Analipwa kiasi cha €10 million kwa mwaka. Anaichezea Real Madrid. Ameshinda kila kombe la level ya vilabu. Amekuwepo kwenye top 3 ya wachezaji wa bora wa dunia mara ya nne mfululizo katika miaka mitano iliyopita. Je unadhani kuna sababu yoyote ya kumfanya Cristiano Ronaldo awe na huzuni wa kikazi pamoja na yote haya? Ronaldo alifunga mabao mawili katika ushindi wa Madrid dhidi ya Granada wikiendi iliyopita na baada ya mechi akasema "Nina huzuni na klabu inajua hilo, kwanini sikushangilia magoli. Watu wa hapa klabuni wanajua kwanini."
Money €€€
Ndio kuna tuhuma kwamba pamoja na kulipwa €10 million kwa mwaka Ronaldo bado anataka fedha zaidi. Ilikuwa ni miezi mitano tu iliyopita Ronaldo alitoa kauli kwamba anataka kusaini mkataba mpya na Real Madrid na hili lilifuatiwa na kuuambia ulimwengu wa soka kwamba anataka kumalizia mpira wake akiwa na klabu yake anayoipenda. Japokuwa amefunga mabao mengi, Madrid ikishinda la liga na kiwango chake katika kuiongoza Ureno mpaka nusu fainali ya Euro na mshambuliaji huyo thamani yake imezidi kupanda.
Ikiwa Ronaldo anataka fedha zaidi matatizo mengi yatatokea kwa Madrid kutokana na sheria ya kodi ya Spain ambayo inawapa rate nzuri wafanyakazi wa kigeni wanaolipwa zaidi. Sheria hii kwa jina lingine inajulikana kama "Beckham Law" kutokana na David Beckham kuwa mmoja ya wageni wa kwanza kuitumia vizuri sheria hiyo kufuatiwa kuanzishwa kwake mwezi June, 2005. Bila sheria hii Ronaldo anaweza kutakiwa kulipa asilimia 40 ya mkataba wowote mpya. Ronaldo anasema ana huzuni na hilo halijapokelewa vizuri nchini Hispania huku wengi wakisema huzuni yake inatokana na suala la kutaka fedha zaidi hivyo kuzidisha hasira kwa wananchi wa Spain ambao sasa wanakabiliwa na hali mbaya ya uchumi - watu 4.6 million wakiripotiwa kutokuwa na ajira.
Kufuatiwa na tuhuma kwamba hana furaha kwa sababu anataka fedha Ronaldo akatoa taarifa rasmi kupitia Twitter;
"Suala kwamba nina huzuni limeleta maneno mengi ya mchanganyiko. Ninatuhumiwa kwamba ninataka fedha nyingi zaidi, lakini siku moja itakuja kujulikana sio kwa sababu hiyo, mpaka sasa, nataka kuwapa uhakika mashabiki wa Real Madrid kwamba mapenzi yangu juu ya klabu, kujituma kwangu, matamanio yangu ya kushinda mashindano yote hayatodhuriwa na suala hili, ninajiheshimu sana na ninaheshimu Real Madrid hivyo siwezi kucheza kwa kiwango cha chini kuliko vile ambavyo naweza."
Hivyo Ronaldo anakataa kwa nguvu zote kwamba ana huzuni kwa sababu ya fedha lakini wakala wake Jorge Mendes amesema kwamba anamsapoti Ronaldo kwa sababu zake za kuwa na huzuni - na kama wengi tujuavyo anapoingia Mendes sehemu ya utata kama hii basi suala la fedha litakuwa linahusika tu. Kwa mujibu wa gazeti la kihispaniola Marca Ronaldo kwa sasa ni mcheza anayeshika nafasi ya 10 kwa mshahara anaolipwa, akilipwa nusu ya mshahara wa mwaka anaopokea Samuel Eto'o kama ambavyo utaona hapo chini. Kwa hakika Ronaldo na Mendes watakuwa wameliona hili na wanaangalia njia ya kuongezwa fedha ikiwa bado anaonekana kuwa na thamani na Madrid.
Kashushwa thamani?
Ebu tuangalie uhalisia hapa - Ronaldo inabidi apewe heshima kubwa sana, ndio Madrid wanamlipa mshahara mzurina walilipa ada ya uhamisho ilivunja rekodi £80 million kumsajili lakini kwa yote aliyoyafanyia mpaka sasa anastahili heshima na mapenzi, ikiwa hilo ndilo analotaka. Alikuwa ndio roho ya timu msimu uliopita katika ushindi wa La liga, akiifungia Madrid mabao 151 katika mechi 149 alizoichezea na anacheza vizuri katika mechi kubwa, akiwa amefunga mara tano mfululizo katika El Classico.
