Kamati ya Ligi ya Kitengo cha michezo cha CLOUDS MEDIA GROUP(Sports Xtra/Bar) iliyokutana Dar es Salaam jana (septemba 20 mwaka huu) imetoa adhabu kwa mchezaji Emmanuel Okwi na onyo kali kwa mwamuzi Judith Gamba.
Emmanuel Okwi wa Simba amefungiwa jumla ya mechi tano za Ligi Kuu na kupigwa faini ya sh. 500,000 baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu Kessy Mapande kwenye mechi hiyo namba 10.
mgawanyiko wa adhabu ya okwi upo kama ifuatavyo:mechi tatu ni kutokana na kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa JKT Ruvu na michezo miwili ni kutokana na kuwatupia mashabiki chupa ya maji.
Pia Kamati iyo imetoa onyo kali kwa mwamuzi Judith Gamba aliyechezesha mchezo namba 5 kati ya Coastal Union na JKT Mgambo.
Kanuni YA 25 ( C ) ya udhibiti wa wachezaji : Tff itadhibiti mienendo ya wachezaji kwa kuchukua hatua kama ifuatavyo.
MCHEZAJI ATAKAYETOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU KWA KOSA LA KUPIGA AU KUPIGANA ATASIMAMA KUSHIRIKI MICHEZO MITATU INAYOFUATA YA KLABU YAKE NA ATALIPA FAINI YA TSH 500,000
For this f*** u Kamati ya Ligi ya Kitengo cha michezo cha CLOUDS MEDIA GROUP(Sports Xtra/Bar)
ReplyDeleteKwa hii video how can you prove that amewarushia chupa washabiki......???? kaitupa kushoto ndio but ukutani pale pana ukuta mrefu
ReplyDeleteHii technology ya video mnaitumia vibaya sana nadhan hamna utaalam wa kuchukua the actual event nyie na simu zenu mnapiga picha yaa mtu kajaa whole screen then katupa chupa kushoto kwake... mshaamka na vifungu..nonsense...!
puce sentence, clear event shabiki gani aliyelalamika kapigwa chupa pale kiwanjani mimi mmoja wapo nilikuwepo eneo la jukwaa la simba pale chini kabisa na kwa macho yangu nimeona okwi akiitupa chupa ya maji ukutani na sio kuwapiga washabiki hapa master of this blog.s.p.t una kosea sana kwa kuweka video za kuchonganisha, jinsi tuna kuheshimu hatutarajii na wewe kama unaweza weka uvundo kwenye blog hii na ndio mana mnasema okwi kampiga kiwiko mchezaji lakini hamuoni okwi alikuwa akipigwa kiwiko na huyo huyo ikiwa refa kapiga filimbi tayari, hayo macho yenu sijui mnaangalia nini????
ReplyDeletetatizo ni waamuzi wa bongo na tff yao wote wapo kwa ajili ya manufaa yao c kwa ajili ya soka wababaishaji!!!
ReplyDeleteHapo mbona inaonekana Okwi akitupa kopo la maji (sio chupa), na mbona wala anayedaiwa kutupiwa haonekani? Kama umetosheka kunywa maji, kwa nini usiitupe kopo na masalia ya maji?
ReplyDelete