Mchambuzi na mwandishi wa habari za michezo Edo Kumwembe leo asubuhi ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba anaamini mchezaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea TP Mazembe kwa mafanikio, anapaswa kuwa nahodha wa timu yetu ya taifa. Je wewe kama wewe mdau wa soka una maoni gani? Unadhani Samatta anastahili kuwa nahodha wa timu ya taifa, je huu ni muda sahihi wa Samatta kupewa beji ya timu ya taifa?? Funguka. |
Tatizo la watanzania wengi,pia wakiwemo wasomi na wataalamu na wajuzi wa mambo mbalimbali,tunapenda kufanya vitu kwa kuiga wenzetu wa nje katika suala hilo wamefanyaje. Jambo ambalo tunajikuta tunaenda kinyume na mambo yanavyotakiwa kuwa kwani tunaiga mambo bila hata kuomba ushauri au kuuliza wale tunaowaiga, walifanya hivyo kwa sababu zipi? Uzoefu wa kuandika, kutazama na kuchambua soka kwa baadhi ya wanaojiita wataalamu wa soka hapa nchini, hujaribu kulaumu mwenendo wa soka la bongo,kwa reference za nje. Jambo hilo linaweza kuwa sahihi, ila je ni kwamba tunao uwezo wa kufanya hivyo?,pia hao wataalamu wana ujuzi gani na kile wanachokipigia kelele sio tu kwa experience ya kuanalia fulani hufanya hivi, bali wanaewza kama wao wakipewa jukumu hilo kutimiza kwa vitendo na wana ujuzi huo? Haya ni maswali ya kujiuliza mtu kama Edo, kwani mimi sijaona kigezo cha kutumia rejelea za wachezaji wakongwe waliocheza ulaya kama aliowataja kuwa nyenzo kuu ya kumshawishi kocha na watanzania kumpa unaodha Samata,eti ni profressional na anacheza vizuri. Je naodha wa sasa wa T -Stars hawezi jukumu hilo kwa kigezo cha kwamba anacheza ligi ya ndani? Ukweli ni kwamba uzoefu wa kuona na kutotenda sio kigezo cha msingi sana kushinikiza watendji kukifuata tena ikiwa ni hoja ya mzoefu wa kusikia na kuona wala hatendi. Tubadilike watanzania, tumuache kocha afanye kazi yake. Ndio mamabo tunayoyaona yakiwatokea makocha wengi wanaokuja kufundisha soka la bongo...kama....?
ReplyDeleteNI WAZO ZURI EDDO BUT ANGALIA PIA NA KIGEZO CHA UMRI WA MCHEZAJI HUSIKA PIA NA BUSARA ZAKE....!!!
ReplyDeleteAbsolutely true,hakika ni wakati wake kuiongoza Starz japo kwa experience ndogo alokuwa nayo...nakumbuka hata CR7 alipokabidhiwa unahodha kila mtu alistaajabu..lakini ameweza na anasonga mbele..hata SAMATA anaweza
ReplyDeletenimependa maoni na ushauri wa ndugu wa kwanza hapo juu, ila akumbuke kua wale wajuzi wa mpira hapa Tanzania haswa wale waliopata nafasi yakucheza mpira wameshindwa kabisa kusaidia kutoa maoni na ushauri kuhusu mpira hapa Tanzania, sasa kama kunatokea watu kama kina Edo na shafii mpaka wanaanzisha blog za michezo ili watanzania tupate taarifa kuhusu mwenendo wa soka la bongo na wakati mwingine kuanzisha matamasha ya mpira ambayo yameleta msisimko wa soka la bongo. watu kama sisi hujiuliza je hao waliopata nafasi ya kucheza mpira mbona hatuoni wakianzisha blogs kama hizi, je ni ukosefu wa elimu au ndo hawapati nafasi ya kuanzisha vitu kama hivi au wapo buzy na masuala mengine, sasa wakijitokeza kina Edo tuwape nafasi juu ya maoni yao, kwan tunaburudika na habar njema wanazotuletea.
ReplyDeletekwahiyo mie sioni tatizo kuhusu maoni ya Edo na namuomba aendelee kutujuza habar njema kama hizi na mie naona ndo wakati vijana wakina samatta kupewa majukumu haya ili wajue umuhimu wa kuichezea nchi yao na upendo uliopo wa kuzichezea nchi zao.
