Search This Blog

Thursday, October 18, 2012

MAMBO 5 CRISTIANO RONALDO ANAYOMZIDI LIONEL MESSI UWANJANII


Sihitaji kuulezea zaidi huu mjadala mpaka kufikia hapa. Ronaldo vs Messi - mjadala huu kwa sasa hauna mwisho.

Nani mchezaji bora wa dunia kwa sasa? Sijui na sitaki kuingia kwenye mjadala huu usioisha. Pointi iliyopo hapa wote wawili Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wote wana maeneo waliyo dhaifu na imara. Kila mmoja wao amebarikiwa kwa namna yake.

Uimara wa yoyote baina yao unaodhani ni muhimu kwa mafanikio ya timu yake, Ronaldo na Messi ndio wachezaji bora wa kizazi hiki na wanapaswa kupewa kila sifa kutokana na soka safi wanalotuonyesha kila wiki.

Kwa kuanzia leo ebu tumuangalia Cristiano Ronaldo ambaye wiki amekuwa na matukio mawili makubwa kuwa mwanamichezo wa kwanza kufikisha idadi ya mashabiki million 50 kwenye mtandao wa Facebook pamoja na kutimiza mechi 100 akiwa na timu ya taifa ya Ureno. Je katika mjadala wa nani mchezaji bora, ushawahi kujiuliza ni vitu gani ambavyo winga huyo wa Real Madrid anavifanya vizuri kuliko mpinzani wake? Ebu tujaribu kuchambua.

1: MBIO / KASI

 
Lionel Messi anaaminika ndio mchezaji hatari sana linapokuja suala la one on one na mabeki, lakini hamfikii Ronaldo katika suala la spidi.

Hii ni silaha kubwa ya Ronaldo inayomfanya anakuwa bora zaidi ya wenzie. Wachache sana wana mbinu kama zake za kiufundi na uwezo wa kukimbia na mpira, lakini hakuna anaweza kukimbizana na spidi ya Cristiano Ronaldo.

Hili linafanya Ronaldo awe ni hatari kubwa hasa kwenye mashambuliizi ya kushtukiza.
Wakati Messi ni hatari zaidi anapokuwa na mpira, then hakuna ubishi Cristiano Ronaldo ni hatari zaidi anapokuwa bila mpira.

2: FREE-KICKS/ ADHABU NDOGO

 
Messi amekuwa akiongeza ubora kwenye eneo hili kila anapopata nafasi ya kupiga adhabu ndogo.

Japokuwa, ikiwa nitatakiwa kumchagua mchezaji wa kupiga adhabu ndogo ya umbali wa yadi 25, hasa ikiwa katika eneo la kati kati lilotazamana na goli, kwa mimi bila shaka nitamchagua Ronaldo.

Hakuna mchezaji anayeweza kupiga mashuti kwa namna anayoweza kuipiga Ronaldo ikiwa kwa hali ya kasi na kushtukiza, ushahidi mzuri anao golikipa wa mbrazili Julio Ceaser. Ana uwezo wa kupiga mashuti ambayo mueleko wake ni danganyifu.

Pindi Ronaldo anapokwenda kuchukua mpira na kuweka kwenye eno la kupiga faulo, huku akirudi nyuma hatua zisipungua tatu na kushusha pumzi kwa nguvu, uwanja mzima unakuwa kimya na kuweka umakini kwenye miguu ya mreno huyo - hii inaonyesha ni namna gani nahodha huyu wa Ureno anavyotisha katika eneo hilo.

3: MAPAMBANO YA HEWANI


Nafikiri kwamba Lionel Messi anapata wakati mgumu kupiga mipira ya kichwa kwa sababu ndogo tu ya kimo chake cha 5'7, lakini hilo halimaanishi hawezi kuiumiza timu pinzani kwa mipira ya hewani - unabisha waulize washabiki wa Man United alichowafanya katika fainali ya UEFA mwaka 2009.

Kwa upande wa Ronaldo, akiwa na kimo cha 6'1 anaweza kupambana na karibia mabeki wote huku akiwa na wepesi wa kuruka na kupiga vichwa katikati ya mabeki hata waliomzidi urefu.

Hili ni moja ya eneo mojawapo ambalo Ronaldo anamzidi Messi kwa kiasi kikubwa.

KUZUIA / KUKABA

Wote wawili Ronaldo na Messi wanaweza kurudi nyuma na kuzia mashambulizi wakati wapinzani wanapokuwepo kwenye eneo la hatari la goli lao.

Kwa wafuatiliaji wazuri tumekuwa tukishuhudia utofauti wawili katika kukaba, kiuhalisia kutokana na umbo lake dogo Messi akiwa na kimo cha 5'7, njia sahihi yake ya kukaba bila kujipa shida na kuingilia pasi za maadui, wakati Ronaldo kutokana na maumbile yake anaweza kuweka ukuta katika upigiwaji wa adhabu ndogo, anaweza kukaba kwa kutumia kasi yake pamoja na nguvu alizonazo, na amekuwa akifanya hivyo mara tu timu yake inaposhambuliwa.

Hawatofautiani sana lakini kwa namna ambavyo tumekuwa tukiwaona, Ronaldo amedhihirisha kwamba ni mzuiaji mzuri kuliko Messi.

NGUVU


Kwa sababu tu ya maumbile ya Ronaldo alivyoumbwa na mwili wake ulivyojengeka, anakuwa na uwezo wa kufanya vitu kadhaa vizuri zaidi ya Messi.

Tofauti yao moja kubwa, Ronaldo anaweza kukufunga kwa shuti la umbali wowote kutoka katika nusu ya kiwanja na hilo mara kadhaa limekuwa likiwapa hofu magolikipa.Kwa upande wa Messi kutokana na jinsi alivyo ni vigumu kuweza kufikia uwezo wa nguvu za Ronaldo katika eneo hilo.

