Mojawapo ya vitu vinavyochangia kushusha Perfomance ya Mchezaji au Timu inapokuwa uwanjani ni Mazingira mabovu ya Kambi pamoja na namna Wachezaji wanavyoishi katika Kambi hiyo, kwa kuendekeza Vitendo vya Starehe zilizopitiliza ama uvivu wa Mazoezi.
Katika Hali isiyokuwa ya Kawaida ni vigumu sana kuona Timu ikiperfom katika kiwango chake kilichozoeleka , wakati Mazingira ya Kambi wanayoishi hayaeleweki kwa Wachezaji wake kuendekeza Starehe zilizopitiliza huku wengine wakisahau wajibu wao.
Hivi karibuni Shirikisho la Mpira Wa miguu nchini TFF lilitangaza Vita dhidi ya Wachezaji watakaobainika kutumia BANGI ama madawa ya Kulevya, taarifa ambayo ilionekana kupokewa katika Mitazamo tofauti na Wadau mbalimbali wa Mpira wa Miguu Tanzania huku wengine wakihoji Iwapo Shirikisho hilo litaweza kutimiza ahadi hiyo .
Taarifa Hiyo ya TFF mbali na kuzua maswali mengi kwa Wadau wa Michezo nchini pia imezua hofu kubwa kwa Wadau hao kutokana na uwepo wa Taarifa ya kwamba asilimia kubwa ya Wachezaji wa Kibongo wanatumia Bangi pamoja na Madawa ya kulevya huku wengi kati yao Wakitoka katika Vilabu vikubwa na vikongwe hapa nchini.
Swali kubwa linalozuka hapa ni kwamba je TFF itaweza kupambana na nguvu ya Vilabu hivi vikongwe kwa kuwaadhibu wachezaji wake ambao wengi ni nguzo ya Timu hizo??? hilo ndilo swali ambalo hadi sasa wadau wa Mpira wa miguu Tanzania wanasubiri kuona namna sinema hiyo itakavyokuwa.
Wakati wadau wa Soka nchini wakisubiri Rungu hilo la TFF kuanza kufanya Kazi Mtandao wa www.shaffihdauda.com umepenyezewa taarifa zinazosema kuwa Mlinzi wa Kambi ya DAR YOUNG AFRICAN(Jina limehifadhiwa) ameuandikia barua nzito uongozi wa Klabu hiyo akielezea namna Wachezaji wa Klabu hiyo kongwe wanavyoisjhi kambini hapo.
Katika Barua yake Mlinzi huyo ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Wachezaji wa Klabu hiyo ikiwemo vya utumiaji wa BANGI, Pombe, pamoja na Madawa ya kulevya(UNGA)
Mlinzi huyo ameuambia Uongozi wa Klabu ya YANGA kuwa tangu alipobaini vitendo hivyo kufanyika klabuni hapo, baadhi ya Wachezaji wanaofanya Vitendo hivyo wamekuwa wakimchukia na hata wengine kupunguza ukaribu na Mlinzi huyo kama ilivyokuwa hapo awali.
Miongoni mwa Wachezaji walioelezwa kujihusisha na vitendo hivyo ni Kiungo mkabaji wa Timu hiyo ATHUMANI IDDI CHUJI, ambaye awali aliwahi kukiri kutumia Madawa ya kulevya (UNGA) na kuthibitisha kuwa kwa sasa hana mpango nayo tena.
Taarifa ya Mlinzi huyo pia imethibitisha kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa hiyo ikawa ni mojawapo ya sababu inayopelekea timu hiyo kutofanya vizuri katika baadhi ya michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania bara inayoendelea.
Taarifa hiyo imekuja wakati klabu ya YANGA inatafuta sababu zinazopelekea baadhi ya wachezaji wake kucheza chini ya Kiwango, katika mechi zilizopita za Ligi Kuu Tanzania bara,na suala lililobaki sasa ni kuangalia Klabu hiyo itafanyia vipi kazi ripoti ya Mlinzi huyo.
WEWE SHAFII MCHEZAJI KAPELEKA TARIFA KWA UONGOZI WEWE UMEZIPATAJE KAMA CYO UCHOCHEZI....?
ReplyDeleteUMESEMA KASEMA WACHEZAJI WENGI WANATUMIA MADAWA YA KULEVYA BUT UMEMTAJA CHUJI NADHANI UNA LAKO JAMBO NA CHUJI ILA TUMIA NJIA MBADALA YA KU DEAL NAYE CYO KUMCHAFUA MBONA CJAONA MAONI KUWA UMEMUHOJI CHUJI AU KIONGOZI YEYOTE AU HATA KAPTANE WA TIMU....?
ACHA UCHOCHEZI KIJANA...!!!!
sasa umeamua kumtaja CHUJI,SI Utakuwa na bifu naye au anaweza kukushtaki kwa sababu hauna ushahidi.
ReplyDeleteHEE!
ReplyDeleteMie nimekuwa nikisema mara nyingi fani ya uhandishi wa habari imevamiwa,mtu kafeli shule anakimbilia uhandishi,story haina balance,je ulimtafuta chuji kujua ukweli?je ulimtafuta kiongozi yeyote wa yanga kujua ukweli au huyo mlinzi?uhandishi ni taaluma jamani
ReplyDeleteshafii endelea na kazi unafanya kazi nzuri sana, ila watu wengi wanacomment kishabiki zaidi! big up sana
ReplyDeleteSHAFFI UNAPIGA KAZI NZURI SANA USIOGOPE BIFU WALIPUE HAO WANAO JIBUSTI NA MADAWA MAAKE SOKA LETU HALIKUI MIAKA NENDA RUDI KAMA INAWEZEKANA TAJA NA WENGINE WENGI.
ReplyDelete"PIGA KAZI BABA"