Search This Blog

Tuesday, October 30, 2012

LIONEL MESSI KIBOKO: AINGIA KATIKA TOP 10 YA WAFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE WA LA LIGA


Leo Messi ameendelea kuvunja rekodi kibao kwenye soka. Muargentina huyo ambaye alifunga mabao mawili dhidi ya Rayo Vallecano wikiendi iliyopita, amefunga jumla ya mabao 182 kwenye la liga pekee yake, hivyo amekuwa mchezaji anayeshika nafasi ya 10 kwa ufungaji wa mabao mengi katika historia ya ligi hiyo akiwa sawa na mchezaji wa zamani wa SevillaJuan Arza aliyecheza kutoka msimu wa 1943 mpaka 1959.


AMEFUNGA HAT TRICKS 13 NA AMEFUNGA MABAO MANNE MARA 2

Messi amefunga mabao 182 katika mechi rasmi za la liga 223. Tangu alipofunga goli lake la kwanza dhidi ya Albacente idadi ya magoli anayofunga mpaka mwisho wa msimu inaongezeka kila mwaka - kuanzia msimu wa 2004/05 alifunga kama ifuatavyo  6, 14, 10, 23, 34, 31 na 50 goals, kwa kila msimu mpaka sasa.

Mwaka huu baadaya mechi tisa tayari ameshatupia kambani mara 13, na ikiwa ataendelea na kasi hii atamaliza msimu akiwa anashika nafasi ya sita au saa kwa idadi ya magoli ya kufunga katika historia ya muda woteya La Liga.

Atlético Madrid na Diego Alves, ndio waliohukumiwa zaidi na Messi.

Atlético Madrid ndio timu ambayo Leo Messi ameifunga zaidi katika historia ya kuichezea Barca. Mpaka sasa ameshatupia kambani mwao mabao 15, matatu zaidi ya ya aliowafunga Racing Santander(12) na manne zaidi ya aliyowafunga Sevilla na Zaragoza. Golikipa Diego Alves ndio mnyonge wa Messi  kwani tayari ameshamfunga mabao 11 - ikiwa ni goli moja tu mbele ya Iker Casillas aliyemfunga mabao 10..

Muagentina huyu tayari ameshafunga hat-tricks 13 na mabao manne manne (quadruples) mara 2 - dhidi ya Valencia na Espanyol, mara zote kwenye msimu uliopita.

HII NDIO LISTI RASMI YA WACHEZAJI WANAONGOZA KUFUNGA MABAO MENGI KWENYE LA LIGA KWA MUDA WOTE.

 The Top-10

251 goals
Zarra (Athletic Club)

234 goals
Hugo Sánchez (Atlético, Madrid and Rayo)

228 goals
Raúl (Madrid)

227 goals
Di Stèfano (Madrid and Espanyol)

223 goals
César (Granada, Barça, Cultural and Elx)

219 goals
Quini (Sporting and Barça)

210 goals
Pahiño (Celta, Madrid and Deportivo)

195 goals
Mundo (Valencia and Alcoià)

186 goals
Santillana (Madrid)

182 goals
Messi (Barça) and Agra (Sevilla)



No comments:

Post a Comment