya taifa, lakini kocha wa 12 de Octubre, mdogo wake golikipa wa zamani wa Paragauay Chilavert, aitwaye Jose Luis, anasisitiza hawezi tena kuwa mchezaji yule yule aliyekuwa mwanzo. "Ukweli ni kwamba sababu za kibinadamu, na sio za kisoka. Tunataka kumsaidia aweze kuwa na kiwango kizuri, lakini haiwezekani. Huyu sio Salvador  yule wa zamani."

Changamoto kubwa aliyonayo Cabanas kwa sasa ni kuweza kupona kabisa ugonjwa wake wa kupooza upande wa kushoto. "Alipoanza kufanya mazoezi na sisi hakuweza kabisa kurusha mguu wala mkono wake wa kushoto vizuri, lakini ameendelea kuwa na maendeleo mazuri sana yanatia moyo," Chilavert anasema.

"Upande wa kushoto wa mwili wangu bado mdhaifu, bado ninahitaji mazoezi sana lakini nitapona kwa baraka za mungu. Nataka kupona kabisa niwe na uwezo wa kupiga mashuti kama nilivyokua mwanzoni." - Anaongea Cabanas 

Japokuwa kuna tatizo kubwa ambalo linaweza kuwa kikwazo kikubwa kwa Cabanas kurudi kama alivyokuwa mwanzoni, Risasi aliyonayo kichwani. "Inabidi niwe muangalifu sana wakati ninapopiga kichwa mpira ambao unasafiri kwa haraka. Inabidi nifanye niwezavyo kutuliza mpira ule na paji langu la uso kwa sababu ikiwa tofauti unaweza ukasababisha risasi iliyomo kwenye ubongo kuhama na kusababisha matatizo mengine."

Katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Club Martin Ledesma, Chilavert na makocha wenzake walipata wasiwasi mkubwa pale Cabanas alipongongana na mchezaji wa timu pinzani, lakini kwa bahati nzuri hakuguswa kichwani akasalamika na kuendelea mchezo.

Kwa sasa, Cabanas anacheza mechi za nyumbani tu tena kwa dakika 45. "Akili yake ya kucheza soka itakuwepo pale siku zote,"  anasema kocha Chilavert.
"Anacheza vizuri sana kuunganisha safu ya kiungo na ushambuliaji, lakini anacheza taratibu kidogo."
Hata hivyo kwa sasa hivi kocha Chilavert ameacha kazi yake kwenye klabu akitoa sababu kwamba mabosi wa klabu yake wanamlazimisha amuweke Cabanas kwenye timu. Wachezaji wenzie pia wamekuwa na la kusema kwamba ule uwezo wa zamani wa Cabanas bado sana kurudi. Lakini baada ya kuweza kurudi uwanjani tu, Cabanas anaamini atatisha tena kama ilivyokuwa mwanzoni. "Hakuna aliyepona kutokana na jeraha nililolipata mie. Ilikuwa miujiza ya mungu. Na mungu huyo huyo ataniwezesha muda mfupi ujao niweze kucheza dakika zote 90, na muda wowote kutoka sasa nitaanza kufunga mabao."
Akiwa amesimama kwenye mlingoti wa goli kwenye mazoezi jua linampiga kichwani tena mahala pale kwenye kovu la risasi aliyopigwa - alama ya milele atakayokaa nayo ambayo itamkumbusha tukio la usiku ule kwenye ile bar jijini Mexico. Lakini pamoja na hayo yote Cabanas hamtakii mabaya aliyempiga risasi.

Balderas, anayejulikana kama 'JJ', alienda kujificha  kwa miezi mitatu baada ya kumtundka risasi ya kichwa Cabanas. Bosi wake muuza madawa ya kulevya La Barbie alikiri kwamba alimficha Balderas kwenye  kwenye ofisi zake zilizopo karibu na mji mkuu wa Mexico, mpaka pale alipokuja kukamatwa.

Mwaka jana mwezi wa 9, Balderas alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kutumiwa dokumenti za uongo, lakini  bado anakabiliwa na mashtaka ya uingizaji silaha za magendo na jaribio la kumuua Cabanas.

"Nimemsamehe Balderas," anasema Cabanas. "Ataitumikia adhabu yake kwa kile alichofanya. Kama ambavyo mungu amenisadia mimi kuwa hapa sasa hivi, yeye ndio atamhukumu Balderas. Chochote kitakachotokea namuombea kwa mungu familia yake iwe vizuri."

Cabanas bado ana mkataba  na Club American na ana matumaini ya mbali kuweza kurudi nchini Mexico, lakini timu ilikataa kumlipa kwa miezi nane baada ya kupigwa risasi, ambo ambalo lilipelekea mkewe Maria Lorgia Alonso afungue kesi dhidi ya klabu.

Alonso anasema kwamba familia yake ilikuwa kwenye hali mbaya ya kiuchumi na hatimaye wakafikia makubaliano kwamba na American mwaka jana, ambayo yalihusisha mechi kati ya timu ya taifa ya Paraguay nchini Mexico kwa ajili ya kukusanya fedha za kumsaidia Cabanas na familia yake.

"Nilichokihitaji kutoka kwao ni ukamilishaji wa haki zangu zote zilizo kwenye mkataba ambazo ni kunilipa," anasema Cabanas. Sasa yameisha sina hasira tena juu yao."

Leo hii akiwa na afya njema japo sio sana, ameweka akili yake katika kuisadia klabu yake ya 12 de Octubre kufanikisha malengo yake  ya kupata mafanikio. "Unajua nilipoanza matibabu yangu nilikuwa naweza kusimama kwa kutumia magongo tu. Hivyo kuamka na kuweza kusimama na kucheza uwanjani kumenifurahisha sana. Nitafanya kila niwezalo niweze kuisadia klabu yangu kupanda daraja na kurudi kwenye daraja la kwanza."

Cabanas ambaye bado anakunywa dozi ya kutwa mara 3, alipewa ruhusa mwezi January kurudi dimbani na kwa haraka akawasiliana na Raisi wa klabu  ya De Octubre Luis Salinas kuandaa kurudi kwake klabu hiyo katikaUwanja wa Juan Pettengill, ambao una jukwaa moja la kuingiza mashabiki 500, mbali kabisa na ule wa Azteca nchini Mexico ambao unaingiza mashabiki 104,000 - uwanja pekee duniani kuchezwa fainali mbili za kombe la dunia.

"Ni tofauti  sana hapa," anasema. "akini hapa ni nyumbani kwetu kabisa. Ni mahala pazuri kwangu kwa sababu ndipo nilipojifunza mpira na kukuzwa kama mchezaji. Ninatoa shukrani kubwa sana kwa klabu kunipa hii nafasi. Siku zote nimekuwa kuwa mcheza soka na nina furaha sana kuanza kucheza tena ."



BY AIDAN SEIF CHARLIE

No comments:

Post a Comment