Messi kiuhalisi amejaaliwa zaidi ujuzi wa kumiliki mpira na touch nzuri, lakini Ronaldo ana nguvu na uwezo wa kuchezea mpira vile vile, kwa maana hiyo kutokana na nguvu alizonazo Ronaldo zinampa nafasi ya kumzidi mpinzani wake kwenye eneo lingine.

21 comments:

  1. oya unaposema ronaldo kamzidi messi kwa nguvu nakataa kabisa kwasababu messi yupo ngangari kwnye stamina.sababu huyo jamaa ronaldo anpoguswa hua anadondoka hovyo lakin messi ni mgumu

    ReplyDelete
  2. shaffih acha unazi kila siku habari za ronaldo hatuoni habari za messi mechi mbili kacheza timu ya taifa hatujaona umeweka hata habari zake mara umeweka kuwa ronardo mechi ya yake ya 100, balace kote kote sio upande mmoja tu thanks

    ReplyDelete
  3. ki ukweli messi ni bora katika timu bora na iliyo na mafundi wa hatari dats y anaogopa kuhama maana anajua atachemka 2 ingekuwa ronardo ndio katupiwa pale barca nafikiri angeweka rekordi ya magoli ambayo hayajawahi kufungwa na mchezaji yoyote yule duniani

    ReplyDelete
  4. acha unazi wa kizamani ww safi sijui shafii semaga ukweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. ukweli ni upi acha. maana ya unazi ni nini? una elimu gani ya mpira kukosoa wengine.

      huyo unayeona anafaa amecheza ligi gani tofauti na hiyo LA LIGA?

      Delete
    2. kwani wanaposema pele ni mfalme wa soka duniani, alicheza ligi gani zaidi ya kwao brazil? achilia mbali marekani alikokwenda kumalizia mpira wake. so ubora hauji kwa kucheza ligi nyingi!! messi ni bora hata kama hajacheza zaidi ya la liga

      Delete
  5. Nyinyi mnaosema shaffih aache unazi ni wapumbavu wa mwisho,hebu heshimuni mawazo ya mtu wapuuzi nyinyi kwani hamuwezi kutoanhoja ya kupinga kistaarabu mpaka mseme fulani mnazi wakati nyinyi ndio mmekalia unazi hamna hata robo ya hoja za kiuana michezo,badilikeni bana mnabore kishenzi washamba nyinyi

    ReplyDelete
  6. UNAZI UKIZIDI SANA MWISHOWE MTU HUONEKANA CHIZI. KWELI NIMEAMINI UKIPENDA CHONGO HUITA KENGEZA. SHAFIWI HUJIELEWI. VP MZEE AKILIMALI MBONA KIMYA MPAKA SA HIZI AU NJAA YAKO IMESABABISHA USHINDWE KUMFANYA LOLOTE NA MAMILIONI YAKE?

    ReplyDelete
  7. huu ni ukweli na ndio maana nakukubali kaka

    ReplyDelete
  8. someni aya ya pili ya habari hii mtamuelewa Shaffih (kila mchezaji ana udhaifu wake na yeye (Shaffih) katoa uimara wa Ronaldo dhidi ya Messi) cha kufanya sasa hivi Shaffih tupe uimara wa Messi dhidi ya Ronaldo. kwa mf. kukusanya kijiji,na umaliziaji ulioenda shule. Akhsanteni sana.

    ReplyDelete
  9. asante kaka shaffi kwa kuongea ukweli ata wakipinga uo ndio ukweli mwambie mesi aje england kwakina shawcross mabeki wenye roho mbaya tuone atakua nanguvu za kupunguza watatu kilicho kua kinambeba ronaldo pale ni speed aliyokua nayo ya kukimbizana nao yeye mwenyewe ronaldo alisha mwambia nani ukiwa england sahau swala la kutokua majerui sasa tumwite mesi

    ReplyDelete
  10. upo sahihi! ila iyo point ya kwanza mi nakataa! kwenye kasi na mbio,si tunaona kila siku messi anavofungasha tera la mabeki kama treni hafu isitoshe ana uwezo wa kupunguza mabeki na mbinu zaidi ya ronaldo!

    ReplyDelete
  11. Shafih, mi naona hao wanaotukana ni malezi mabovu ya toka kwa mama zao na elimu finyu, kwanza umeeleza kuwa leo unaangalia ubora wa CR7 dhidi ya messi, inawezekana baada ya hapo ukaeleza ubora wa messi dhi ya CR7, sasa wanacholalamika ni nini? wawe waelewa huu ujinga wa kutosoma vitu kwa umakini ndo unaigharimu nchi kuwa na VIHIYO wengi wasiojitambua. Kama sivyo hebu Mwambieni huyo paka shume wenu messi ahame ligi kama atafunga hata goli 10 kwa msimu. Mreno katulia labda wivu kwa sababu alihama MAN U? wengi ya wanaomchukia ni wapenzi wa Man u

    ReplyDelete
  12. CR is da best in da world, the guy has everythin,he is capaable of scoring from any angle with both right and left foot.

    ReplyDelete
  13. CR 7 EPL &LA LIGA MESSI ONLY LALIGA
    CR 7 ON TOP

    ReplyDelete
  14. Fala sana we shaffih dauda uchambuzi wako huwa ni wa kishabiki hauko smart kabisa wewe huna akili by the way nyie watu wa clouds fm mpompo tu we na kibonde mna upeo finyu wa mawazo mimi Arthur Minja ulie nikimbia.

    ReplyDelete