Alessandro Del Piero amekiri kwamba alikataa nafasi ya kujiunga na Liverpool kwasababu ya kumbukumbu ya tukio la janga la Heysel.
Mashabiki wapatao 39 wa Juventus walifariki dunia katika tukio la Heysel mwaka 1985 katika mechi kati ya Juventus na Liverpol, na mshambuliaji huyo wa zamani wa Italy anaaminikuhamia kwenye timu hiyo ya EPL kusingeleta picha nzuri kwa washabiki wa timu yake pendwa Juventus.
“Mazungumzo na Sydney yalikuwa yameshaanza wakati Liverpool walipokuja kunihitaji, na hapo nikafikiria kilichotokea kule Heysel," aliliambia La Gazzetta dello Sport.
“Juventus na Liverpool wameweza kutengeneza mahusiano yao, lakini tukio lile la Heysel daima litakuwepo kwenye kumbukumbu za watu wengi."
Del Piero pia alizungumzia namna alivyosikitika kuondoka katika klabu ya Juventus, lakini akawasifu mashabiki wa timu hiyo kwa jinsi walivyomuaga .
“Sikuwahi kufikiria kama naweza kuja kuondoka Juventus namna hii. Sikufikiria hili miezi 18 iliyopita, japokuwa mambo yanabadilika.
“Naondoka huku nikiwa na fikra za kutosheka , ingawa, nikiwa najua kwamba nilijitoa kwa kila kitu kwa ajili ya Juventus.
"Mashabiki walinifanya nisijkie fahari sana, siku zote nilikuwa najua wananipenda lakini sikuwahi kufikiria ningekuwa maarufu hivi kwao, Gig Buffon aliwahi kuniambia ananionea wivu."
No comments:
Post a Comment