Search This Blog

Thursday, September 6, 2012

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YANAVYOTISHIA KUMFILISI MWANASOKA NEYMAR


Hakuna ubishi juu ya kipaji alichonacho mwanasoka wa kibrazil Neymar .
Neymar kwa sasa sio tu mwanasoka anayependwa sana kuliko wote nchini Brazil, bali pia ni tumaini kubwa la kuiwezesha nchi hiyo kutwaa kombe la dunia mwaka 2014, ambalo litafanyika katika taifa hilo la bara la Amerika ya kusini.


Ameelezewa na Pele, ambaye anatajwa kama mwanasoka bora kabisa kuwahi kutokea katika historia ya mchezo huo - kuwa na mtaalam wa soka, mwenye miguu ya majaabu, huku akiwa na umri wa miaka 20. Lakini kipaji cha Neymar uwanjani ni tofauti kabisa na akili yake linapokuja suala la matumizi ya fedha. Anatengeneza fedha nyingi sana lakini anatumia karibu na chote anachoingiza.


Gari aina ya Porsche Panamer
 Ndani ya miaka miwili tu, Neymar ameripotiwa kununua jumba ambao ndani lina nyumba zingine tatu tofauti kwa $750,000 na hekalu lingine lenye thamani ya $2million - zote zikiwa kwenye eneo la pwani ya kaskazini ya jiji la Sao Paolo; pia amenunua flat yenye thamani ya $150,000 hapo hapo Sao Paolo. Amenunua gari aina ya Porsche Panamera Turbo yenye thamani kati ya $400,000 mpaka $550,000.  Pia alimpa mama wa mtoto wake mwenye umri wa miaka 18 Apartment iliyo kwenye moja ya majengo marefu pale Santos ambayo ina thamani ya $1,000,000 - huku akiwa anatoa $15,000 kwa mwezi kwa ajli ya malezi ya mtoto. Lakini kubwa kuliko ni pale aliponunua boti ya kifahari ambayo hata baadhi ya matajiri wakubwa duniani hawana - yenye thamani ya $8 million, ambayo gharama yake ya matengenezo na services kwa muda ni kiasikisichopungua $120,000 kwa mwaka.

Yatch ya Neymar
Ingawa hakuwemo kwenye listi ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi duniani ambayo ilitolewa na jarida la Forbes la Marekani mwezi wa nne mwaka huu huku nafasi ya kwanza ikishikwa na David Beckham, Neymar anarudi nyumbani kwa mwaka na mshahara wa $4million kwa mwaka kutoka Santos, kalbu yake ya kibrazil ambayo ana mkataba nayo mpaka 2014. Shukrani kwa dili za udhamini kutoka Nike ($1 million kwa mwaka) na Red Bull na dili nyingine kutoka kwenye makampuni kadhaa ya kibrazil ambayo yanamfanya Neymar apeleke benki kiasi kingine cha fedha kipatacho $4 million kwa mwaka - kwa maana hiyo ingizo lake lote kwa mwaka ni $8million. Fedha hizi ni kidogo ukilinganisha na wanasoka wengine wakubwa kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Kaka na hata Beckham , ambao wote wanatumia fedha zao vizuri sana. Kwa mfano Beckham ambayo yeye hupendelea kukodisha boti ya kifahari kwa maana ya kupunguza gharama nyingi za kununua na kuihudumia boti hiyo.

Neymar na mwanae ambaye anamgharimu zaidi ya $15,000 kwa mwezi kumlea.
Miezi kadhaa iliyopita vyombo vya habari vya Brazil vilikuwa vinapotosha na kusema kwamba Neymar anaingiza kiasi cha $18 million kwa mwaka, jambo ambalo lilikuja kuonekana sio sahihi pale alipoanza kufanya mazungumzo mapya juu ya mahitaji yake kwenye mshahara mpya na klabu yake ya Santos. Kwa maana hiyo Neymar bado hajaweza kuingiza fedha nyingi kiasi cha kuweza kununua matoi  ya kuchezea kwa matajiri kama boti za Yatch.
"Kiukweli anatumia fedha nyingi sana karibu na kile chote anachoingiza," anasema mtaalam wa mambo ya fedha wa jarida la Forbes bwana Settimi huku akisisitiza lazima klabu yake itakuwa inamsaidia kwa kumpa fedha nyingine nje ya mkataba wake. 


