Risiti niliyopewa mara tu baada ya kukata Rufaa.
Baada ya jana Shaffih Dauda kuwasilisha rufaa kwa kamati ya uchaguzi ya TFF iliyo chini ya mwenyekiti Deo Lyatoo ya kuipinga kamati ya uchaguzi ya DRFA kuwapitisha wagombea Issack Mazwile na Muhsin Said.
MGOMBEA wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na mwakilishi wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Isaac Mazwile, amejitoa katika uchaguzi wa chama hicho uliopangwa kufanyika 12 Desemba, mwaka huu.
Gazeti la Mwananchi la leo 22 Novemba, 2012, limeandika, Mazwile ambaye jina lake lilipitishwa kuwania uongozi bila ya kufanyiwa usaili, amejitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kubanwa na majukumu ya kazi kwa muajiri wake, ambaye ni benki ya National Microfinance (NMB).
Mazwile alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya DRFA iliyo chini ya Mwenyekiti, Juma Simba ‘Gaddafi’ kuwania uongozi katika nafasi zilizotajwa hapo juu huku akiwa na amewekewa pingamizi na mgombea mwenzake (wa uwakilishi wa mkutano mkuu wa TFF), Shaffih Dauda.
Mapingamizi aliyowekewa Mazwile ni kutokuwa muadilifu katika uongozi wa soka hasa alipokuwa akiongoza katika Chama cha Soka Kinondoni (KIFA), kutokana na kitendo chake cha kumuacha mtu aliyefahamika kwa jina la Seif Ally Mailo 'Saddam' akisaini nyaraka mbalimbali za chama hicho huku akiwa hana madaraka yoyote ndani ya chama.
Pingamizi hilo, lilitupwa na viongozi wanne wa kamati ya uchaguzi ya DRFA ambao ni Makamu Mwenyekiti, Abdallah Faraji, Katibu Mkuu, Peter Hella na wajumbe Mwarami Ally Kobe na Said Rubeya. Mwenyekiti Gaddafi hakuwepo katika kikao hicho kutokana na kutingwa na mambo ya chama (CCM).
Mazwile pia, alipitishwa na kamati hiyo kuwania uongozi wa DRFA bila hata ya kuhudhuria usaili uliofanyika kwenye ukumbi wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam hivi karibuni hivyo kuibua minong’ono miongoni mwa wadau wa michezo.
Hata hivyo, Shaffih Dauda tayari alikuwa ameshawasilisha rufaa kwenye kamati ya uchaguzi ya TFF kupinga Mazwile pamoja na Muhsin kupitishwa kuwania uongozi ndani ya DRFA.
Pia Shaffih Dauda aliweka pingamizi kwa Muhsin Said kutokana na kutokuwa na elimu ya kidato cha nne. Awali Shaffih Dauda alimuwekea pingamizi Balhabou lakini kamati ya uchaguzi ilitupa pingamizi hilo kwa kumpitisha Balhabou huku ikiahidi kufuatilia vyeti vya mgombea huyo katika taasisi husika.
N.B
Shaffih Dauda jina lake halikuondolewa kwenye mchakato ila anapigania haki tu za wapenda soka!
TUENDELEE KUWA PAMOJA...........
NAONA UMEAMUA KUPAMBANA KAKA!
ReplyDeletePambana kaka maana madudu kwenye soka la bongo yamezidi. Naomba kwenye sports extra hii leo lizungumziwe zaid na zaid tupate undani wake. Hiyo risiti mbona kama magumashi?????
ReplyDeletealuta continua!
ReplyDeleteShaffih kwanza lini umeshawahi kuwa kiongozi wa klabu yoyote nchini au kuwa kiongozi wa chama gani cha soka nchini, usifikiri kuchambua mpira kwenye tv na kwenye radio ndio utaweza kuendesha soka, kama ndio hivyo basi hata Dr.Liki angekua rais wa tff, wewe bora uendelee huko huko kwenye uchambuzi wako wa mpira kwenye tv na radio
ReplyDelete