Wazo sio baya lakini nadhani Kuna vigezo au QUALITIES ZA KUWA CAPTAIN wa timu fulani ambavyo vimekaa ki-uongozi ongozi. Sasa kabla ya kuamua bora vigezo hivyo viwekwe kwanza. Ningekubali hoja moja kwa moja kama kwa mazingira yaliyopo TP mazembe, Mbwana angekuwa Kaptein kule pia. Kwa sasa nahisi bado hajakomaa kibusara kiasi cha kupewa majukumu ya kuwaongoza wenzake.
ReplyDeletethats right kwa mtu anayeona mbali! cheki Messi kapewa ukaptain now days timu ya taifa anajituma zaidi na kufunga sana! Ronaldo pia! tujifunze mazuri mabaya tunayaacha! coment ya kwanza is unthinkable reaction towards our soka! tunajifunza toka kwa mtu anayejua! je mtu asiyejua kusoma na kuandika atakuwa Mwalimu!!!!!!!!!!!!!!thats unaficha even your name! Your an enemy of Bongo soka I dare to call you that!
ReplyDeletemoja kati ya makala za michezo ambazo sipendi kuzikosa ni ile ya eddo ya kila juma nne ktkt gazeti la siku hiyo hivyo na muheshimu sana huyu mtu,
ReplyDeleteila kwa wazo la samata bado sijaona kama ni mudamuafaka kwake kuvaa bagge hiyo,na kwa hili mtawaza kumpa u-captain adam nditi,
mimi sijaelewa hapa hivi ni kigezo gani kinatumika kumpata captain wa team hasa ya taifa?!! , je ni yule anaye cheza mpira nje ya nchi, anayefunga magoli huko ughaibuni,nidhamu yake ndani na nje ya mchezo huo??
na kama hivyo ndio vigezo mbona hakuwa captain njohore,said maulid,machupa,nizal, nawengine wengi hawatoshi hapa walio wahi kucheza kwa mafanikio huko.. na kama ni kujua mpira ndio kuwa captain hebu mtazame boban, chuji,kapombe,kazimoto,javu,selembe,msuva,ngasa, cholo,mkude,domayo,razack alfan, je kwa viwango vyao hawatoshi kuwa macaptain??? nime wataja hawa kwasababu naamini wanaweza kucheza mpira nje ya nchi hii tena kwa viwango vikubwa, mbona kapewa nsajigwa amabaye hasifiki kwa soka safi?, mbona ni kaseja amabaye si kipabora hata A.mashariki?
hivi captain wa ENGAND john terry ambaye hasififik vyema ndani na nje ya uwanja, anafaa kuwa na nafasi hiyo kwa nini asiwe lampad? ambaye kwanza the way anavyo kuwa na mpira ana ku impress kumuangalia atakacho kifanya.
hii ina nikumbusha kauli ya baba wataifa; ambapo alisema walijikuta waziiga nchi za ulaya bila ya kujua wenzao walitumia akiligani kuzifanya nchi zao zipendeze hali iliowapelekea wao kuga bila kuuliza wakajikuta wanafanya mabo hovyo hovyo aliita hali hiyo ni ujinga coz lazima uwe hakika ya jambo unaloiga liliwezavipi kufanikiwa kwa kiwango hicho kwa maana hii nataka kusema tunaiga sana bila kujua kwa nini tunaiga eti kwakuwa cameroon,nigeria,senegal,ivorycost, wanafanya hivyo, mbona hatujiulizi zambia hawafanyi hivi? misri mbona hawafanyi hivi?
hivi eddo kweli unaweza kumfanisha mess na samatta? ronaldo na samatta kweli ni sawa? hawajamaa walipo sasa tunaona hata wapotoka tena kwa ushahidi wa video, sasa kaka sisi hapa kaziyetu ni kujiambia tunaweza na kujifananisha na kina neyma bila kujua tunahitaji maandalizi, leo hii samatta unaweza kupa ucaptain na asiwe kamaunavyo dhani. Don fight because u have weapons fight because u have a reasons.