"Inawezekana Santos wana mkono wao kwa sababu ukiangalia matumizi yake ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita unaona kwamba ametumia zaidi ya kile alichoingiza - kuna taarifa zinasema klabu yake inampa fedha nyingi hata nje ya mkataba ili kumridhisha na kumfanya asahau kwenda barani ulaya."

Mhariri mkuu wa jarida la Forbes Kurt Badenhausen anamfananisha Neymar na Mike Tyson: " neymar ndio kwanza anakuwa na anatengeneza fedha nzuri sana.  Kama ilivyokuwa kwa Tyson ambaye nae alianza kutengeneza fedha akiwa na miaka 18 na miaka kadhaa baadae alikuwa na utajiri wa $400 million - hivi ndivyo nahisi Neymar akavyokuwa ikiwa itaacha kutumia vibaya fedha zake."


Mike Tyson akiwa kwenye kiwango cha juu, pambano lake moja alikuwa akitia ndani kiasi cha $30 million. Lakini wakati wa kipindi hicho, Tyson alinunua mahekalu, magari ya kifahari, chui wa kufuga. Mwishoni mwa mwaka 2002,  aliingia kwenye duka la kuuza vito na kununua cheni ya dhahabu yenye thamani ya $174,000 huku ikiwa imenakishiwa na almasi kiasi. Miezi nane baadae Tyson akatangaza kufulisika huku akiwa na madeni yanayofikia $23 million.


Watu wengine maarufu ni kama vile star wa NBA Antoine Walker, ambaye alitengeneza zaidi ya $110 million wakati akicheza bado, na Evander Holyfield, wote wamefilisika.


Mfano mwingine mzuri haupo mbali na yeye. Nchini Brazil mwanasoka Romario, ambaye  alikuwa mchezaji muhimu sana kwa Brazil katika fainali za kombe la dunia 1994, alikamatwa mwaka 2009  kwa kesi ya kushindwa kutoa fedha ya malezi ya mtoto. Huku akiwa na deni linalofikia $5 million.


Neymar anatakiwa kufuata mfano wa gwiji wa soka wa nchi hiyo Ronaldo De Lima ambaye aliwekeza fedha zake vizuri. Ronaldo sasa hivi anamiliki asilimia 45 za kampuni ya 9ine Sports and Entertainment  Agency, kampuni inayodili na masuala ya soka, ambapo moja ya wateja wao ni Neymar.


Shukrani kwa 9ine inayofanya vizuri sana kwenye biashara zake, Ronaldo de lima sasa ana thamani ya utajiri unaofikia $250 million. Kwa maana hiyo Neymar itabidi afuate nyayo za huyu jamaa ili aweze kuwa na mafanikio miaka kadhaa ijayo, na sio kufuata nyayo za Romario na akina Tyson.

2 comments:

  1. Wewe usionacho ndio unasema hivyo, mwenye fedha zake ndio anazitumia hivyo.Umaskini bwana, sasa wewe na fedha za Clouds hizo unataka kumpangia mtu anayepokea zaidi dollars million 8 kwa mwaka jinsi ya kutumia...aha ahaa, aha, umaskini huo.

    Mdau
    Washington

    ReplyDelete
  2. acha ujuha ndugu yangu, ww vp?, hapo amereport kwa mafans wa neymar wajue na ameongea ukweli kwan wapo wanamichezo waliobahatka kupata pesa na wakafilisika, sion tatizo hapo, ww kama unafikiri kufika washington ndio ucheke umaskin wa wenzako soon utaexpire.

    ReplyDelete