Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Ed Woodward amesema kwamba listi ya watakaowania nafasi ya Fergie ipo tayari na wanaijua watu wachache sana lakini hakuna tarehe inayojulikana kuwa ndio itakuwa mwisho wa kocha Mscotland pale Theatre of Dreams.
Alisema: "Tayari tuna mtazamo wa namna mchakato mzima wa kumpata mbadala wa SAF utakavyokuwa na ni aina gani ya mwalimu tunataka na vipi tutampata huyo mwalimu.
'Lakini kila kitu kuhusu jambo hilo kipo kwenye makabati na mipango yote itakaa huko hata zaidi ya tunavyofikiria."
Majina kama Jose Mourinho na Pep
Guardiola, vilevile David Moyes, mara nyingi yamekuw yakihusishwa na kazi ya kumrithi Fergie katika klabu yenye mafanikio kuliko zote pale Uingereza, japokuwa bado haijajulikana lini babu huyo atastaafu.
Akiongea mapema mwaka huu wakati akisherehekea miaka yake yake 25 ndani ya klabu hiyo, babu mwenye miaka 70 alisema: " Sijui ni muda gani nitaweza kuwa hapalakini kama afya yangiu itaniruhusu sidhani kama miaka mingine mitatu au miwli itakuwa shida.
'Nafikiri unahitaji nguvu katika kazi hii. Nimebarikiwa kitu hicho. Nitafahamu wakati utakapofika sifurahii kazi na ikifia hatua hiyo kwa hakika nitastaafu.
No comments:
Post a Comment