Search This Blog

Friday, October 5, 2012

SUNDAY OLISEH: MWISHO WA FERGUSON MAN UNITED - NA WANAOWEZA KUMRITHI



Hakuna anayeishi milele. Kifupi hakuna kinachodumu milele. Fomu ya sasa au upungufu wa ubora wa kiwango kilichoonyeshwa hivi karibuni na Manchester United kwa mawazo ni dalili zinazoonyesha kwamba kuna vitu kadhaa vimefikia mwisho ndani ya Manchester United. Mojawapo ya vitu hivyo ni utawala wa Sir Alex Ferguson.

Kuna uwezekano kwamba kunaweza kukatokea mabadiliko ya utawala katika jiji la Manchester. Kwanza ni kutwaa ubingwa wa ligi kwa Manchster City msimu uliopita, walimaliza utani wa kuitwa "Majirani wenye kelel" kwa United kama ambavyo  Sir Alex Ferguson alivyokuwa akiwaita na kwa maoni yangu  naona huu ndio mwanzo wa mabadiliko yasiyozuilika. Kustaafu kwa Sir Alex Ferguson!

Alizaliwa 31 December 1941 - Ferguson ni mmoja wa makocha mwenye mafanikio makubwa katika historia ya mchezo huu wa soka. Amekuwepo Old Trafford tangu mwaka 1986, miaka 26 iliyopita!

Kwa kipindi chote hiki ameshinda makombe 37, kati ya hayo 12 ni makombe ya ligi kuu ya England. Maisha yake ya ukocha yalianza tangu mwaka 1976.

Kutoka wakati huo amekusanya makombe jumla 48 na ameshinda tuzo binafsi zipatazo 64 kama yeye binafsi na kama kocha. Japokuwa, unapoangalia mambo yanavyoenda pale United, kuna dalili nyingi kwamba ameanza kupoteza makali yake kama kocha na katika kuilinda heshima kubwa aliyojiwekea na mafanikio aliyoyapata, itakuwa vizuri sana kama msimu huu utakuwa wa mwisho kwake katika kufundisha soka.

KWANINI NAFIKIRI KUFANYA HIVYO KUTAKUWA NI SAHIHI

Timu ya United inazeeka na Ferguson ameendelea kuwatumia wachezaji wake wazee katika moyo wa timu, kitu ambacho mara kadhaa kimekuwa kinawagharimu points United. (Ryan Giggs, Rio Ferdinand, na hata muda mwingine Paul Scholes)

Najiuliza ni vipi Ferguson anawafanya chipukizi wenye vipaji wajisikie, kwa kukaa nje kwenye benchi kuwapisha wachezaji wazee ambao kwa mara kadhaa tumeona wakiigharimu timu. Kiukweli hili linaondoa balance kwenye timu!.

Usinifikirie vibaya, Rio, Giggs na Scholes ni magwiji walioifanyia makubwa sana timu yao, lakini kuna sababu muhimu sana inayosema kwamba muda mzuri na sahihi kustaafu soka katika ligi ya ushindani kama England ni miaka 33!

Paul Scholes bado ni mpiga pasi bora kabisa duniani, Giggs bado na ufundi wake katika kuisadia timu kwa kasi yake na ujuzi wa kuuchezea mpira na Ferdinand ambaye sasa mara kadhaa amejikuta akiwa hana kasi lakini bado ni mlinzi mzuri lakini mashabiki wa Manchester na klabu yenyewe inastahili wachezaji 11 kwa muda wote bila kuwa na matatizo ya hawa wazee.

Kwa miaka mingi United ilikuwa klabu tajiri zaidi duniani na chaguo la kwanza la wachezaji wengi, lakini sasa kwa uvamizi huu wa waarabu na warusi na fedha zao za mauzo ya nishati, wachezaji kadhaa siku za hivi karibuni wamekuwa wakizichagua City au Chelsea mbele Manchester United.
Hata kuna wakati mchezaji kipenzi wa timu hii Wayne Rooney alitaka kuhama United kwa ajili ya kwenda timu zenye uwezo wa kununua wachezaji wazuri na wenye majina!

