Mechi
ya kwanza ya raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 10
za Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani nchini
Morocco kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Kenya itachezwa Septemba 9
mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Tayari
Serengeti Boys chini ya Kocha Jakob Michelsen na Msaidizi wake Jamhuri
Kihwelo ikiwa na wachezaji 28 iko kambini jijini Dar es Salaam tangu
jana (Agosti 27 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoanza saa 10
kamili jioni.
Wachezaji
waliko kambini ni makipa Abdallah Bakar (Mjini Magharibi), Hamad Juma
(Azam) na Peter Manyika (JKT Ruvu). Mabeki ni Abdallah Salum (Mjini
Magharibi), Basil Seif (Morogoro), Hassan Mganga (Morogoro), Ismail
Gambo (Azam), Mgaya Abdul (Azam), Miraji Selemani (Polisi Morogoro),
Miza Abdallah (Kinondoni), Mohamed Hussein (Azam), Pascal Matagi
(Dodoma) na Paul James (Kinondoni).
Viungo
ni Farid Musa (Kilimanjaro), Hussein Twaha (Coastal Union), James
Mganda (Kipingu Academy), Mbwana Ilyasa (Simba), Mohamed Haroub
(Zanzibar), Mohamed Kapeta (Kinondoni), Mudathiri Yahya (Azam), Mzamiru
Said (Morogoro) na Selemani Bofu (JKT Ruvu).
Washambuliaji
ni Abdallah Kisimba (Mwanza), Calvin Manyika (Rukwa), Dickson Ambunda
(Mwanza), Joseph Lubasha (Azam), Kelvin Friday (Azam) na Salvatory
Nkulula (Kipindu Academy).
Mechi
ya marudiano itachezwa jijini Nairobi, Kenya kati ya Septemba 21, 22 na
23 mwaka huu. Timu itakayofanikiwa kusonga mbele itacheza raundi ya
pili dhidi ya Misri. Mechi ya kwanza itachezwa nyumbani kati ya Oktoba
12, 13 na 14 mwaka huu wakati ya marudiano itakuwa kati ya Oktoba 26, 27
na 28 mwaka huu.
Misri
ni kati ya timu 17 zilizoingia moja kwa moja raundi ya pili. Nyingine
ni Afrika Kusini, Algeria, Burkina Faso, Cameroon, Congo Brazzaville,
Cote d’Ivoire, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Mali, Rwanda, Senegal,
Sierra Leone, Tunisia na Zambia.
No comments:
Post a Comment