Hatimaye leo hii sakata la uhamisho wa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani waliosajiliwa na klabu ya Yanga na kuwekewa pingamizi na timu ya Simba limefikia mwisho baada ya wachezaji hao kuidhinishwa na kamati ya sheria, maadili na hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka TFF, chini mwenyekiti mwanasheria Alex Mgongolwa, kuichezea klabu bingwa ya Afrika mashariki na kati Dar Young Africans.
Kwa taarifa za uhakika nilizozipata kutoka ndani ya shirikisho la soka nchini ni kwamba wakati kamati ya maadili na sheria ilipokaa mkutano wa kujadili mapingamizi ya wachezaji hao ilishindikana kabisa kwa wajumbe wa kamati kufikia makubaliano juu ya hukumu ya mapingamizi hayo hasa la Kelvin Yondan na hapo ndipo ikamuuriwa kwamba zipigwe kura miongoni mwa wajumbe kuamua ni wapi mchezaji huyo akacheze msimu kati ya Yanga au Simba ambazo zote zina mkataba naye. Wajumbe wakapiga kura na hatimaye kura nyingi zikachague aidhinishwe ajiunge na Yanga.
Kwa upande wa suala la mchezaji Mbuyu Twitte liliamuariwa kwa Yanga iwalipe Simba kiasi cha $32,000 ambazo Simba walimlipa Mbuyu Twitte ajiunge nayo kabla ya Yanga kuwazidi nguvu mahasimu wao na kumtwaa mchezaji huyo huku akiwa tayari kashasaini mkataba na Simba, malipo haya yafanyike ndani ya siku 21 na baada ya hapo Twitte atakuwa huru kukipiga jangwani.
dah tanzania bwana!!,ndo kusema sheria zimewashinda kutumia!
ReplyDeleteila shaffih big up sana kaka, unaandika riport nzuri sana haineshi ubayasi,co kama wandishi wengine wa blog taarfa inajirudiarudia,hadi inaboa kusoma,ukisoma mwanzo 2 basi usiendelee marudio yanaanza,
Kama ni kweli! Basi bongo mpira haupo, hakuna asiejua Kama Tff Yanga wako wengi alafu mnapiga kura, kosa lakisheria poa Lina kura??? Mohd elhind
ReplyDeleteIssue ya usajili inaamuriwa kwa kura??? Sijawahi kusikia!! Ziko wapi kanuni na taratibu zinazotakiwa kuamua mambo kama haya, au ni mapambo tu kwenye makabati ya TFF?! Tanzania zaidi ya uijuavyo!
ReplyDeleteHAYO NDIO MAAMUZI YA KAMATI YA MATAKOLWA
ReplyDeleteHiv sisi Tanzania tumelaaniwa na nani kwa sababu kila kitu hatuwezi,elimu ndo usiseme,maendeleo ya nchi ndo basi, mpira acha kabisa, jaman sasa sheria zimewekwa za nini,kama ni kweli bora wangepga tu hizo kura toka mwanzoni,hapakua na umuhim wa kusubiria,
ReplyDeleteTukishangilia ulaya mni2ambia sio wazalendo....ss uzalendo ndo kutia sheria na kanuni mifukon halafu kupiga kura???2taishia kucheza ndo ndo tu...
ReplyDeletesheria na kanuni zipo kwa nini wafikie hatua ya kupiga kura? hii inaonyesha wazi soka letu bado pamoja na uongozi wa soka kwa ujumla umejaa siasa,,,vile vile huu usimba na uyanga ndo vinaaharibu kabisa soka letu la TZ
ReplyDeleteAnd then we wonder why Tanzania never progresses in football. Probably the most horrible and pathetic decision making ever seen in the history of football!
ReplyDeleteInasikitisha sana kama hata sheria haziheshimiwi.. dah najitoa kushabikia soka la hapa kwetu mpaka niridhike na mabadiliko.
