Golikipa wa timu ya taifa ya Ghana Richard Kingson amesema kwamba alikataa hongo ya $300,000 ili aweze kucheza hovyo wakati akiitumikia Ghana kwenye fainali za kombe la dunia 2006 nchini Ujerumani.
Kingson, 34, ametoa kauli hiyo akiwa kwenye kanisa la Synagogue Church of All Nations lilopo nchini Nigeria kwamba ofa iliyotolewa wakati Ghana ilipokuwa ikijiandaa kucheza dhidi ya Jamhuri ya Czech.
Aliendelea kusisitiza kwamba fedha hizo zilitolewa kwake ili kuhakikisha Czech inashinda kwa ushindi wa 2-0 - lakini alikataa baada ya mkewe kumuomba sana asikubali kufanya kitu kile kwani atajishushia sana heshima yake.
Kingson aliambia TV Emmanuel inayomilikiwa na kanisa hilo kwamba alichanganyikiwa juu ya mawazo ya kuwa na utajiri wa dola laki tatu baada ya mechi, huku ikiwa ataisadia Ghana ishinde basi angepata kiasi cha dola 30,000 tu.
"Katika kombe la dunia 2006 nchini Ujerumani, tulikuwa tunajiandaa kucheza Czech.
"Kuna mghana mmoja aliniongoza kwenda kuonana na watu fulani hivi kuchukua rushwa hiyo na alikuwa mwanamke huyu(mkewe) aliyenishauri nisichukue zile pesa. Nilikuwa nimechanganyikiwa na sikujua nini cha kufanya lakini nikampigia simu mke wangu na akaniambia: "Richard, Nakupenda sio kwa sababu ya fedha zako, hivyo huhitaji kupatwa na tamaa kwa sababu hii ofa na ukapoteza heshima yako na uaminifu."
Magoli kutoka kwa Asamoah Gyna na Sulley Muntari yaliwafanya waghana washinde 2-0.
No comments:
Post a Comment