Siku moja baada ya kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF kutoa maamuzi juu ya mapingamzi ya Simba dhidi ya wachezaji Kelvin Yondani na Mbuyu Twitte kuichezea klabu Yanga - kwa kuwaidhinisha wachezaji hao kuichezea Yanga. Leo hii klabu ya Simba imesema inafikiria hatua za kuchukua juu ya uamuzi huo wa kamati ya Alex Mgongolwa.
Kwa taarifa za kuaminika nilizozipata kutoka ndani ya uongozi wa Simba ni kwamba kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakutana usiku wa leo kujadili hatua za kuchukua huku baadhi ya wajumbe wakisema kutokana na uonevu wanaotendewa na TFF itabidi wajitoe kushiriki kwenye ligi kuu kwa sababu hawana imani na shirikisho hilo.
Simba inalalamika kwamba wachezaji wote wawili Mbuyu Twitte na Kelvin Yondan wamesajiliwa na Yanga isivyo halali. Kwa upande wa Twitte walitaka walipwe fedha zao $32,000 walizompa mchezaji huyo na akasaini nao mkataba kabla ya Yanga kuwazidi kete na kumsainisha mkataba mpya beki huyo aliyekuwa akiichezea APR ya Rwanda, na pia walitaka Twitte afungiwe kwa sababu alisaini mkataba na kalbu zote mbili kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Kwa upande wa Yondani Simba wanadai mchezaji huyo ni halali yao kwa sababu bado ana mkataba na klabu hiyo, pia wakataka Yanga iadhibiwe kwa kitendo cha kufanya mazungumzo na mchezaji ambaye bado ana mkataba na klabu yake ya zamani.
Lakini jana kamati ya kamati ya sheria, maadili, na hadhi za wachezaji ya TFF ikatoa maamuzi ya kuwaidhinisha Yondani na Kelvin Yondan kwenda Yanga, maamuzi ambayo Simba wamesema sio sahihi.
Kama ni kweli acheni hizo. Hatuwaungi mkono. Acheni tucheze mpira. Sisi tulishatarajia kuwa maamuzi yatakuwa hivyo. Hili si la kwanza. Tusonge mbele.
ReplyDeleteHAKUNA HAJA YA KUJITOA LIGI, MUHIMU HAPA NI KUWAPELEKA FIFA ILI YANGA WAFUNGIWE KUSAJILI 2 YEARS, YONDANI NA TWITE WAFUNGIWE, YANGA WANYAGANYWE POINTS ZITAKAZOTOKANA NA KUWACHEZESHA WACHEZAJI HAO KWA VILE HADI UAMUZI UNATOKA WATAKUWA TAYARI WAMESHAWACHEZESHA.
ReplyDeleteaaaaaaha! Simba bwana!
ReplyDeletePamoja na posho za bungeni na biashara zao bado simba inawanufaisha waachane na siasa hakuna mwenye jeuri ya kujitoa Viongozi wanu wanakurupuka na kuwafanya washabiki wao hamnazo, na wao wanawashangilia. THINK B4 YOU DO.
ReplyDeleterage ni msanii na simba hilo hawalijui wanamuamini sana ila ni full msanii... hebu kesho tumuulize habar ya kujenga uwanja mabwepande imeishia wapi mana yeye na kaburu wamekua wanatusanii kila siku...wametuletea beki ochieng ni mzigo tu hawataki kusikia ushauri wowote
ReplyDeleteHata Patrick Ochan Alisemwa Hivyo Hivyo Kwamba Hana Kiwango. Mchezaji Hahukumiwi Kwa Mechi Moja.
ReplyDeletecha msingi ni kuangalia kanuni za TFF na FIFA zinasemaje. Mkataba wa yondani na simba ulishabakiza siku chache kwisha hali inayoruhusu klabu zingine kuongea naye. Hivyo yanga hawana makosa. Twite ni Kwamba simba hawakufuata taratibu za kuongea na klabu ya mchezaji huyo (FC Lupopo) hivyo yanga ndio walifuata njia sahihi kwa kuongea na klabu kwa kuwa mchezaji huyo alikuwa bado na mkataba mrefu na Lupopo...... Sasa inashangaza na mtoa mada anatafuta nini anatafuta nini wakati kila kitu kiko wazi !!!!!!
ReplyDelete