ReplyDeleteShafii we ni mjanja sana wa kupindisha maneno. Ila ukweli unaufahamu.Kwanza suala la Twite halikuwa na utata wowote kuwa achezee wapi maana taratibu zipo na unazifahamu ila unazi wako tu.Simba wanalalamika kuwa Yondani kasajiliwa Yanga bila yanga kuongea na timu(Simba) yake kabla. Iweje haohao wamsainishe Twite bila kuongea na klabu yake kabla? waambie wanasimba wenzako ukweli kuna tatizo kwenye uongozi wenu.Simba walicholalamikakuhusu Twite ni lack of fair play si uvunjifu wa kanuni. we hujaona mara ngapi timu inaacha kufanya fair play uwanjani na hakuna anayekata rufaa?hiyo si sheria ni best practice tu.hivyo uamuzi labda suala la Yondani ndio ungelizungumzia si Twite. Na kuhusu Yondani unakumbuka mwaka jana aling'ang'ania sana kuenda yanga? uongozi wote makini ungejua tu kuwa hili lingekuja tokea huko mbele ya safari. Nasisitiza viongozi wenu wa Simba si makini.Ona Yanga akina Manji na Kifukwe wantoa hela tu wanawaachia wataalam akina bin kleb wafanye usajili sio nyie mnataka akina hans pope na rage wasajili mtachemsha tu.Naamini mngemuachia Kaborou angeweza fanya mambo ya maana kidogo. Nawaukumbusha subirini Flamu ya Ngasa mwakani maana mlikurupuka pia.
ReplyDeleteMnazi wa Yanga
katika sheria mapenzi hkn hapo sio vingozi wa simba wamekosea inaelekea wewe ndy hujui kitu shafii yuko sawa tu kama unasema shafiisimba na mahamoud zubery jee? acha uyanga wako sisi tunajua ktk mpira wa miguu sheria ndy iko mbele hapo TFF wamepepesa macho lazima wakiri mgongolwa aachie ngazi
Deletesafi sana kamati ya maadili maana mmeweka uhalali na usawa kwa mchezaji na pia ni fundisho kwa viongozi wazembe kama wa simba kujua majukumu yao ya kusimamia usajili na sio kupiga picha na mchezaji wakati hujamsajili au kumsainisha mchezaji kwa tarehe ambayo hata wewe msainishaji hujui kama utaifikia.ni mimi shabiki namba moja wa simba anayesimamia usawa mbwige
ReplyDeleteaibu sana mataaram kupiga lamri ili kupata majibu,mfano, unampeleka mkeo kupima mimba dr anaita wenzie na kupiga kula badara ya kuingia maabara na kupata majibu kitaaram.bola turudi kwenye ramli!!!
ReplyDeletemwanasheria mkongwe na wakujitigemea, amechemka hadharan.Ndio maana naogopa kuona mstakabari wa taifa hili miaka kumi au ishirini ijayo kama tutaongozwa na watu waoga kutoa maamuzi kama hawa.
carlos M
Hii ndiyo hulka ya mpira wa Tanzania. Nani anaweza akasimama akaeleza mantiki ya kikanuni ya jambo hili???. Mgongolwa?? mwanasheria aliyesajiliwa kama wakili unaweza jambo la kikanuni ukaliamua kwa kura? Hivi Mgongolwa, unaweza precedence hii ukaitumia katika kesi nyingine kama hii?? nafikiri ni aibu kwa kamati, TFF na Sisi wapenda mpira. Hivi nani ataamini kuwa maamuzi yalizingatia kanuni na si maslahi ya klabu fulani???.
ReplyDeleteMaaamuzi mengine hadi moyo unadunda. Uweledi hauruhusu mtaalam kufanya maamuzi haya. Na kamati ile ina weledi wengi. Hawa ni watu mashujaa sana kwa mapenzi ya roho zao. Maamuzi haya yanaweza kufanywa kuwa ni rejea kwenye mambo yanayofanana na hili yakijitokeza? au itaamuliwa upya kwa mtazamo tofauti ili haya yawe ni maamuzi maalum>
ReplyDeleteUshabiki tuu umewajaa, sasa hapo kura za nini wakati kila kitu kipo wazi?? Lwani sheria za usajiri zipo wazi sasa wanaangaika nini?
ReplyDeleteKama mchezaji kasaini timu mbili wakati mkataba mmoja wapo sio halali ataadhibiwa vipi??
Viongozi wa mnyama mjipange.
yote sawa tu,imetoka hiyo!nyie mtawekaje watu kwenye kamati kwa kuangalia simba na yanga tu!kama wengi wa wajumbe wangekuwa simba,ama azamu uamuzi ungekuwaje!badilisheni mfumo mzima!hata nyie waandishi mnatuboa tu,maana baadhi yenu ni dhahiri mnaonekana ni mashabiki wa hizi timu!si ajabu tungewapeleka mle na nyie mngetuharibia tu. wajumbe watoke timu zote,na sheria zifuatwe
ReplyDelete