Kuwasili kwa Boris Bunjuk kama kocha mkuu wa timu ya Azam FC, ni wazi kuwa wachezaji fulani watanufaika na wengine wataathiriwa na mabadiliko hayo. Azam inaonekana kucheza katika lugha moja na hata kimpira hawatofautiani sana kiuchezaji. Himid Mao Mkami kiungo chipukizi wa timu hiyo na mtoto wa mchezaji wa zamani, wa Taifa Star, Mao Mkami. Katika uchezaji wake, Himid amejitambulisha kama kiungo mwenye nguvu, wakati Baba yake alitamba zaidi akiwa na timu za Pamba ya Mwanza na Reli ya Morogoro na kujitambulisha kama 'ball dancer' mbele ya mashabiki wa soka nchi, kwa Himid ni tofauti kabisa yeye ana miaka mitano ndani ya Azam FC na anataka kuwa shujaa wa klabu yake.
SWALI; Tuzungumzie mambo ya ufundi na mbinu, unadhani nini siri ya ninyi kuwa na ukuta mgumu kwa msimu wa pili sasa, unadhani mabeki wenu ni bora zaidi nchini au kuna cha ziada ambacho kinawafanya muwe imara, kipi hicho?
HIMID; Kwanza kabisa timu yetu ni nzuri sana kuanzia mbele katikati na nyuma, pia tuna mabeki na kipa mzuri lakin siri ya kuwa na ukuta mgumu ni wachezaj wote kujitolea 100% tunapokuwa uwanjani.
SWALI; Ninapoitazama Azam kiujumla inaonekana ni timu iliyokamilika hasa na yenye wachezaji mahiri, pamoja na ubora wenu unadhani nini ni udhaifu wenu na kipi ambacho ungependa kuwaambia wenzako kuhusu hilo la udhaifu ili mpate kuwa na matokeo bora zaidi katika ligi na michuano ya kimataifa?
HIMID; Kweli timu yetu ipo vizuri kila idara, sidhan kama kuna mapungufu sehemu yeyote kwakuwa hatujapoteza mchezo wowote hadi sasa, nafikiri tunatakiwa kupata magoli mengi zaidi ili tujiweke katika mazingira mazuri katika ligi na mashindano ya kimataifa .
SWALI; Unamzungumziaje kocha, Boris mbinu zake na malengo ya klabu vinaendana?
Coach ni mzuri pia Ana mbinu nzuri za ushindi ndiyo maana tuna matokeo mazuri kwa ligi
SWALI; Ipi silaha yako uwapo uwanjani?
HIMID; Silaha yangu ni uwezo mkubwa wa kukaba.
SWALI; Kiungo gani bora ambaye umewahi kucheza naye timu moja?
HIMID; Kiungo bora kuwahi kucheza nae ni Sureboy, ana kipaji cha hali ya juu,
SWALI; Umesema silaha yako kubwa ni uwezo wa kukaba, unadhani nini unahitaji kuongeza katika mchezo wako ili uwe bora zaidi?
HIMID; Nafikiri ni mazoez ndio nahitaji kuongeza ili niwe bora zaidi
SWALI; Sifa tano ambazo zinakufanya uwe katika kikosi cha kwanza cha Azam?
HIMID; 1. Uvumilivu,
2 kujituma,
3. Kushirikiana vizuri na wenzangu,
4. Kufuata maelekezo ya kocha,
5. Support kutoka kwa Mungu, wazazi, familia yangu na rafiki zangu
SWALI; Polisi Moro ambayo mnacheza nayo jumamosi hii, haijashinda mchezo wowote kati ya mitano iliyocheza, unafikiria itakuwa mechi ya aina gani kwani wewe unaijua vizuri Polisi?
HIMID; Mechi itakua ngumu sana, tumejiandaa vya kutosha nafikiri tutapata matokeo mazuri
SWALI; Kwa msimu huu umeshacheza michezo mingapi na umetengeneza ama kufunga mabao mara ngapi?
HIMID; Nimecheza mechi 6, sijafunga mara nyingi nakua nyuma kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi.
Swali: Unazungumziaje mwenendo wa timu nne za juu katika ligi, ni nini taswira ya ligi uionavyo hadi kufikia raundi ya kumi?
HIMID; Ushindani ni mkubwa sana kwa timu nne za juu, lakin naweza kusema ni kwa timu zote, ligi inazidi kuwa ngumu na ikifika round ya kumi ndio itazidi kuwa ngumu na ushindani utaongezeka
SWALI; Kipi kikosi bora ambacho umewahi kukichezea, ukiwa Azam au timu ya Taifa?
HIMID; Vikosi vyote vilikua bora........
SWALI; Nini mtazamo wako kuhusiana na soka la Tanzania?
HIMID; Soka la Tanzania liko vizuri, sema inahitajika jitihada za makusudi ili kuliinua zaidi
No comments:
Post a Comment