Mabingwa wa Afrika mashariki na kati, klabu ya Yanga ya Dar es Salaam leo hii imekula kichapo mabao matatu kwa nunge kutoka kwa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro.
Katika mchezo huo ambao umekuwa na matokeo hasi kwa upande wa timu ya Jangwani ulianza kwa kwa timu kusomana lakini dakika ya 11 ya mchezo akaipatia timu yake ya Mtibwa bao la kuongoza, kabla ya Juma Javu kuongeza la pili katika dakika ya 45 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na timu zikaenda mapumziko Mtibwa wakiwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili Yanga wakafanya mabadiliko kwa kuwaingiza Saimon Msuva na Stephano Mwasika kuchukua nafasi za Frank Domayo na David Luhende lakini haikusadia chochote. Dakika ya 66 akatoka Mbuyu Twitte na kuingia Didier Kavumbangu lakini mambo yaliendelea kuwa magumu kwa upande wa watoto wa Manji.
Dakika ya 77 ya mchezo alikuwa yule yule Juma Javu akaenda kumtungua golikipa Ally Mustapha Barthez goli 3 na la mwisho katika mchezo huo. Dakika ya 90 Yanga wakapata penati lakini Hamis Kiiza akashindwa kufunga na mwamuzi akapuliz kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo.
mbuyu twite naona alikuwa mchicha twite.mpira si kupompi pompi.
ReplyDeleteMwanamke unamtolea mahari mengi kumbe tasa twiteeeeeeee!
ReplyDelete