Search This Blog

Wednesday, October 31, 2012

EMMANUEL OKWI NA WACHEZAJI WENGINE WANNE WA KIGENI BORA KATIKA VPL MPAKA KWENYE RAUNDI YA 10


Ligi kuu ya Tanzania bara imefikia kwenye raundi ya 10 mpaka sasa, huku Simba wakiongoza ligi. Katika ligi kuu kuna wachezaji wengi wa kigeni wanaocheza soka la kulipwa hapa bongo, lakini ni wachache sana wanaostahili kuitwa mapro wa kweli.  www.shaffihdauda.com inakuletea top 5 ya wachezaji wa kigeni waliocheza vizuri katika kuzisaidia timu katika VPL mpaka kufika sasa.


1: EMMANUEL OKWI):
Mchezaji muhimu zaidi wa Simba msimu huu. Okwi ambaye anacheza msimu wa nne katika klabu ya Simba, ametokea kuwa jibu kubwa la klabu ndani ya uwanja kutokana na ubora wake wa kukimbia na mipira kwa kasi, kufunga mabao ya mbali, na wakati mwingine akifunga kwa mipira ya faulo ama penati. Umuhimu wake ulionekana vizuri katika mechi ya juzi hapo dhidi ya Azam akifunga mabao muhimu tena kwa uwezo binafsi, ama kwa hakika kwangu mimi naamini Okwi ndio mchezaji bora kabisa wa kutoka nje ya nchi katika ligi kuu ya VPL kwa sasa.

 
2:
KIPRE TCHECHE:
Azam FC, baada ya kufanya usajili wa wachezaji watatu wa Afrika Magharibi, wawili kutoka Ghana na mmoja kutoka , Ivory Coast. Waghana walichemsha mapema na kusema soka la Tanzania limejaa uchawi, Tchetche, ameweza kuondoa shaka kuhusu hilo miezi nane tangu Waghana hao watoe visingizio. Kinara wa mabao hadi sasa, mwenye nguvu, kasi, mfungaji na mtengenezaji muhimu wa mabao ya ' patna' wake, John Bocco. Ukitazama miongoni mwa wachezaji wote wa kigeni nchini, Tcheche anaonekana kufanya kazi yake zaidi uwanjani na si mzungumzaji wa mara kwa mara katika vyombo vya habari. Azam wanacheza kama timu moja, lakini ukiitazama kiundani zaidi, utagundua, Tcheche ni muhimu zaidi ndani ya timu hiyo kwa sasa na anashika nafasi ya pili.


3: MBUYU TWITE:
Wengi walikuwa wanasubiri kuona nini atafanya baada ya kusajiliwa kiutata na Yanga kwa staili ya kuwapora Simba. Tangu kuondoka kwa ' Kocha asiyemkubali' Tom Saintifiet, Mbuyu ameweza kutokea mchezaji muhimu zaidi kikosini Yanga, ndiye mchezaji anayeongoza kwa kulipwa mshahara wa juu kikosini, na mchango wake kuanzia mchezo wa JKT Ruvu hadi ule wa mwisho dhidi ya JKT Oljoro, jumamosi Mbuyu amekuwa akijitolea sana kikosini, Yanga. Anapocheza kama mlinzi wa pembeni utasema ' ni full back mzuri sana yule' lakini ubora wake huonekana zaidi akicheza beki ya kati. Mpigaji bora wa mipira ya adhabu katika ligi kuu Bara. Anashika nafasi ya 3.


4: JERRY SANTO:

Nafasi ya nne kwenye listi hii inamdondokea kiungo wa kati aliyekamilika katika ligi kuu, wengi walidhani, Simba ingemrudisha Mkenya huyu hasa baada ya wachezaji kadhaa muhimu kutokuwepo msimu huu, matokeo yake ameangukia Coastal Union na tayari ni bora zaidi kikosini humo. Anazuia na kushambulia kwa wakati mwafaka na wakati mwingine amekuwa akitumia nguvu nyingi katika kukaba, ni kiungo namba sita asiyependa kupiga pasi za nyuma mara kwa mara na anaweza kucheza vizuri mipira ya kulala ' tackling'. Ameshafunga mabao mawili hadi sasa katika michezo tisa ya timu yake.
 
5: ENYINNA DARRINGTON:
Nafasi ya 5 inashikwa na mshambuliaji wa Kimatifa kutoka, Nigeria. Aliweza kufunga zaidi ya mabao sita katika msimu wake wa kwanza nchini, akiwa mchezaji wa Toto Africa. Alikaribia kutua Yanga wakati wa usajili uliopita, lakini sasa yupo Kagera Sugar, ambapo ametokea kuwa mfungaji na msaidizi mzuri wa kutengeneza nafasi za kufunga kwa wenzake. Enyinna, ana kasi, nguvu na mjanja anapokuwa mchezoni, aliwasumbua sana walinzi, Juma Nyosso na Paschal Ochieng wa Simba, na hata Yanga tayari aliwaadhibu msimu uliopita alipokuwa, Toto. Kocha, Abdalah Kibadeni anamtaja mshambuliaji wake huyo kama ' Silaha namba Moja'. Mchezaji huyu anajitolea sana uwanjani na mwenye kuijali kazi yake, Themi Felix na George Kavila pia wanafanya vizuri, lakini wanaamini, Mnigeria huyo ameongeza kitu kikosini kwao, MABAO NA PASI ZA MABAO.

No comments:

Post a Comment