Mlinzi wa kati wa kutumainiwa wa klabu ya Young Africans na timu ya
Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Kelvin Yondani anaendelea vizuri mara
baada ya kuanza kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
kitengo cha mifupa MOI jijini Dar es salaam.
Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz,
Daktari wa timu ya Young Africans Dokta Suphian Juma, amesema Yondani
alipata mshtuko katika mfupa wake mkubwa, baada ya kuchezewa vibaya na
kiungo wa timu ya Simba Haruna Moshi 'Boban'.
Dr Suphian anatoa
wasi wasi wapenzi na washabiki wa Young Africans, kwamba Yondani
anaendelea vzuri na anatazamiwa kurudi dimbani baada ya wiki mbili.
'Unajua Yondani baada ya kukanygwa na Boban alipata mshituko katika
mfupa wake mkubwa mguuni, hivyo anapata matibabu ya kumrejesha katika
hali yake ya kawaida.
Katika hali ya kushangaza mwamuzi wa mchezo
huo wa watani wa jadi, Mathew Akrama alishindwa kumonyesha kadi nyekundu
Boban kwa mchezo mbaya uliopelekea Yondani kutolewa nje na kushidwa
kuendelea na mchezo.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom
iliyowakutanisha watani wa jadi wakongwe Afrika Mashariki iliishia kwa
sare ya mabao 1-1, mabao yaliyofungwa na Amri Kiemba Simba dakika ya 4
na Said Bahanunzi aliyesawazisha kwa upande wa Young Africans dakika ya
67.
Young Africans leo imeendelea na mazoezi katik uwanja wa shule
ya sekeondari ya Loyola kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya timu ya
Kagera Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya jumapili katika uwanja wa
kaitaba mjini Bukoba.
No comments:
Post a Comment