Tangu tabia ya vilabu kumwaga fedha nyingi kwenye usajili ilipoanza katika madirisha ya usajili yanapofunguliwa katika misimu kadhaa iliyopita. Arsenal na Porto, vilabu viwili vikubwa sana duniani vinavyotambulika na kuwa na mashabiki duniani kote, lakini havijawahi kununua mchezaji kwa bei ya zaidi ya £20 million. Kuna sababu nyingi juu ya hili na mafanikio yao katika misimu 10-20 iliyopita, na kuna namba zenye kutoa ushahidi juu ya hilo.
Arsene Wenger siku zote amekuwa akiwafahamisha wapenzi wa Arsenal na vilabu vingine kwamba hatofanya kufuru kwenye usajili, huku akiangalia sehemu atakapopata kinda lenye kipaji lakini kwa bei rahisi. Lakini hili halijamsaidia sana linapokuja suala la kushinda vikombe katika kipindi cha miaka 7 iliyopita. Kombe lao la mwisho lilikuwa ni la FA Cup mwaka 2005, na siku zote Wenger amekuwa akilaumiwa kwa sababu ya suala hili na mashabiki wa Arsenal. Lakini kocha huyu kifaransa ameweka historia ya katika Premier League ya kuifundisha timu ambayo haikupoteza mchezo katika msimu mzima - mechi 49 kwa hesabu kamili, Man United walitibua rekodi baada ya kuwafunga kwenye mechi ya 50. Wenger ameshathibitisha kwamba anaweza kukuza vipaji vya wachezaji wa kawaida na kuwafanya kuwa mastaa, lakini kila siku amekuwa akiwauza wachezaji wake muhimu.
Player Bought For Sold For
Robin van Persie £2.75m £24m (Man United)
Alex Song £1m £17m (Barcelona)
Cesc Fabregas Free £35m (Barcelona)
Kolo Toure £150k £16m (Man City)
Samir Nasri £12.8m £24m (Man City)
Emmanuel Adebayor £7m £25m (Man City)
Total £23.7m £141m
Kama uonavyo hapo juu, Arsene anajua namna ya kutengeneza faida kupitia wachezaji vijana. Kutoka kwenye mauzo ya wachezaji hawa, tumeona wachezaji kama Jack Wilshare, Emmanuel Frimpong, Kieran Gibbs na Alex Oxlade Chamberlain wakija kwenye kikosi cha kwanza na kuanza kucheza vizuri kwenye ligi kuu. Lakini je wachezaji wataendelea kuicheza Arsenal na kuirudisha nguvu ya Gunners wa 2005 au itabaki story kama ya waliondoka.
Timu nyingine ambayo imekuwa wachezaji kwa staili ni FC Porto. Moja ya timu tatu kubwa nchini Ureno, sambamba na na Sporting Lisbon na Benfica, Porto ndio imekuwa timu iliyofanikiwa zaidi kwenye miaka ya hivi karibuni wakiwa wameshinda kombe la mabingwa wa ulaya na The Special One Jose Mourinho.
Tangu waliposhinda ubingwa wa ulaya, timu yao imekuwa na mabadiliko makubwa katika kipindi cha miaka nane iliyopita, kutoka kwa makocha, wachezaji na uongozi wa juu. Wachezaji wa daraja la juu la dunia kama Ricardo Carvalho, Hulk, Deco, na Pepe, wote wametoka Porto.
Hii ndio listi ya wachezaji wa daraja la juu waliouzwa kutoka FC Porto kwenda sehemu nyingine pamoja na mgawanyo mauzo na faida.
Player Bought For (€) Sold For (€) Profit
Carvalho free 30m (Chelsea) 30m
Paulo Ferreira free 20m (Chelsea) 20m
Deco 100k 21m (Barcelona) 20.9m
Maniche free 16m (Dynamo Moscow) 16m
Pepe 1m 30m (Real Madrid) 29m
Anderson 7m 32m (Man United) 25m
Quaresma 6m 18.6m (Inter Milan) 12.6m
Jose Bosingwa free 21m (Chelsea) 21m
Lissandro Lopez 2.3m 24m (Lyon) 21.7m
Aly Cissokho 300k 15m (Lyon) 14.7m
Bruno Alves free 22m (Zenit) 22m
Radamel Falcao 3.93 47m (Atletico Madrid) 43.07m
Hulk 5.5m 60m (Zenit) 54.5m
Total 26.13m 356.6m 330.47m
Kutokana na mauzo inaonekana Porto walipata faida kubwa sana katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, huku wakiwa na makombe 23 kibindoni (8 ya ligi, 12 FA Cup na supercup ya Ureno, 1 champions league, na makombe mawili ya UEFA Cup, kiukweli uongozi mzima wa Porto umefanikiwa sana katika kutengeneza wacheza wa daraja la juu na kuwauza kwa bei mbaya tena katika muda sahihi, tofauti na Arsenal wanauza katika wakati mbaya mwanzoni mwa msimu huku wakikosa wabadala wanaofanana na waliouzwa.
FIFA na UEFA wanaleta sheria mpya ya udhibiti wa fedha kwa vilabu, sheria ambayo inatoa ulazima kwa vilabu kutotumia zaidi walichoingiza. Kwa jinsi namba zilivyo, Arsenal na Porto wanaonyesha mfano mzuri namna ya kuiendesha klabu ya soka, kwa kuwekeza vizuri kwenye soka la vijana na kuwakuza na baadae kuwauza kwa bei nzuri kwa wanunuzi wanaowataka. Timu kama Manchester City, Chelsea, PSG wanaweza wakapata wakati mgumu sana sheria hii itakapoanza kutumika, mfano mzuri ni hivi karibuni PSG ilipotumia €140million katika soko la usajili, Chelsea walitumia kiasi cha €98million, huku vilabu vya jiji la Manchester vikitumia €64million kila mmoja.
So hata kama Arsenal wanaweza kuwa wanatania kama vile kuitwa jina "Klabu inayolisha vilabu kama Barcelona, City, na Porto nao hawana mafanikio kama ilivyokuwa zamani, sheria ya FFT itakapoanza uwekezaji mkubwa uliofanywa na vilabu hivi katika soka la vijana utawanufaisha sana Arsenal na Porto na kuwa mfano bora wa kuigwa katika soka la kisasa lilovamiwa na waarabu na warusi wenye fedha za nishati.
No comments:
Post a Comment