Makocha wa timu mbalimbali barani Afrika na waliowahi kufundisha soka barani humu, wametuma maombi ya kupata kazi ya kufiundisha timu ya taifa ya Kenya - Harambee Stars.
Kwa mujibu wa kituo cha Supersport, ukiachana na makocha Otto Pfister, Adel Amrouche, Giuseppe Dossena, Ratomir Dujovic, Goran Stevanovic na Milovan Rojavic, kocha mkuu wa klabu ya Yanga kutoka Ubelgiji Tom Saintfeit nae ametuma maombi ya kutaka kuinoa Harambee Stars.
Tom Saintfiet ambaye bado hajatimiza hata mwezi mmoja tangu aje kujiunga na Yanga anapambana kocha wa zamani Ghana ambaye aliongoza Black Stars katika michuano ya African Cup of Nations 2012 na akatimuliwa baada ya timu kuondolewa kwenye michuano hatua ya nusu fainali.
Japokuwa makocha ni wengi waliotuma maombi lakini Otto Pfitster anaonekana kuwa na nafasi kubwa kutokana na CV yake, akiwa tayari ameshazifundisha timu za Burkina Faso, DR Congo, Cameroon na Ghana. Pia tayari ameshachukua kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 na kikosi cha Ghana.
Siku ya leo ndio shirikisho la soka la Kenya (FKF) kupitia kamati kuu watawatangaza makocha waliongia kwenye kinyang'anyiro cha mwisho katika kueleka kumteua kocha mkuu wa Harambee Stars.
Kaka Shaff habari za Asubuhi!
ReplyDeleteKaka wewe kama mtaalamu wa michezo ungefanya research kabla ya kupost hii article. Inaonyesha ni jinsi gani tunapenda kukopi na kupaste bila kufanyia utafiti.
Kama utakumbuka, wakati Yanga wanafanya maongezi na kocha huyo, tayari alikuwa ametuma maombi ya kufundisha Harambee Stars....
Hii ndo Tanzania wala hata usiulize ujue virabu vyetu vya bongo viige angalau timu kama Azam angalau kidogo labda tutaendelea sio maneno bali vitendo ndo vinahitajika:
ReplyDelete