Na Baraka Mbolembole
Ligi kuu ya Tanzania Bara umeingia katika raundi ya
nane jana kwa timu kumi kucheza michezo . Simba ndiyo inaongoza ligi hiyo
hadi sasa. Ifuatayo ni tathimini na uchambuzi wa timu tano ambazo zinateka
hisia za wengi katika ligi ya msimu huu.
MATARAJIO
SIMBA SC. Miaka miwili iliyopita chini ya kocha,
Patrick Phiri walimaliza msimu pasipo kupoteza mchezo wowote, na sasa baada ya
kutwaa ubingwa msimu uliopita, kocha wa timu hii, Milovan Curkovic anaamini
kuwa timu kadhaa ni nzuri lakini anabaki na imani yake aliyojiwekea ya kutwaa
taji bila kufungwa msimu huu, Yanga, Azam, Mtibwa Sugar , Coastal Union na
Kagera Sugar zinaonekana ni timu zinazotoa ushindani mkubwa katika ligi hiyo.
UDHAIFU WA SIMBA.
Bado timu imeweka imani kubwa kwa Emmanuel Okwi ambaye kimsingi ana mchango mkubwa ndani ya timu hiyo. Haruna Moshi amedai bado hajaridhishwa na mchango wa wacheji wapya wa kulipwa, Paschal Ochieng, Kommabil Keita na Danny Akkuffor. Simba wanacheza vizuri hadi sasa lakini bado timu haina safi imara na nzuri ya ulinzi, kwa mchezo wa juzi dhidi ya Kagera walionesha kutokuwa makini huku kipa namba moja Juma Kaseja akionesha kuchoka mwili. Wataenda kucheza na Mgambo JKT jumapili hii katika uwanja wa Mkwakwani ambap walitoka kuuulalamikia kuwa si mzuri wikiendi iliyopita. Wamepoteza kujiamini na tayari wamepata sare mbili mfululizo baada ya ushindi wa mechi tano za kwanza.

AZAM FC. NI KAMA CHELSEA
Kuna timu mbili ambazo hazijapoteza michezo katika raundi saba za ligi kuu ya Tz Bara na ligi kuu England, wakati Chelsea na Manchester City zikifanya hivyo, England, Simba na makamu bingwa mtetezi Azam FC hajizafungwa katika VPL. Azam ambayo imeruhusu mabao mawili tu ilishinda katika mikoa ya Kagera na Morogoro na ilipata sare jijini Mwanza iliweza kulinda rekodi yao ya kutofungwa jijini Mbeya dhidi ya Prisons kutokana na mchezo wao wa ushirikiano tena pasipo kuwa na mchezaji staa, wachezaji wote wapo katika levo inayofanana kimchezo na kiuwajibikaji.

UDHAIFU. Japo
hawajapoteza mchezo wowote huku wakionekana kuimarika zaidi ya msimu uliopita,
Azam bado hawaonekani ni wenye kujitolea asilimia ya uchezaji wao wakati wa
mchezo, ni timu inayokata tamaa mapema. Imeshinda dhidi ya Kagera Sugar, Polisi
Moro na kupata sare dhidi ya Toto Africa na Prisons, lakini wakati
wanapokabiliwa na michezo migumu zaidi timu huonesha udhaifu wa 'team work'
tatizo ambalo liliwanyima ubingwa msimu wa 2010/11 na kuwapatia, Yanga ambayo
haikuwepo katika dalili za ubingwa hadi mechi ya tatu kabla ya ligi
kumalizikana dhidi yao ( Azam FC) mechi ambayo, Jerry Tegete alifunga mara
mbili huku aliyekuwa kipa namba moja Vladimir Niyonkuru akifukuzwa kwa madai
ya hujuma. Baada ya sare ya jana dhidi ya Prisons Azam FC imebaki ni timu
‘isiyofungika’ pamoja na Simba hadi sasa.
UTABIRI.
Wanapigania kutwaa taji la
kwanza la ligi katika msimu wake wa tano tangu kupanda daraja. Wamekuwa na
bajeti nzuri ya msimu mzima na hata wachezaji si wa kulalamika matatizo kama
wale wa timu nyingine, bado wana mtihani mkubwa wa kuwapiku KULWA na DOTTO
katika mbinu mbalimbali za kutwaa taji. Kuwa na pesa pekee haitoshi ili kuwa
juu ya Yanga na Simba na huu ndiyo mzigo uliowashinda, Moro United na hata
Prisons katika miaka ya 2002 na 2008 miaka ambayo walitakiwa kuwa mabingwa wa
haki kutokana na mchezo wao. Azam itamaliza ndani ya tatu bora na wakijipanga
vizuri wanaweza safari hii wakatimiza ndoto yao ya kutwaa taji.
No comments:
Post a Comment