Search This Blog

Friday, September 7, 2012

MASHABIKI WA AL-AHLY WAVAMIA MAKAO MAKUU YA SHIRIKISHO LA SOKA KUPINGA LIGI KUENDELEA

Mamia ya watu walifurika makao makuu ya ofisi za shirikisho la soka la Misri jana kupinga suala la michezo ya ligi kuu ya nchi kuruhusiwa kuendelea wakati kuna kesi inayoendelea ya juu ya vifo vya mashabiki 70 waliokufa kwenye vurugu zilizjitokeza katika mchezo kati ya AL-Masry na Al Ahly.

Waandamanaji hao ambao wengi wao ni mashabiki wa Al Ahly, walilishambulia jengo la baruti na vitu vingine vya moto, anasema shuhuda wa tukio hilo.

Polisi tisa ni baadhi ya watu wanaoshtakiwa kwa kesi ya mauaji ya mashabiki 70, kesi imeanza mwezi April.

Wengi wanaamini kwamba vurugu zile zilizotokea pale Port Said zilizpangwa aidha na polisi au mashabiki waliokuwa wafuasi wa Raisi Hosni Mubarak.

Mashabiki wa Al-Ahly , ambao walihusika kwa kiasi kikubwa katika kumuondoa Mubarak madarakani, wamekitaka chama cha soka cha nchi hiyo kusimamisha mechi zote mpaka kesi itakapoisha.

No comments:

Post a Comment