United walipata mafanikio yao makubwa katika timu za miaka nyuma kutokana na nidhamu, umakini, mchanganyiko wa damu changa na wachezaji wakubwa ambao bado ni bora duniani waliounda timu nzuri ya ushindani. Sifa hizi zinakosekana kwenye United ya sasa na unapoangalia soka lao sasa utaliona hilo. Mfano mzuri ni soka bovu kuliko niliyoiwahi kuishuhudia United wakicheza hivi karibuni, katika mechi dhidi ya Tottenham kwenye kipindi cha kwanza, mechi ambayo mwishoni iliisha kwa vijana wa Sir Alex wakifunga na Spurs kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 23.


Mwisho wa Ferguson kwa mfano akaamua kustaafu mwishoni mwa msimu, je nani atakuwa mrithi wake.

WABADALA WANAOWEZA KUMRITHI Ni mtihani mgumu sana ambao bodi ya wakurugenzi wa Manchester United wanabidi kuutafutia majibu yake. Unaanzaje kumbadili kocha kama Sir Alex Ferguson? Lakini wapo baadhi ya vijana ambao wanatajwa kuweza kurithi nafasi ya Fergie. 

JOSE MOURINHO : The ‘Special One’ siku zote amekuwa akiweka wazi anatamani kurudi katika ligi kuu ya England na tetesi zinasema anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa Sir Alex, ingawa bado yupo kwenye mkataba na Real Madrid. Ana uwezo mkubwa wa kuongoza ambayo klabu inahitaji, lakini wasiwasi wangu pekee kwake ni  tabia yake ya kupenda kuvuta attention kutoka kwa vyombo vya habari inaweza isivumiliwe na United, lakini staili yake ya kufundisha soka la kujilinda na kucheza vizuri huku wakitaka ushindi linawafaa United.

JOSEP GUARDIOLA: Huyu kocha akiwa na Barcelona katika miaka 3 alishinda nusu ya makombe aliyoshinda Sir Alex Ferguson katika miaka 36. Sio muongeaji sana lakini ni mkali kiasi, kijana, ana nidhamu na staili yake ya kufundisha ni kumuliki mpira na kucheza soka zuri, akisisitiza kushambulia ndio njia sahihi ya kuzuia na kupata ushindi

Kitabia namuaona ndio mtu sahihi kwa Manchester United ikiwa Sir Alex Ferguson ataamua kustaafu.

KIZUIZI KINACHOWEZEKANA? Kutokujua vizuri lugha ya kiingereza. Naamini tutamuona akifundisha soka Uingereza muda mfupi ujao na ndio maana kwa sasa anaishi na familia yake jijini New York. Ni wapi sehemu nzuri unaweza kujiandaa kufundisha soka England kwa kujifunza lugha ya kiingereza kwa uwepesi zaidi ya Amerika?
Kwa Sir Alex Ferguson, naamini maisha yake baada ya United yatakuwa magumu, kwa mtu ambaye ambavyo alivyo mweledi na anayeipenda klabu ambayo amekaa nayo karibia nusu ya maisha yake, kuiacha nafasi yake ni ngumu, lakini gwiji huyu kama anataka kuondoka kwa heshima na kwa amani na furaha katika klabu ya Manchester United, naamini mwisho mwa msimu huu achukue maamuzi magumu na kuiacha United kwenye mikono ya kocha mwngine. 

Heshima kwa Sir Alex Ferguson
 *********************************************************************************
Makala hii ameandika kiungo wa zamani wa Nigeria Sunday Oliseh - akisisitza ni muda sasa Ferguson akaachia ngazi Old Trafford. Je wewe msomaji wa mtandao hu una Maoni gani? Unadhani yupo sahihi. 

No comments:

Post a Comment