Inawezekana Ronaldo haoni kama anathaminiwa vya kutosha kwa sababu ya mkataba wake na inawezekana kutokana na kutoonyeshwa mapenzi na wachezaji wenzie. Baadhi ya waandishi wa Spain waliripoti kwamba Ronaldo hakujisikia vizuri Marcelo aliposema kwamba Iker Casillas anabidi ashinde tuzo ya Ballon d'Or na akamsifia sana Lionel Messi. Katika kuongezea kwenye hili Sergio Ramos alimsifia na kumpongeza sana Andres Iniesta katika kumshinda Ronaldo na kuchukua tuzo ya Mchezai bora wa Ulaya. Ronaldo anahisi kwamba ilibidi ashinde tuzo hiyo na anataka sapoti kutoka kwa wachezaji wenzake ili kuweza kufanikiwa kwenye hilo. Kutokana na hilo inaonekana kuna mgawanyiko ndani ya kikosi cha Real Madrid, ikiwa sio mara ya kwanza katika utawala wa Mourinho. Ronaldo na uhusiano wake wa karibu na bosi wake Jose Mourinho na ukweli kwamba wote wapo chini ya wakala mmoja kunaweza kukawa kunaleta mgawanyiko fulani kwa wachezaji kutokana na uwepo na hali ya upendeleo.
Akinukuliwa na Marca, mchezaji mwenzie Ronaldo Alvaro Arbeloa aliwaambia maripota katika kambi ya timu ya taifa pale Las Rozas:
"Anahitaji upendo zaidi kutoka kwa kila mtu, na hilo tunaweza kumpa. Kila mtu ana haki ya kuwa na huzuni; ni binadamukama ilivyo kwa wengine. Hana matatizo kama ya watu wengi wa Spain lakini ni sahihi kabisa na haki ya kuwa na huzuni."
Mwisho
Mchezo dhidi ya Granada ulikuwa mgumu kwa Cristiano Ronaldo kwanza kwa sababu ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya miaka saba tangu baba yake mzazi afariki dunia. Hii inaweza ikawa sababu kwanini alikuwa na huzuni lakini mwenyewe alikataa na kusema lilikuwa jambo la kikazi zaidi. Ronaldo siku zote amekuwa mtu anayependwa kuthaminiwa sana, akiwa na Manchester United alikuwa na mahusiano ya karibu na Sir Alex Ferguson na Sir Alex alijua namna ya kum-manage kijana wake na alijua alikuwa ni mchezaji ambaye alihitaji kudekezwa na kuthamniwa. Alikuwa pia na mahusano mazuri sana na wachezaji wa Manchester United na alifanikiwa sana. Akiwa kwenye kilele chake na United mwaka 2008 alikuwa hashikiki na kulikuwa hakuna mwingine kwenye ligi aliyekuwa akimkaribia, hakuwahi kushindania attention na sifa na Lionel Messi, hakuwa na wasiwasi wa kutoshinda tuzo kwa sababu ya wachezaji wa Barcelona kwa sababu alikuwa anashinda tuzo zote. Sasa akiwa na Madrid anapata shida kuweza kuwa na himaya kama aliyokuwa nayo England, hana mahusiano mazuri na wachezaji wenzie kama ilivyokuwa Old Trafford.
Pamoja na kukataa kwake Ronaldo na wakala wake kwa hakika watakuwa wanaangalia uwezekano wa kutaka ongezeko la fedha ili kuwa mchezai anayelipwa zaidi au kukaribia huko. Wanasema fedha haziwezi kukunulia furaha - sawa labda kama wewe ukiwa Ronaldo €10 million haziwezi lakini €20 million zinaweza. Hata kama ameshaelezea huzuni yake, angesema wiki moja kabla kama angekuwa nataka kuondoka? Kulisema hili sasa, wiki moja baada ya dirisha la usajili kufungwa linaashiria kwamba hahitaji kuondoka kabisa. Hivyo suala linabki kuwa kwenye njia panda kujua nini anahitaji ili aweze kuwa na furaha lakini hilo suala halihusiani na kutaka kuondoka.
Labda anataka fedha zaidi. Labda anataka upendo zaidi. Labda anataka tuzo binafsi zaidi au vinginevyo. Tutafahamu zaidi kwanini hana furaha pale Santiago Bernabeu na kuona namna Madrid inawapenda na kuwathamini mastaa wao lakini ili litakuja na gharama kubwa sana.
No comments:
Post a Comment